ofisi ya mbunge rungwe

*Taarifa Kutoka Ofisi ya Mbunge Jimbo la Rungwe 24/04/2023**ISYONJE-ISONGOLE*Katibu wa Mbunge Jimbo la Rungwe Gabriel Mw...
24/04/2023

*Taarifa Kutoka Ofisi ya Mbunge Jimbo la Rungwe 24/04/2023*

*ISYONJE-ISONGOLE*
Katibu wa Mbunge Jimbo la Rungwe Gabriel Mwakagenda amemwakilisha Mbunge wa Jimbo la Rungwe *Mhe; Anton Mwantona* kwenye hafla ya Uzinduzi wa *Zahanati ya Kijiji Cha Isyonje* Kata ya *Isongole*.

Zahanati hiyo iliyoanzishwa kwa nguvu za Wananchi imezinduliwa Leo na Mkuu wa Wilaya ya Rungwe *Mhe; Jaffar Haniu* kufuatia michango ya wadau Mbalimbali wa Maendeleo, Kisha Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Kutoa Fedha za ukamilishaji pamoja na Vifaa Tiba.

Akitoa salam za Mhe; Mbunge; Katibu amesema katika kuunga Mkono Juhudi za wananchi wa Isyonje katika kufanikisha Ujenzi wa Zahanati hiyo Mhe; Mbunge alijitolea *Madirisha (Alminium) 18 yenye thamani ya Tsh 6,200,000* pamoja na gharama za kufunga ikiwa ni Ahadi aliyoitoa wakati wa Kampeni za Uchaguzi mwaka 2020.

Pia Katibu amewasihi Wananchi kuendelea kujitolea na kushiriki katika shughuli Mbalimbali za Maendeleo huku wakiendelea kuiunga Mkono Serikali inayoongozwa na Mhe; Rais wetu *Dkt; Samia Suluhu Hassan* ili kufanikisha lengo la Serikali katika kusogeza Huduma za kijamii karibu na Wananchi.

* #*

*Taarifa Kutoka Ofisi ya Mbunge wa Jimbo la Rungwe 21/04/2023**Kata ya Mpuguso*Mbunge wa Jimbo la Rungwe *Mhe; Anton Mwa...
21/04/2023

*Taarifa Kutoka Ofisi ya Mbunge wa Jimbo la Rungwe 21/04/2023*

*Kata ya Mpuguso*
Mbunge wa Jimbo la Rungwe *Mhe; Anton Mwantona* amefanya ziara Kata ya Mpuguso kukagua Maendeleo ya Ujenzi wa Shule Mpya ya Msingi ya Ushirika Kisha kuzungumza na Wananchi wa Kata ya Mpuguso.

Mhe; Mwantona amekabidhi Jumla ya *Bati 236* zenye thamani ya Tsh *8,260,000* kwa ajili ya ukamilishaji wa Vyumba 4 (Vinne) na Ofisi 2 (Mbili) katika Shule ya Msingi Ushirika.

Vile vile Mhe; Mbunge amekabidhi Jumla ya Computer 3 (Tatu) zenye thamani ya Tsh *2,800,000* kwa Shule ya *Sekondari ya Mpuguso* na Shule za *Msingi Masebe na Mpuguso* kwa ajili ya kusaidia kwenye uandaaji wa Majaribio ya wanafunzi na shughuli Mbalimbali za kiofisi.

Katika hatua nyingine ili kuboresha Miundombinu ya Shule ya Msingi *Mpuguso* Mhe; Mbunge ameahidi kuwapatia Madirisha 30, Madawati 10 na kuwapatia Mahitaji yote ya Shule Wanafunzi wasiojiweza wanaosoma kwenye Shule hizo.

Pia Mhe; Mwantona amekabidhi *Saruji Mifuko 100* kwa ajili ya Ujenzi wa vyumba vya Madarasa unaoendelea Katika Shule ya Msingi *Mpumbuli*

*Mwisho;* Mhe; Mbunge ametumia nafasi hiyo kumshukuru *Mhe; Rais Dkt; Samia Suluhu Hassan* kwa Kutoa Fedha nyingi kwenye Miradi ya Maendeleo Jimbo la Rungwe na kuwasihi Wananchi wa Kata ya Mpuguso na Jimbo la Rungwe kwa ujumla kuendelea kumuunga Mkono Mhe; Rais kwa kujitolea kushiriki kwenye shughuli Mbalimbali za Maendeleo.

*Gabriel Mwakagenda*
*Katibu wa Mbunge Jimbo la Rungwe*

*Taarifa Kutoka Ofisi ya Mbunge wa Jimbo la Rungwe 31/03/2023*Mbunge wa Jimbo la Rungwe Mhe; Anton Mwantona ametoa fedha...
01/04/2023

*Taarifa Kutoka Ofisi ya Mbunge wa Jimbo la Rungwe 31/03/2023*

Mbunge wa Jimbo la Rungwe Mhe; Anton Mwantona ametoa fedha Tsh *1,000,000* kwa ajili ya kusaidia Matibabu ya *Veronica Richard Kabojela* Mkazi wa Kijiji Cha *Igembe,* Kata ya *Kinyala,* Wilaya ya *Rungwe,* Mkoa wa *Mbeya*

Veronica Richard anasumbuliwa na ugonjwa wa Kansa iliyosababisha kuoza kwa miguu yake yote miwili. Baada ya kushindwa kumudu gharama za matibabu yeye na wadogo zake walifika Ofisi ya Mkuu wa Wilaya ya Rungwe kwa ajili ya kuomba msaada Kisha Mbunge kupata taarifa kupitia Ofisi ya Mkuu wa Wilaya.

Mgonjwa amefikishwa katika Hospitali ya Rufaa Kanda ya Mbeya kuendelea na Matibabu kwa Ushirikiano mkubwa uliofanywa na Ofisi za Mkuu wa Wilaya, Ustawi wa Jamii, Mkurugenzi Mtendaji (H) ya Rungwe na Mbunge.

Mhe; Mbunge anawaomba wasamalia wema watakaoguswa na kuwiwa kuchangia Matibabu ya Veronica Richard kuwasiliana naye kwa Simu namba *0769 088 641* Jina; *Veronica Richard Kabojela*

*Gabriel Mwakagenda*
*Katibu wa Mbunge (J) Rungwe*

*Taarifa Kutoka Ofisi ya Mbunge Jimbo la Rungwe 15/03/2023**ILALABWE-IPONJOLA*Katibu wa Mbunge Jimbo la Rungwe Gabriel M...
15/03/2023

*Taarifa Kutoka Ofisi ya Mbunge Jimbo la Rungwe 15/03/2023*

*ILALABWE-IPONJOLA*

Katibu wa Mbunge Jimbo la Rungwe Gabriel Mwakagenda, kwa niaba ya Mbunge wa Jimbo la Rungwe *Mhe; Anton Mwantona* amekabidhi *Bati 135* Shule ya Msingi *Ilalabwe*, inayoundwa na Vijiji viwili vya *Ilalabwe* na *Ngana,* Kata ya Iponjola, Wilaya ya Rungwe.

Bati hizo ni kwa ajili ya ukamilishaji wa Vyumba 2 (Viwili) vya Madarasa na Ofisi 1 (Moja) ya Walimu ikiwa ni kuunga Mkono Juhudi za wananchi waliojenga Jengo hilo hadi kufikia hatua ya Boma. Kwa Sasa wanaendelea na Upasuaji wa Mbao kwa ajili ya Upauaji.

Hii ni Awamu ya pili kwa Mhe; Mwantona kuunga Mkono Juhudi za wananchi wa Kijiji Cha Ilalabwe, Baada ya hapo awali *03, December, 2020* kuwapatia *Saruji Mifuko 100* kwa ajili ya Ujenzi wa Zahanati ya Kijiji hicho.

* #*
* #*

*Taarifa Kutoka Ofisi ya Mbunge Jimbo la Rungwe 12/03/2023**KATABE-KYIMO*Katibu wa Mbunge Jimbo la Rungwe Gabriel Mwakag...
12/03/2023

*Taarifa Kutoka Ofisi ya Mbunge Jimbo la Rungwe 12/03/2023*

*KATABE-KYIMO*

Katibu wa Mbunge Jimbo la Rungwe Gabriel Mwakagenda leo 12/03/2023 amemwakilisha Mbunge wa Jimbo la Rungwe *Mhe; Anton Mwantona* kwenye hitimisho (Fainali) ya Mashindano ya Mpira wa Miguu yaliyofanyika katika *Kijiji Cha Katabe, Kata ya Kyimo* Wilaya ya Rungwe

Mashindano hayo maarufu K**a *Kikende Cup* yaliyokuwa na lengo la kukusanya Fedha kwa ajili ya ununuzi wa Printer ya Rangi (Colored Printer) kwa ajili ya matumizi kwenye Shule ya Msingi Katabe yenye thamani ya *Tshs 500,000* (Laki Tano) yaliandaliwa na Mwenyekiti wa Kijiji Cha Katabe *Bw; Boaz Kikende* yameshuhudia timu Mbili za *Kiwira City* toka Kata ya Kiwira na *Itebe FC* kutoka Kata ya Lufingo zikicheza Fainali na Timu ya *Itebe FC* kufanikiwa Kuwa Mshindi wa Mashindano hayo.

Kupitia Mashindano hayo jumla ya Fedha Tsh *250,000* zimekusanywa huku Mhe; Mbunge akiahidi kuwapatia Fedha iliyobakia Tsh *250,000* ili kukamilisha lengo la kupata Tsh *500,000* kwa ajili ya kununulia Printer na kumaliza Changamoto katika Shule ya Msingi Katabe.

* #*
* #*

*Taarifa Kutoka Ofisi ya Mbunge Jimbo la Rungwe 10/03/2023**(a) Malindo*Katibu wa Mbunge Jimbo la Rungwe Gabriel Mwakage...
10/03/2023

*Taarifa Kutoka Ofisi ya Mbunge Jimbo la Rungwe 10/03/2023*

*(a) Malindo*

Katibu wa Mbunge Jimbo la Rungwe Gabriel Mwakagenda kwa niaba ya Mbunge wa Jimbo la Rungwe *Mhe; Anton Mwantona* amekabidhi Vifaa vya Ujenzi Katika *Shule ya Sekondari ya Kapugi* Kata ya Malindo.

Katibu amekabidhi *Saruji Mifuko 40,* *Tofari trip 2 na Mchanga trip 2* kwa ajili ya Ujenzi wa Choo chenye *Matundu 9 (Tisa)* katika Shule ya Sekondari ya Kapugi ikiwa ni sehemu ya utekelezaji wa Ahadi ya Mhe; Mbunge aliyoitoa tarehe *11/07/2022* alipofanya Ziara ya kusikiliza changamoto/kero za wananchi Kata ya Malindo.

Mbali na vifaa hivyo Mhe; Mwantona pia aliahidi kuwapatia *Bati 50* kwa ajili ya kukamilisha Ujenzi wa Choo hicho cha wanafunzi.

*(b) Mpuguso*

Vile vile Katibu amekabidhi kiasi Cha Fedha *Tsh 500,000* (Laki Tano) kwa *Mchg; Madaraka Ndenjela Sindondwa* wa Kanisa la *E. A. G. T* Mpuguso ikiwa ni Ahadi aliyoitoa Mhe; Mbunge tarehe *20/12/2022* alipowatembelea Kanisani hapo kuwajulia Hali kufuatia Maafa waliyopata Baada ya Jengo lao la Kuabudia kuezuliwa kwa kimbunga.

* #*
* *

*Taarifa Kutoka Ofisi ya Mbunge Jimbo la Rungwe 25/02/2023*Katibu wa Mbunge Jimbo la Rungwe, Gabriel Mwakagenda Amefanya...
25/02/2023

*Taarifa Kutoka Ofisi ya Mbunge Jimbo la Rungwe 25/02/2023*

Katibu wa Mbunge Jimbo la Rungwe, Gabriel Mwakagenda Amefanya Ziara ya kukabidhi vifaa kwa niaba ya Mbunge wa Jimbo la Rungwe *Mhe; Anton Mwantona* kwenye Kata za *Isongole* na *Lupepo*

*1. Kata ya Isongole*
Katibu amekabidhi *Saruji Mifuko 50* katika Shule ya *Msingi Idweli* Iliyopo Kijiji Cha Idweli, kwa ajili ya ukamilishaji wa Vyumba 2 (viwili) vya Madarasa vilivyojengwa kwa nguvu za Wananchi.

*2. Kata ya Lupepo*
Vile vile Katibu Amekabidhi *Mabati 190* Katika Shule Mpya ya Msingi Lyale, Iliyopo Kijiji Cha Lupepo, kwa ajili ya ukamilishaji wa Vyumba 3 (Vitatu) vya Madarasa na Ofisi 1 (moja) kufuatia Ombi walilolitoa Wananchi hao wakati wa Ziara ya Mhe; Mbunge aliyoifanya kwenye Kata ya Lupepo tarehe *22/12/2022*

*Kipekee;* kwa niaba ya Mhe; Mbunge niwapongeze Sana Wananchi wa Lyale, kwa mshikamano na morali/shauku kubwa ya kimaendeleo waliyoonyesha wakati wa mapokezi ya vifaa siku ya leo. Ni matarajio ya Mhe; Mbunge kwamba, Ujenzi wa Shule hiyo utakamilika mapema na kwa wakati ili michakato mingine ya usajiri wa Shule ianze.

* #*
* #*

*Taarifa Kutoka Ofisi ya Mbunge wa Jimbo la Rungwe 23/02/2023*Katibu wa Mbunge Jimbo la Rungwe Gabriel Mwakagenda Amefan...
23/02/2023

*Taarifa Kutoka Ofisi ya Mbunge wa Jimbo la Rungwe 23/02/2023*

Katibu wa Mbunge Jimbo la Rungwe Gabriel Mwakagenda Amefanya Ziara ya kukabidhi vifaa vya Ujenzi kwa niaba ya Mbunge wa Rungwe *Mhe; Anton Mwantona* Kata ya Isongole kwenye Vijiji vya *Ngumbulu na Ndwati*

*1. Kijiji Cha Ngumbulu*
Katibu amekabidhi *Saruji Mifuko 100* katika Shule ya Msingi Ngumbulu, Kata ya Isongole kwa ajili ya ukamilishaji wa Chumba kimoja Cha Darasa.

*2. Kijiji Cha Ndwati*
Vile vile Katibu Amekabidhi *Saruji Mifuko 50* Katika Shule ya Msingi Mpya inayojengwa ya Ndwati, kwa Viongozi wa Serikali ya Kijiji na baadhi ya wawakilishi wa wananchi.

Makabidhiano hayo yamefanyika Katika Kijiji Cha Unyamwanga kutokana na changamoto ya kuharibika kwa Miundombinu ya Barabara kufuatia Mvua kubwa iliyonyesha mapema Leo hivyo kusababisha magari kukwama Njiani na kushindwa kufika Kijiji hicho.

Ifahamike kwamba kijiji cha Ndwati ni miongoni mwa Vijiji vichache ambavyo havina kabisa Shule ya Msingi hivyo kupelekea wanafunzi kusafiri Hadi Kijiji jirani Cha Unyamwanga umbali wa zaidi ya km 7 kufuata Shule.

Hivyo Basi; kwa kushirikiana na wananchi na wadau Mbalimbali Mhe; Mbunge December, 2020 alitoa *Saruji Mifuko 100* iliyotumika kwa hatua ya awali kujenga Vyumba Vitatu Hadi hatu ya Boma.

Matarajio ni kwamba ifikapo May, 2023 vyumba hivyo vitakuwa Vimekamilika na kuanza kutumika kwa kuanza na wanafunzi wa *Darasa la kwanza* Hadi *Darasa la Tatu* (Kuwapunguzia umbali watoto wadogo) wakiendelea kutumia usajiri wa Shule wanayosoma Sasa huku michakato ya usajiri wa Shule Mpya ukiendelea.

* #*
* #*

*Taarifa Kutoka Ofisi ya Mbunge Jimbo la Rungwe 22/02/2023*Katibu wa Mbunge Jimbo la Rungwe *Gabriel Mwakagenda* Amefany...
22/02/2023

*Taarifa Kutoka Ofisi ya Mbunge Jimbo la Rungwe 22/02/2023*

Katibu wa Mbunge Jimbo la Rungwe *Gabriel Mwakagenda* Amefanya Ziara kwenye Kata za Ibighi na Ikuti.

*1. Kata ya Ibighi*
Katibu Amekabidhi *Saruji Mifuko 100* Shule ya Msingi *Katumba I*, Iliyopo Kijiji Cha Ilinga, Kata ya Ibighi, kwa niaba ya Mbunge wa Jimbo la Rungwe *Mhe; Anton Mwantona* kwa ajili ya ukamilishaji wa Chumba kimoja Cha Darasa na Ofisi moja ikiwa ni ahadi aliyoitoa Mhe; Mbunge wakati wa Ziara yake aliyoifanya Kata ya Ibighi tarehe *18/07/2022* Ziara ya kusikiliza changamoto/kero za wananchi.

Hatua hiyo ya Mhe; Mbunge inafuatia jitihada zilizoonyeshwa na wananchi hao kwa kukamilisha kufyatua tofari Baada ya hapo awali Mbunge kuwapatia *Saruji Mifuko 50*

*Kata ya Ikuti*
Akiwa Kata ya Ikuti, kwa niaba ya Mbunge wa Jimbo la Rungwe, Katibu Amekabidhi *Saruji Mifuko 100* Katika Shule ya Sekondari ya Ikuti, iliyopo Kijiji Cha Ikuti, Kata ya Ikuti, kwa ajili ya Ujenzi wa Daharia (Hostel) ya Wavulana ikiwa ni utekelezaji wa ahadi aliyoitoa Mhe; Mbunge kwenye Mahafari ya kidato Cha Nne tarehe *24/10/2022* akiwakilishwa na Katibu wake.

Kwa niaba ya Mbunge wa Jimbo la Rungwe *Mhe; Anton Mwantona* Katibu anatoa Shukrani za dhati kwa Ushirikiano na Mshikamo ulioonyeshwa na Viongozi wa Serikali, Chama na wananchi walioshiriki kwenye mapokezi ya vifaa hivyo kwenye maeneo yao. Hatua hiyo inaonyesha dhahiri dhamira na utayari Wenu katika kuwaletea Maendeleo wananchi Wenu.

* #*
*Kazi #*

*Taarifa Kutoka Ofisi ya Mbunge Jimbo la Rungwe 20/02/2023*Katibu wa Mbunge Jimbo la Rungwe *Gabriel Mwakagenda* leo 20/...
21/02/2023

*Taarifa Kutoka Ofisi ya Mbunge Jimbo la Rungwe 20/02/2023*

Katibu wa Mbunge Jimbo la Rungwe *Gabriel Mwakagenda* leo 20/02/2023 kwa niaba ya Mbunge wa Jimbo la Rungwe *Mhe; Anton Mwantona* amekabidhi jumla ya *Bati 100* zenye thamani ya *Tsh 3,500,000* kwa Uongozi wa Serikali ya Kijiji Cha *Kikota* wakiongozwa na M/kiti, Mtendaji na Wajumbe wa Halmashauri ya Serikali ya Kijiji) Mbele ya Viongozi wa Chama Cha Mapinduzi.

Bati hizo zimetolewa kwa ajili ya kukamilisha Ujenzi wa Zahanati ya Kikota. Ikiwa ni Awamu ya pili ambapo kwa Awamu ya kwanza Mhe; Mbunge alitoa Bati 100.

* #*
* #*

08/02/2023

Mbunge wa Jimbo la Rungwe Mhe; Anton Mwantona leo tarehe 08/02/2023 amepata nafasi ya kuuliza swali la nyongeza Wizara ya Ujenzi na Uchukuzi

Mhe; Mbunge amemuuliza Mhe; Naibu waziri wa Ujenzi; Je ni lini Wizara itaanza zoezi la uwekaji taa za barabarani kwenye Miji ya Kiwira, Tukuyu na Ushirika?

Akijibu Swali hilo Naibu waziri wa Ujenzi Mhe; Kasekenya amesema tayari Mkandarasi alishapatikana na yupo kwenye hatua ya Upelekaji wa Vifaa (Mobilization) kwenye maeneo yanayohusika.

Ufungaji wa Taa hizo ni Juhudi zilizofanywa na Mhe; Mbunge wa Jimbo la Rungwe kufuatia Ombi alilolitoa kwa Mhe; Rais Dkt; Samia Suluhu Hassan wakati wa Ziara ya alioifanya Wilayani Rungwe mnamo tarehe 07/08/2022 akisalimia wananchi wa Kiwira

* *
* #*

Address

Tukuyu
Tukuyu
53826

Website

Alerts

Be the first to know and let us send you an email when ofisi ya mbunge rungwe posts news and promotions. Your email address will not be used for any other purpose, and you can unsubscribe at any time.

Contact The Organization

Send a message to ofisi ya mbunge rungwe:

Share