Logos Ministry

Logos Ministry Listen to God and live forever.....! l

KUACHILIA/KUSAMEHE.Ni pale unapokuwa huru ndani mwako, Jambo hili linatupoteza wengi sana ,na mwishowe tunarudi kuwalaum...
29/04/2024

KUACHILIA/KUSAMEHE.

Ni pale unapokuwa huru ndani mwako,

Jambo hili linatupoteza wengi sana ,na mwishowe tunarudi kuwalaumu wachawi Kwamba ndio wanaotukwamisha mambo yetu kumbe hiyo ni sumu uliyokaa nayo ndani mwako ndio tatizo la mafanikio yako.

Kuna mtu unakuta ametunza kinyongo,ametunza Hasira,ametunza roho mbaya ,ametunza negativity za Kila aina na watu/vitu muda mrefu ,hiyo ni sumu ambayo inakudhuru na kukurudisha nyuma mambo yako mengi ,ikiwemo kutokuusikia ulimwengu jinsi unavyozungumza nawe,maana umejaa sumu ndani mwako.

Sasa basi jawabu ni kuachilia/KUSAMEHE na kuwa tupu ndani mwako.
Ndipo UTAONA mambo mapya yanaanza kumea na kukua ndani mwako.

Hata k**a mtu alikufanyia jambo baya Namna gani wewe jitahidi uliachilie/samehe .

KUSAMEHE ni dawa katika mambo yako yaliyokwama .

⚠️ "Habari LOGO samahani naomba ficha utambulisho wangu,, mm ni binti wa miaka 26 nina mtt mmoja,,  kilicho nileta kwenu...
29/04/2024

⚠️ "Habari LOGO samahani naomba ficha utambulisho wangu,, mm ni binti wa miaka 26 nina mtt mmoja,, kilicho nileta kwenu ni juu ya mahusiano niliyo nayo,, niko na mahusiano ambayo mwanzo niliamin ni urafiki wa kushauriana tuu cozi ni mume wa mtu,, lakini CK zilivyo zidi kusonga tukajikuta tumependana kweli na yeye akiwa bado yuko na mkewe,,

mpaka sasa tuko na miaka miwili kwenye mahusiano ya kimapenzi,, mala akaanza kuleta malalamiko kuhusu mkewe kitu ambacho ckuwa napenda akawa anasema mkewe anadai kuondoka na sio mara ya kwanza kusema hvy,, mm nikawa nikimshauri asimwache mkewe akaondoka coz sikutaka kuonekana ni chanzo cha mkewe kuondoka,,

na mpaka sasa naomba ushauri ni kwa sababu mkewe kaondoka na yeye anadai mkewe kaondoka kwa ajiri ya mali maana hakutoa mahari kwao na chanzo cha kutokutuo ni kutokana na mkewe huyo alishawahi kuiba fedha kiasi cha laki 9 anakimbilia kwao na wakampokea,,

ndipo akawaambia kuwanhy ndo mahari yenyewe,, lakini saiv baada ya kuondoka kwa mara ya nne, anasema hawezi kumpa nafasi ya kurudi tena,, nimemuomba sana apeleke mahari na k**a hana mm nitamchangia lakini Kagoma,,

mm najisikia vby kwa kuondoka kwakwe yule mwanamke najihisi mm ndie mwenye hatia maana alikuwa akinijua na meseji alikuwa akinitumia za kunitukana,, sasa mwanaume anataka kunioa mm,,

lakini mm cko tayari maana dhamira yangu haikuwa kuolewa na mme wa mtu hata k**a mkewe kisha ondoka,, naombeni ushauri nifanyeje 😭😭😭 "

Na kukumbusha
28/04/2024

Na kukumbusha

28/04/2024

⚠️ :Logo ficha ID yangu mimi ni mama wa miaka 25 nipo na mwaka na nusu kwenye ndoa pia na mtoto umoja

Mwanzo nilipoolewa na Mume wangu alikuwa ananiadithia jinsi mama ake(mamkwe) anavyopenda hela sana na yeye ndo sababu ya baba ake kutokuwa tajiri(kutopata hela nyingi) wana za kula na kulipa nyumba tu mama mkwe ni mtu wa kupenda starehe sana,vikoba vingi,magroup ya kuchangia kwenye harusi na hana kazi

Sasa mimi natoka kwenye familia inayojiweza ,mda naolewa nilikuja na pesa juu mume wangu alikuwa hana hela zile hela zangu zikawa mtaji tukaanza maisha vizuri sana na tukawa tunaishi vizuri kwa kupendana

Tatizo limeanza hizi siku kila ata elfu 20 tumepata ananambia mamkwe(mama ake) amemuomba hela anataka azimpe mi nikakataa nikaona tusije tukawa k**a familia yake

Sasa tatizo lilianzia apo mimi na mume wangu hatuongeleshani juu nimemkataza kumpa hela mama yake kila siku na yeye anasema atampa juu ni mama ake

Nimechanganyikiwa nataka ushauli wenu wadau niko nafanya makosa au juu hali ya hewa mimi na mume wangu apa nyumbani sio salam kabisa??? Nitasoma comment"

24/04/2024

⚠️ "Hellow Swahili nimerud tena kwa lengne....samahn naomba nipostie kwa wadau wanifafanulie hili. Ucku wa Jana kuamkia Leo nimeota ndoto mbili sijazielewa kwanza nliota mpenz wang anatafutwa na police had nyumban mara kdg akaja nyumbn akakuta wale askar na wak**atwa Nikashtuka

Nlipo lala tena nkaota nimepigiwa cm mama angu amefariki nikafunga safari kurud nyumbn lakin muda mref niliutumia kituon ckujua nlikuwa nafanyaje,nkiwa njian naelekea nyumban nkakutana na Mdogo wangu akiwa amevaa nguo za Nusu uchi nyeus na nyekundu akanipa mfuko nrudi nao nyumbn na nlipo fika nyumban nakuta wanaume wamekaa nje na wanawake walijaa sehem wakishangaa kitu

lakin wala hawakujali kuhusu mimi hata Baada waliponiona nalia na katika wale wanawake palikuwa na mama angu Mdogo amesimama mlangon ananicheka Ambaye mtoto wake nlikutana nae njian..Na nkashtuka hapo ilikuwa saa 10 ucku"

Bless me today and my favorite family
24/04/2024

Bless me today and my favorite family

Kundi la maprofesa waliitwa kupanda ndege. Milango ilipofungwa maprofesa wote walifahamishwa kuwa ndege hiyo imetengenez...
24/04/2024

Kundi la maprofesa waliitwa kupanda ndege. Milango ilipofungwa maprofesa wote walifahamishwa kuwa ndege hiyo imetengenezwa na wanafunzi wao. Maprofesa wote wakakimbilia kwenye mlango wa ndege wakiomba kushuka. Isipokuwa profesa mmoja tu alibaki ameketi kwa ujasiri na utulivu. Kuna mtu alimuuliza, "kwanini hauhangaiki kushuka kwenye ndege k**a wenzako?" Profesa akajibu kwa kujiamini, "Ni wanafunzi wangu waliunda hii ndege". Akaulizwa tena, "Kwahiyo una uhakika uliwafundisha vizuri? Profesa alijibu; "K**a ni wanafunzi wangu, Nina uhakika haitopaa.."

Kutoka Kwa Pastor Rose ShabokaKuna wanawake Mungu amewapa tu akili nyingi. Yaani naturally tu ana akili kubwa, ana mawaz...
17/04/2024

Kutoka Kwa Pastor Rose Shaboka

Kuna wanawake Mungu amewapa tu akili nyingi. Yaani naturally tu ana akili kubwa, ana mawazo ya mbali, ana upeo mkubwa, yuko serious na maisha, yuko very calculative na akikushauri ukamsikiliza unatoboa. Wengi wa aina hii wanakuaga viongozi au wakuu kwenye maeneo fulani. Most of them are very strong minded. Focus yao ni maendeleo. Wako tough pia kwa sababu zinacharge sana.

Anaweza kuwa na umri mdogo lakini akili yake na hekima yake haifanani na umri wake. Ni Mungu amemuumba hivyo. Anaweza kuwa na madhaifu k**a binadamu lakini kichwa chake kimechangamka. Saa zingine ni k**a anaweza kuwa anakuzidi akili hivi ukimuangalia japo huwezi ku-admit. Unajikaza kiume🀣 of which inaeleweka. Hatukulaumu, mfumo dume unatesa wengi. Anaweza kukutandika maswali na kukufikirisha mpaka ukafikiri sijui uko kwenye mtihani gani lakini lengo lake ni kujenga.

Sasa ikitokea unaye wa design hii k**a mke fanya hivi;

1) Kubali kwamba mwanamke uliyeoa sio kilaza na ana akili nyingi na kukubali sio udhaifu. Ni hekima na inaonyesha ukomavu na inaonyesha unajiamini na unajua nafasi yako k**a Kichwa haiwezi kubadilika hata k**a mke ana akili kiasi gani.

2)Mpokee kwa shukrani k**a zawadi yako kutoka kwa Mungu. Badala ya kumuona mjuaji, Muone ni asset. Mfanye rafiki na mshauri wako wa karibu. Hiyo ni rasilimali Mungu amekupa kaka.

3)Ona kwamba Mungu amekupendelea sana kukupa aina hiyo ya mwanamke kwa sababu wanaume wenzio wanatamani wangepata wa hivyo na hawana. Mtunze, mlee k**a lulu yako ya thamani ili akusaidie ufanikiwe sana.

4)Akili zake zisikutishe, Wala usimuone tishio. Baraka kwenye familia zinaweza kuja kupitia mke, mume au wote wawili kwa pamoja. Kuwa positive, mpe nafsi na zitumie akili zake kukuletea wewe na familia faida. K**a umeshamjua ni mzuri kwenye jambo fulani usijitutumue sababu ni mwanaume wakati kiukweli yeye anaweza kuliko wewe. Weka EGO chini, Mpe nafasi afanye ili mfanikiwe.

5) Mpende sana.

😌😌
01/02/2024

😌😌

25/01/2024

Usipende kuwaambia watu jinsi ulivyoumizwa au ulivyo na shida kwa sababu;

A) 25 % Watakusikiliza kwa makini lakini hawatakusaidia.

B) 44% Watakusikiliza kwa makini na kuonyesha kusikitika sana lakini wakitoka hapo Watakucheka na watapata ya kuhadithia huko mitaani.

C) 30% Watakusikiliza na kukusikitikia na hawatakusaidia chochote na wana matatizo makubwa kuliko wewe.

D) 01% Watakuhurumia na kukuombea.

NB: NI HERI KUMWELEZA MUNGU

25/01/2024

Kuendelea kuwasiliana na Ma Ex wako wakati upo kwenye mahusiano mengine ni kukosa heshima

Wafungie vioo wote, Futa namba zao, acha wawe watu ambao walikuwepo kwenye historia iliyopita

Kamwe usiruhusu hata majina yao yatajwe katika mahusiano yako mapya

Ni mkosi mkubwa kuwa karibu nao, unayavuta matatizo yaliyopita yaje kuharibu mahusiano yako mapya

Haijarishi mahusiano yako mapya yana hali gani, lakini kumbuka ulishaamua kuachana naye kwahivyo hawezi kuwa bora hata kidogo

Hata k**a kuna mtu utaingia naye kwenye mahusiano basi asiwe yeye

mpaka ukaondoka kwake ulishajiridhisha kuwa hafai hata kidogo sasa kwanini unaendelea kuwasiliana nae

Usiseme ni rafiki yako wewe ni Mpumbavu, wewe haukuwa unatafuta rafiki

kila mtu kwenye maisha yako anakundi lake, na unavyotafuta watu kwenye kila kundi huwa unaangalia nani anafaa

wewe ulitaka awe kwenye kundi la mpenzi lakini lilisha mshinda

marafiki tafuta wengine mbona wapo kibao tu kwani lazima awe yeye?

Akikuuliza umenisamehe mwambie ndio ila sitaki hata kuja kukuona

Kwani umesahau Mungu alicho mfanyia Adam na Hawa walipo kosea bustani ya Edeni..?

Aliwasamehe lakini aliwafukuza edeni hakutaka kuwaona tena, unadhani Mungu mjinga?

Kuna watu wakishakukosea hutakiwi kuwaacha jirani hata kidogo

Ukiwaacha majuto uliyojuta mwanzo ni madogo sana

Utakuja kujuta zaidi pale ambapo mahusiano na huyo Ex wako yalivunjika, Alafu anakuja kwenye mahusiano yako mapya anayavuruga alafu hakutaki pia

Hii ni ya mwisho, Kabla hujafuta hiyo namba Block kwanza alafu ndio uifute

Acha kuwaza waza, Vitu vigumu havijawai tatuliwa kwa maamuzi mepesi

Vitu vigumu vinatatuliwa kwa maamuzi magumu

Kuwa jasiri simama sema mimi naweza sijazaliwa kwaajili ya yeyote

Usiwazee Maumivu au watakuonaje, kumbuka duniani hauishi kwaajiri ya mtu yeyote yule na watu hawajali kuhusu lolote lile kwako

Ukiona wanakukera futa hadi namba za mashemeji na mawifi

πŸ“ŒπŸ“ŒπŸ“ŒπŸ“ŒπŸ“ŒπŸ“ŒπŸ“ŒπŸ“ŒπŸ“ŒπŸ“ŒπŸ“ŒπŸ“ŒπŸ“ŒπŸ“ŒπŸ“ŒπŸ“ŒπŸ“ŒπŸ“ŒπŸ“ŒπŸ“ŒπŸ“ŒπŸ“ŒπŸ“ŒπŸ“ŒπŸ“ŒπŸ“Œ*NYIE VIUMBE WA K**E KUENI MAKINI NA TAMAA ZENYU ZA PEXA NA MAGARI TUMEPOTEZA WASCHANA TAKRIBA...
21/01/2024

πŸ“ŒπŸ“ŒπŸ“ŒπŸ“ŒπŸ“ŒπŸ“ŒπŸ“ŒπŸ“ŒπŸ“ŒπŸ“ŒπŸ“ŒπŸ“ŒπŸ“ŒπŸ“ŒπŸ“ŒπŸ“ŒπŸ“ŒπŸ“ŒπŸ“ŒπŸ“ŒπŸ“ŒπŸ“ŒπŸ“ŒπŸ“ŒπŸ“ŒπŸ“Œ*NYIE VIUMBE WA K**E KUENI MAKINI NA TAMAA ZENYU ZA PEXA NA MAGARI TUMEPOTEZA WASCHANA TAKRIBANI 600. KUTOKANA NA KUSHAWISHIWA KWA PESA NA WATU MNAO WAJUA NA MSIO WAJUA KWENDA NAO MAHOTELINI AU MAJUMBANI MWAO UKIJUA KUA UTARUD NA PESA MINGI __SASA TENA TUMEPOTEZA RAIA MUNGINE ...BAADA YA KULAGHAIWA KWA PESA NA KUTAKA KUCHUKULIWA VIUNGO VYAKE NA KWENDA KUUZWA KWA ZAID YA MILLION 700/=Tzsh.... HIVYO BASI JESHI LA POLICE LINAWATAKA RAIA WOTE KUTOA USHILIKIANO KWAO ILI KULINDA TAIFA KWA UJUMLA NA KUA MAKINI NA MTU YEYOTE ANAE KUKALIBIA ..IWE URAFIKI KIMAPEMZI AU KWA NAMNA YEYOTE ILE ............... πŸ™πŸ™TAFADHALI SHARE KWA WENGINE PIA πŸ™πŸ™ujumbe huu umewalenga Saana wadada zetu Kwan ndiy wahanga wakubwaa kbsa.... πŸ“ŒπŸ“ŒπŸ“ŒπŸ“ŒASANTENIπŸ“ŒπŸ“ŒπŸ“ŒπŸ“ŒπŸ“Œ

Address

Temeke

Opening Hours

Monday 09:00 - 17:00
Tuesday 09:00 - 17:00
Wednesday 09:00 - 17:00
Thursday 09:00 - 17:00
Friday 09:00 - 17:00
Saturday 09:00 - 17:00
Sunday 09:00 - 17:00

Telephone

+255758216943

Alerts

Be the first to know and let us send you an email when Logos Ministry posts news and promotions. Your email address will not be used for any other purpose, and you can unsubscribe at any time.

Contact The Organization

Send a message to Logos Ministry:

Share