Wizara ya Kilimo

Wizara ya Kilimo Karibu kwenye Ukurasa rasmi wa Wizara ya Kilimo

Waziri wa Kilimo Mhe. Hussein Bashe, amekutana na kufanya mazungumzo na Waziri wa Kilimo, Viwanda vya nyama na Uvuvi kut...
27/04/2023

Waziri wa Kilimo Mhe. Hussein Bashe, amekutana na kufanya mazungumzo na Waziri wa Kilimo, Viwanda vya nyama na Uvuvi kutoka Uganda, Mhe. Kyakulaga Fred Bwino pamoja na Balozi wa Uganda nchini Tanzania,Mhe.Fred Mwesigye, Leo tarehe 27 April 2023 jijini Dodoma.

Katika Mazungumzo hayo wamejadiliana kwa kina kuweka makubaliano ya kimaandishi kushirikiana katika kukuza sekta Kilimo hususani upatikanaji wa Mbolea na pembejeo za kilimo, kuona uwezekano wa Kampuni ya Itracom Fertilizer ya jijini Dodoma kuuza mbolea yake nchini Uganda. Aidha, wamekubaliana kuimarisha mifumo ya usafirishaji wa bidhaa za Kilimo pamoja na kubadilishana uzoefu katika Kilimo Cha Kahawa.

/30

Waziri wa Kilimo, Mhe. Hussein Bashe ameongoza kikao cha tathimini ya uzalishaji, ubanguaji, na masoko kwa msimu wa 2022...
24/04/2023

Waziri wa Kilimo, Mhe. Hussein Bashe ameongoza kikao cha tathimini ya uzalishaji, ubanguaji, na masoko kwa msimu wa 2022/2023 na maandalizi ya msimu wa 2023/2024, kilichofanyika jijini Dodoma leo tarehe 24/04/2023.
Katika kiako hicho, Waziri Bashe amewataka wasambazajj wote wa viuatilifu kusajili upya na hatasita kufuta viuatilifu vyote ambavyo havikusajiliwa upya, hii ni kuweka mfumo thabiti wa kulinda wakulima na kukumbana na viuatilifu visivyokidhi viwango.
Kikao hiki cha wadau wa sekta ya korosho kimejadili kwa kina changamoto za sekta na kuweka mikakati ya kujuza sekta ikiwa ni pamoja na kusajili wakulima wote kwenye mfumo wa kidigitali ili kuwatambua wakulima wa korosho nchini

/30


Eid Mubarak   /30
22/04/2023

Eid Mubarak

/30


Waziri wa Kilimo Mhe. Hussein M. Bashe leo tarehe 17 Aprili,2023 jijini Dodoma amezindua Bodi ya Wakurugenzi ya Mamlaka ...
17/04/2023

Waziri wa Kilimo Mhe. Hussein M. Bashe leo tarehe 17 Aprili,2023 jijini Dodoma amezindua Bodi ya Wakurugenzi ya Mamlaka ya Afya ya Mimea na Viuatilifu(TPHPA) na kuitaka bodi hiyo kuisimamia Mamlaka hiyo kutekeleza majukumu yake kwa uadilifu kwa manufaa ya sekta ya kilimo.
Mhe Bashe, ameitaka TPHPA kuhakikisha inajikita katika kuwezesha biashara ya mazao ya kilimo nje ya nchi, kuhakikisha inaimarisha uwezo wake katika kilimo anga kwa kutumia teknolojia katika kukabiliana na visumbufu mimea na mazao.
Aidha, ameiagiza TPHPA kuwafutia leseni wafanyabiashara wa viatilifu ambao walioghushi katika sekta ya mbolea na kufutiwa leseni.
Kwa upande mwingine ameitaka TPHPA kufanya usajili upya wa viuatilifu vyote nchini ikiwa ni njia mojawapo ya kudhibiti viuatilifu visivyo na ubora nchini.
/30


UTEUZI
16/04/2023

UTEUZI

Tanzania itakuwa mwenyeji wa Mkutano mkubwa wa Mifumo ya Chakula Afrika(AGRF-Africa Food System Summit)Serikali kupitia ...
30/03/2023

Tanzania itakuwa mwenyeji wa Mkutano mkubwa wa Mifumo ya Chakula Afrika(AGRF-Africa Food System Summit)
Serikali kupitia Wizara ya Kilimo imeendelea kufanya uwekezaji mkubwa katika sekta ya kilimo nchini.

/30



Recover, Regenerate, Act: Africa’s Solutions to Food Systems Transformation is anchored around building back better Food Systems and Food Sovereignty with the youth and women at the center.

Vijana wa BBT wakiendelea kupata  mafunzo katika kituo cha BIHAWANA , Dodoma leo tarehe 25.03.2023, ikiwa ni siku ya nne...
25/03/2023

Vijana wa BBT wakiendelea kupata mafunzo katika kituo cha BIHAWANA , Dodoma leo tarehe 25.03.2023, ikiwa ni siku ya nne tangu walipofika katika vituo hivyo vya mafunzo.
Hivi karibuni Mheshimiwa Dkt. Samia Suluhu Hassan, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania alizundua rasmi mpango wa serikali wa kuanzisha mashamba ya pamoja(block farms) kwa ajili ya vijana na wanawake, na program ya vijana na wanawake kuingia kwenye sekta ya kilimo ya BBT; hafla iliyofanyika katika mashamba ya Chinangali II, Dodoma. Mheshimiwa Rais amewataka vijana hao 812 walipata fursa ya kuanza mafunzo hayo kwa awamu ya kwanza kuwa na juhudi na kisha kwenda kuzalisha kwa tija na kibiashara.
“Twendeni tukalime kibiashara” alisisitiza Mhe Rais


/30

Waziri wa Kilimo Mhe. Hussein Bashe leo tarehe 23/03/2023 amekutana na kufanya mazungumzo na Balozi wa Marekani nchini T...
23/03/2023

Waziri wa Kilimo Mhe. Hussein Bashe leo tarehe 23/03/2023 amekutana na kufanya mazungumzo na Balozi wa Marekani nchini Tanzania, Mhe. Balozi Michael Battle, katika ofisi za wizara ya kilimo jijini Dodoma. Mazungomzo hayo yamelenga kuimarisha ushirikiano na kuvutia wawekezaji kwenye sekta ya kilimo na hasa katika kutatua changamoto ya ajira kwa vijana na wanawake.


/30

Vijana wa BBT wakiwa katika kituo atamizi cha Bihawana jijini Dodoma, wakiendelea na mafunzo ya uandaaji na uzalishaji w...
23/03/2023

Vijana wa BBT wakiwa katika kituo atamizi cha Bihawana jijini Dodoma, wakiendelea na mafunzo ya uandaaji na uzalishaji wa miche! Kazi imeanza!


/30

“Twendeni tukalime kibiashara” Maneno ya Mheshimiwa Dkt. Samia Suluhu Hassan wakati akizundua mashamba makubwa ya pamoja...
20/03/2023

“Twendeni tukalime kibiashara” Maneno ya Mheshimiwa Dkt. Samia Suluhu Hassan wakati akizundua mashamba makubwa ya pamoja, leo tarehe 20.03.2023 Chinangali, Dodoma

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan akizindua Mradi wa Mashamba Makubwa (Block Farming...
20/03/2023

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan akizindua Mradi wa Mashamba Makubwa (Block Farming) kwaajil ya Vijana na Wanawake kupitia Programu ijulikanayo k**a Building Better Tomorrow (BBT) ya Wizara ya Kilimo ambapo pia ameweka jiwe la msingi kwenye Mashamba ya Chinangali Chamwino Mkoani Dodoma.

Uzinduzi huo umeenda sambamba na kukabidhi mitambo na Magari kwa Tume ya Taifa ya umwagiaji kwaajil ya maboresho kwenye sekta ya kilimo.

Rais Dkt. Samia pia atashuhudia uwekaji Saini mikataba ya usanifu, ukarabati na ujenzi wa miundombinu ya umwagiliaji!


Address

P. O. Box 9192
Temeke
255

Opening Hours

Monday 07:30 - 15:30
Tuesday 07:30 - 15:30
Wednesday 07:30 - 15:30
Thursday 07:30 - 15:30
Friday 07:30 - 15:30

Alerts

Be the first to know and let us send you an email when Wizara ya Kilimo posts news and promotions. Your email address will not be used for any other purpose, and you can unsubscribe at any time.

Contact The Organization

Send a message to Wizara ya Kilimo:

Share