Aquaculture And Agriculture Service for Conservation

Aquaculture And Agriculture Service for Conservation A.A.S provide enviromental sustainable skills for aquaculture and agriculture to society by conducti

This page was created to provide, hear and share the important knowledge, news and updates conducted by A.A.S in various regions of Tanzania.

Join our  hands together to show our passion with the nature,early in the morning on 5th June  2022 at  PANGANI,along se...
06/06/2022

Join our hands together to show our passion with the nature,early in the morning on 5th June 2022 at PANGANI,along sea side and Panga deco beach, 300 trees(casuarina spp.) has been planted and beach has been cleaned while celebrating international environmental day.

#
cleaning #
#
for trees Tanzania #
District Council #
Coastal community Network #
and agriculture service for conservation #
BMUS (community) #

Thanks for your cooperation to save our earth.

A.A.S INAPENDA KUTOA PONGEZI ZA DHATI  KWA MHESHIMIWA RAIS  MAMA SAMIA SULUHU HASSAN KWA KUTIMIZA MWAKA WA UONGOZI WAKE.
22/03/2022

A.A.S INAPENDA KUTOA PONGEZI ZA DHATI KWA MHESHIMIWA RAIS MAMA SAMIA SULUHU HASSAN KWA KUTIMIZA MWAKA WA UONGOZI WAKE.

SHUGHULI ZA UTENGENEZAJI ZANA HALALI ZA UVUVI AINA YA MADEMA ZAWA CHANZO MBADALA CHA MAPATO  KATIKA KIJIJI CHA STAHABU W...
05/03/2022

SHUGHULI ZA UTENGENEZAJI ZANA HALALI ZA UVUVI AINA YA MADEMA ZAWA CHANZO MBADALA CHA MAPATO KATIKA KIJIJI CHA STAHABU WILIAYANI PANGANI MKOANI TANGA:

JUHUDI ZA KUPIGA VITA UVUVI HARAMU KWA NJIA SHIRIKISHI YA JAMII YAANZA KUZAA MATUNDA: Wanakijiji wa kijiji cha Stahabu Wilayani Pangani Mkoa...

HAWA NI NANI NA WANAFANYA NINI? Hawa ni BMU ya kijiji cha Stahabu,kijiji kimojawapo kati ya vijiji vya wilaya ya Pangani...
15/02/2022

HAWA NI NANI NA WANAFANYA NINI?
Hawa ni BMU ya kijiji cha Stahabu,kijiji kimojawapo kati ya vijiji vya wilaya ya Pangani mkoani Tanga.
Hawa ni miongoni mwa wale wachache wanao pata elimu ya uhifadhi na kuitekeleza kwa vitendo.

Je ni furaha iliyoje tunapoona muitikio mzuri kwa jamii zetu k**a hizi zikitimiza haya kwa vitendo bila ya shuruti na malipo yeyote kwa faida ya wengi?

Bila shaka na dhahiri inatia faraja na kufurahisha.

Je mambo haya yanaweza kuwa endelevu kwenye jamii?

Mambo hayanaweza kuwa endelevu kwa jamii kwa kuhakikisha yafuatayo:

1.nivizuri ziungwe mkono mapema ili kuhakikisha juhudi zao zinakuwa endelevu kwa namna moja ama nyingine (mfano:kwa kupatiwa vifaa vya kufanyia kazi hizo kwa ufasaha zaidi,pia vifaa hivyo viweze kutumimika pia kuingiza kipato kwao k**a njia mbadala ya kuwaingizia kipato wakati wanapofanya shughuli hizi fukweni na hata mitaani).

2.Pindi vinapotokea vikundi k**a hivi basi vipewe kipaumbele kwenye kupata fursa mbalimbali (mfano: tenda za kazi za usafi hususani kwenye taasisi zetu mbalimbali kwa malipo ,hii itasaidia k**a motisha kwao na pia kuwaingizia kipato )

3.Elimu za uhifahi za mara kwa mara ziwafikie bila kusahau miradi ya maendeleo ya kiuhifadhi.

Huyu ni pweza,moja kati ya viumbe wapatikanao katika bahari ya hindi.Pweza wamekuwa ni moja kati ya zao la bahari lenye ...
06/01/2022

Huyu ni pweza,moja kati ya viumbe wapatikanao katika bahari ya hindi.
Pweza wamekuwa ni moja kati ya zao la bahari lenye soko sana,yaani soko la ndani na la nje pia,wamekuwa wakipendwa na kununuliwa sana na wenyeji pia na wageni hususani watalii.

Hali hii imepelekea uvunwaji mkubwa na kusababisha uhitaji mkubwa wa viumbe hawa.

Chakusikitisha zaidi idadi kubwa ya jamii zetu za pwani bado hatujajua kuwa pweza sasa anapungua kwa kasi sana kitokana na matumizi kuwa makubwa ukilinganisha na uzalianaji na ukuaji wake.

Pweza hupendelea kuishi kwenye miamba ipatikanayo baharini, kwa wastani pweza hutumia miezi mitatu na kuendelea katika ukuaji wake mpaka kufikia hali ya ukomavu unaofaa kuingizwa sokoni na kuuzika.
Uvuvi wa pweza usiozingatia uhifadhi endelevu wa mazingira ya bahari hususani miamba wanayopendelea kuishi pweza imezidi kuwa tatizo na hatarishi kwa maisha ya pweza kwaani umesababisha uharibifu mkubwa wa miamba na nyumba za pweza na kupelekea idadi ya pweza kupungua katika pwani yetu.

Juhudi mbali mbalimbali za uhifadhi na urejesheaji wa makazi ya asili ya pweza umeanza kufanyika kwa kasi na wadau mbalimbali k**a vile secta binafsi,NGOs ,Wizara na Serikali kwaujumla zikipokelewa kwa moyo na jamii za pwani yetu ya Tanga,Zanzibar na Kilwa.

Wananchi wa kijiji cha Ushongo wilayani Pangani mkoani Tanga wamekuwa mfano na Kivutio kwa vijiji jirani na kwa wadau mbalimbali kwa kuonyesha mfano wa uhifadhi wa Pweza kwa vitendo wakishirikiana na taasisi mbalimbali ikiwemo taasisi binafsi na Serikali kwa kuanzisha zoezi la kufungia shughuli za uvuvi kwa miamba ya pweza kwa muda wa miezi mitatu katika maeneo yao ili kupisha uzalianaji na ukuaji wa pweza kwa haraka na kwa wingi katika maeneo yao.

Hii inapelekea wao kupata pato jingi na lenye uwezo wa kushindana na soko mara tu baada ya miezi mitatu ya uvumilivu.

Vijiji vingine jirani wamevutiwa na hatua waliyoamua kuichukua kijiji cha ushongo na hivi sasa wanataka kufuata mfano huo ili kukuza pato la pweza katika maeneo yao lakini vile vile kuhifadhi mazingira yao kwa kurejeshea miamba iliyoharibiwa hapo awali.

NINI RAI NA WITO TOKA KWA JAMII HIZI JUU YA SUALA HILI :

(1) Jamii k**a hizi zilizo amua na kujinyima na kujitoa kuhifadhi mazingira kwa vitendo ziungwe mkono kwa vitendo zaidi ili wasivunjike moyo.

(2) Elimu ya uhifadhi kwa vitendo na nadharia iimarishwe zaidi kwa jamii hizi na nyinginezo zenye kuonyesha muitikio wa uhifadhi kwa vitendo.

(3) Miradi ya maendeleo hususani ya shughuli mbadala zinazozingatia suala zima la uhifadhi ielekezwe kwenye jamii hizi ili kuweza kunusuru rasilimali hifadhiwa.

(4) Fursa za vitendo za kutembelea maeneo yanayofanyiwa aina hizi za uhifadhi zitolewe kwa walengwa,yaani wanajamii wenyewe wapate fursa za kutembelea maeneo wanayofanya uhifadhi huu vizuri zaidi na kwa utaalamu zaidi ili kukuza ujuzi na kupiga hatua wakati ujao.

and agriculture service for conservation #
endelevu kwa ustawi wa jamii zetu #
bila zana haramu unawezekana #
πŸ πŸŸπŸ‹πŸ¬πŸš£πŸ‘Ύ

Je wajua kilimo cha mwani kinaweza kuwa k**a chanzo bora cha pato mbadala kwa jamii za pwani na kuchangia suala zima la ...
04/01/2022

Je wajua kilimo cha mwani kinaweza kuwa k**a chanzo bora cha pato mbadala kwa jamii za pwani na kuchangia suala zima la uhifadhi wa mazingira ya pwani yetu?

Moja kati ya kilimo bahari kinachofanyika wilaya ya Pangani mkoani Tanga katika kijiji cha Ushongo mabaoni,Kipumbwi, Sange,Stahabu na Mikocheni ni kilimo cha mwani aina ya Spinosum.

Mwani huu umekuwa ukilimwa kwa miaka mingi sasa,simulizi mbalimbali za wakulima wa vijiji hivi zinasema yakwamba hapo awali walikuwa wakilima aina zote mbili yaani Spinosum na cotonii,kutokana na mabadiliko ya hali ya hewa kwa sasa imeonekana Spinosum ikifanya vizuri zaidi ya cottonii kwa mazingira haya hivyo ikawalazimu kuhamisha nguvu zao zaidi kwenye aina hii ijapokuwa imekuwa na soko la bei ya chini kwa sasa ukilinganisha na cottonii.

Kilimo hiki kimekuwa msaada kwenye baadhi ya familia ziishizo katika ukanda huo.

Hivi sasa na kipindi cha karibuni soko kuu la mwani huo ni Zanzibar, wakulima wamekuwa wakilima na kuuza Zanzibar.

Kwa makadirio kwa kiwango cha chini kwa mwaka kijiji kimoja chaweza vuna tani 5 mpaka 6 kwa kilimo cha kienyeji na cha hali ya chini,na watu wachache.

Kwa mtazamo huu waweza ona na kutambua fika ya kwamba endapo kilimo hiki kikifanywa kwa utaalamu zaidi na kutafutiwa soko Zuri la uhakika kinaweza kubadili maisha ya jamii ziishizo maeneo hayo hususani kwa wakulima wenyewe.

Kwa mujibu wa maelezo ya baadhi ya wakulima kilio Chao kiko kwenye soko la uhakika na lenye bei nzuri, kwani kwa sasa wamekuwa wakiuza kilo moja chini ya sh 1000/= za kitanzania hali ambayo imekuwa ikimdidimiza mkulima kwaani mwani huu hjpimwa wakati ukiwa umekaushwa hali ambayo huupelekea kuingia kwa wingi kwani unakuwa mwepesi tayari.

Rai,wito na ombi la wakulima hawa:

1.wanaomba watafutiwe masoko mazuri yenye bei nzuri ya ununuzi na ya uhakika.

2.wanahitaji elimu zaidi juu ya kilimo hiki kwa njia za kitaalamu(elimu ya vitendo na nadharia).

3.Wanahitaji kupata safari za kujifunza na kuona toka kwa wengine waliofanikiwa.

na ustawi wa mazingira ya bahari #
and agriculture service for conservation #
coastal community network #
endelevu kwa ustawi wa pwani yetu #
bila mabomu unawezekana #
bila zana haramu unawezekana #
kwa ustawi wa utalii wetu #

πŸ‘ΎπŸš£πŸ πŸ¦ˆπŸŸπŸš

18/08/2020

Wanahitajika wafanyakazi wa tatu (vibarua wa shamba).
Sifa:Elimu sio lazima awe amesomaWenye uzoefu na kilimo cha matikitiWachapakaziSio watumizi wa kilevi chochoteWenye uwezo na utayari wakuishi kambini eneo la shambaKazi mkataba miezi mitatu Mshahara 100000/= Kwa mwezi ,posho na chakula vitakuwepo.Maswali zaidi piga simu namba 0622386925

Maliza maadhimisho ya nanenane kwa kuongeza ufahamu wako na AAS:πŸŒ±πŸ΅πŸŒΉπŸŒ²πŸŒ³πŸŒΊπŸ‘πŸ“πŸŸ*Je wajua unaweza ukahifadhi mazingira kwa kufa...
08/08/2019

Maliza maadhimisho ya nanenane kwa kuongeza ufahamu wako na AAS:πŸŒ±πŸ΅πŸŒΉπŸŒ²πŸŒ³πŸŒΊπŸ‘πŸ“πŸŸ

*Je wajua unaweza ukahifadhi mazingira kwa kufanya matumizi mazuri ya tairi zako za gari zilizokwisha chakaa?

*Je wajua tairi hizo zaweza kutumika kutengeneza bustani nzuri ya kuvutia ndani na nje ya fensi ya nyumba yako na kukunufaisha kwa mbogamboga na kuleta mvuto wa kipekee wa mauwa?

*Jifunze haya na mengine mengi juu ya kilimo na ufugaji mseto wa kisasa unaozingatia uhifadhi mazingira bureee kabisa kwa kufuata Link hii:
https://aaservicetanzania.blogspot.com

and agriculture service for conservation (AAS Tanzania) #
development #
East Africa farming community #
Agriculture Tanzania (SAT) #

MAENDELEO NA UHIFADHI WA MAZINGIRA VINAWEZEKANA!!πŸ”₯πŸ”₯✊✊

β€’Development while preserving is possible!!!  the world green #🌳🌳  planting #🌳🌳  agriculture  #🚜  aquaculture #πŸŸπŸ™  Devel...
22/04/2019

β€’Development while preserving is possible!!!

the world green #🌳🌳
planting #🌳🌳
agriculture #🚜
aquaculture #πŸŸπŸ™
Development #πŸš›πŸ›«πŸ­πŸ™
Fishery #πŸ›³βš“πŸš£

β€’Contact: +255764175381
+255755168998
Email: [email protected]

β€’Visit us : "A A S TANZANIA LTD" https://aaservicetanzania.blogspot.com

https://www.YouTube.com/channel1/UCpHSkmbvIeSleScnl-wc2JqA

πŸ’₯πŸ“·πŸ“ΈπŸ’₯>>>Credit to !!

Mobile/movable fish pond:  Sustainable fish farming  #  #πŸŸπŸšπŸ™πŸ¬πŸ‹πŸ   #πŸ πŸšπŸ—πŸ˜πŸŒ²πŸŒ±  #🐟🐠  #🐟🐠  #πŸ—πŸ˜πŸΏ  Agriculture #πŸŒ±πŸŒ»πŸ’πŸŒ³  Development...
17/04/2019

Mobile/movable fish pond:

Sustainable fish farming #
#πŸŸπŸšπŸ™πŸ¬πŸ‹πŸ 
#πŸ πŸšπŸ—πŸ˜πŸŒ²πŸŒ±
#🐟🐠
#🐟🐠
#πŸ—πŸ˜πŸΏ
Agriculture #πŸŒ±πŸŒ»πŸ’πŸŒ³
Development #πŸ›«πŸ­πŸ¬πŸ™

"A A S TANZANIA LTD" https://aaservicetanzania.blogspot.com

Phone: +255764175381
+255789134628
Email: [email protected]

KILIMO CHA MITI KWAAJILI YA MBAO, CHAKULA, MIFUGO(YA MAJINI NA NCHI KAVU) NA MAHITAJI MENGINE K**A KIUNGO BORA KUPUNGUZA...
11/03/2019

KILIMO CHA MITI KWAAJILI YA MBAO, CHAKULA, MIFUGO(YA MAJINI NA NCHI KAVU) NA MAHITAJI MENGINE K**A KIUNGO BORA KUPUNGUZA MIGOGORO YA UHIFADHI NA KUCHANGIA UCHUMI WA PANDE ZOTE MBILI:
(πŸŒ±πŸŒ²πŸŒ³πŸπŸœπŸ¦‚πŸ‘πŸ€πŸ‘πŸŸπŸ¬πŸ˜)

 UKIWA K**A MKULIMA WA MITI /MTUMIAJI WA RASILIMALI HII ,VIGEZO VIFUATAVYO VITAKUSAIDIA WEWE K**A MKULIMA MDOGO KATIKA KUCHAGUA MITI YA KUOTESHA MBEGU AU VIPANDIKIZI:

(A) MATUMIZI:
β€’ Matumizi ya baadaye ya mti ni kigezo muhimu kwaajili ya kuchagua mti wa mbegu.Miti kwaajili ya mbao ni tofauti na mitii kwaa jili ya malisho na kadhalika.Zifuatazo ni sifa za miti ya mbegu /Vipandikizi kutokana na matumizi yake:

MITI YA MBAO:
β€’ Uwe mrefu
β€’ Uwe umenyooka
β€’ Usiwe na mafundo
β€’ Usiwe unapanda

MITI YA CHAKULA CHA MIFUGO:
β€’ Uwe mfupi
β€’ Uwe na matawi makubwa na majani mengi

MITI YA KUNI:
β€’ Uwe na mashina mengi
β€’ Uwe na matawi mengi
β€’ Uweze kutoa vishina kirahisi

(B) MITI YENYE AFYA:
β€’ Epuka kuvuna mbegu kutoka miti midhaifu,yenye magonjwa na mifupi.

(C) MITI ILIYO KOMAA
β€’ Miti mizuri kuvuna mbegu ni miti iliyo komaa,ukivuna kutoka kwenye miti isiyo komaa mbegu hazitaota vizuri.

KUMBUKA: KILA UNAPOVUNA MBEGU HAKIKISHA UNAVUNA ZAIDI YA MITI 30 ILIYO KATIKA UMBALI WA MITA 100 KUTOKA MTI MOJA HADI MWINGINE ILI KUEPUKA UZAA MUMO (INBREEDING).USIPOFANYA HIVYO YAWEZA KUKULETEA MADHARA MITI YAKO KUWA NA GENES ZINAZOFANANA SANA NA KUWA RAHISI KUSHAMBULIWA NA MAGONJWA AMA TATIZO LOLOTE NA KUAMBUKIZANA NA HATIMAYE KUFA YOTE.

Usisahau kushare post za page yetu,kulike na Ku subscribe YouTube channel yetu kwenye blog,fuata link hapa chini :

https://aaservicetanzania.bogsport.com/

Address

Tanga

Alerts

Be the first to know and let us send you an email when Aquaculture And Agriculture Service for Conservation posts news and promotions. Your email address will not be used for any other purpose, and you can unsubscribe at any time.

Contact The Organization

Send a message to Aquaculture And Agriculture Service for Conservation:

Share