Rais wetu MagufuliJP

Rais wetu MagufuliJP Political organization

“Nina imani kubwa kuwa watanzania wamefurahi ujio wa ndege yetu hii k**a wapo ambao hawajafurahi basi watapata tabu sana...
08/07/2018

“Nina imani kubwa kuwa watanzania wamefurahi ujio wa ndege yetu hii k**a wapo ambao hawajafurahi basi watapata tabu sana”

“Tumefufua ATCL kurejesha heshima ya nchi, ilikuwa aibu kutokuwa na ndege kwa nchi kubwa k**a Tanzania yenye sifa mbalimbali

“Ndege hizi ni matokeo ya Watanzania kulipa kodi na kuchapakazi. Nawapongeza wote walioshiriki kikamilifu, Ndege zote hizi tumenunua kwa fedha zetu wenyewe, hatujakopa kwa mtu”

“Tunataka Balozi wa Marekani utufikishie salam Boeing kuwa ile Dreamliner ya pili waikamilishe haraka, hela tunazo”

“Tumeleta ndege hizi pia ili ziimarishe na kuongeza mapato yetu ya utalii nchini, 70% ya watalii wanatumia ndege”

“Tunaboresha usafiri wa reli, barabara, waliodhani kuwa maboresho ya Bandari hayana tija sasa wameaibika, tunatekeleza kwa kasi miradi ya maji, umeme, Afya na Elimu, mwaka huu tutaanza mradi wa umeme wa Stiglers”

“Tumebana mianya yote na tunahakikisha kuwa kila hela inayopatikana inatumika kwa maslahi ya watanzania, Tanzania yenye maendeleo, Tanzania yenye sifa, Tanzania yenye neema inakuja, tumefanikiwa hili tutafanikiwa na mengine.”

Nasikitishwa na sifurahishwi na mjadala wa kuongeza kipindi cha Urais, sina mpango na wala sitarajii kuongeza kipindi ch...
13/01/2018

Nasikitishwa na sifurahishwi na mjadala wa kuongeza kipindi cha Urais, sina mpango na wala sitarajii kuongeza kipindi cha Urais. Ni kinyume na katiba.

Happy Birthday....
29/10/2017

Happy Birthday....

Watachukia, watafurahi, lakini nasema hakuna kusafirisha mchanga kokote, ni mara kumi hata wakiamua waache kuchimba dhah...
02/04/2017

Watachukia, watafurahi, lakini nasema hakuna kusafirisha mchanga kokote, ni mara kumi hata wakiamua waache kuchimba dhahabu yetu, tutaichimba tutakapokuwa na akili, kuliko kuliwa kiasi hicho.....

"Ndio maana nilimchagua waziri Mbarawa kuendesha wizara ya ujenzi huku Bara, yote ni sababu ya Muungano wetu kuwa imara ...
12/01/2017

"Ndio maana nilimchagua waziri Mbarawa kuendesha wizara ya ujenzi huku Bara, yote ni sababu ya Muungano wetu kuwa imara

Tuliamua kuanzisha utaratibu wa kutoa fedha Hazina na kuzipeleka moja kwa moja mashuleni ili kuondoa mianya ya mafisadi

Tumetenga shilingi trilioni moja kwaajili ujenzi wa reli ya kisasa (Standard Gauge) tutatumia pesa za ndani sio wafadhili.

Kuijenga Tanzania mpya inahitahi mkono wa Mungu, najua nina kazi ngumu, mimi nafanya kwa niaba yenu wananchi.

Fedha zilizokuwa zinachukuliwa na mafisadi nchi hii zilikuwa nyingi mno, ndio maana nimeamua kujitoa sadaka kwaajili yenu.

Watu walikuwa wanasafiri nje ya nchi kwa fedha za maendeleo wakati kuna wananchi wanapata shida mtaani.

Serikali ya mkoa jipangeni kwenye hilo yeyote atakayewakwamisha njooni kwangu nitamkwamua mwenyewe.

Hii nchi tumepata tabu mno, tumeteseka mno, sasa basi imetosha.

Nawahakikishia nitafanya kazi kwa ajili ya wananchi wote bila kujali chama, dini wala kabila.

Nawashukuru sana Wanashinyanga na ninaahidi kuwatumikia kwa nguvu zangu zote"

Umeme unakwenda mpaka kwa masikini walioumbwa kwa mfano wa Mungu alafu Mtu pekee sababu ya cheo unapandisha bei ya umeme...
02/01/2017

Umeme unakwenda mpaka kwa masikini walioumbwa kwa mfano wa Mungu alafu Mtu pekee sababu ya cheo unapandisha bei ya umeme‘
‘Haiwezekani unapanga mikakati kujenga viwanda na kusambaza umeme vijijini alafu Mtu sababu ya cheo chako unapandisha bei ya umeme‘
‘Namshukuru Waziri wa Nishati ameshatengua maamuzi kwa hiyo umeme hakuna kupanda, majipu bado yapo na nitaendelea kuyatumbua.....

'Mikopo mingi imeenda kwa wasio walengwa na wengi Wanasiasa, niko serikalini najua, wengine wanadaiwa Mabilioni na ndio ...
07/11/2016

'Mikopo mingi imeenda kwa wasio walengwa na wengi Wanasiasa, niko serikalini najua, wengine wanadaiwa Mabilioni na ndio wapiga kelele'

'Narudia tena..... wakati wa kupiga dili haupo tena, wale wa serikalini waliokua wanapiga dili hawatapiga tena sanasana watapigwa wao'

'Tuliposimamisha ajira kwa miezi miwili haikua na maana zimezuiliwa, sasa hivi zinaendelea na juzi tumetoa za Madaktari.

'Sasa hivi tunaajiri lakini kwa uangalifu tusije kuwarudisha Watumishi hewa, hizi fedha zilizokua zinawalipa ni fedha za maskini'

'Takwimu za kutosafiri mimi na wengine kiasi gani tumeokoa ijulikane tu ni Mabilioni na isieleweke hatusafiri kabisa, pia tuna Mabalozi'.

'Msafara wa Rais kwenda nje ya nchi unabeba mpaka watu 40 lakini unapomtuma Waziri unaweza kukuta ni watu wawili'

'Sheria mpya ya huduma za habari, sifahamu Wabunge watachoamua ila sitaki unafiki siku itakayoletwa kwangu siku hiyohiyo nitaisaini'

'Utaona Vita hizi tunazozipata ni za maslahi, ni bora nisiwe Rais maarufu lakini siku moja mtanikumbuka au nitakua maarufu mbinguni.

'Kuhusu katiba mpya niache kwanza niinyooshe nchi, hata kwenye kampeni zangu nilikozunguka hakuna mahali nilizungumzia katiba mpya'

'Wanasiasa wanamamidomo kweli utadhani ni wasafi, hizi ni changamoto ambazo naziona.. Waandishi mnawalinda'

'Matunda yameanza kuonekana, nidhamu kazini imeanza kuonekana, tumepitisha sheria ya kupambana na mafisadi, kesi ya kwanza imeanza jana'

'Katika kazi yoyote kukosolewa na kupongezwa ni kitu cha kawaida, katika muda wote niliochaguliwa kuwa Rais sijagandamiza demokrasia'

'Nimefanikiwa kubana matumizi, nimealikwa mialiko 47 nje ya nchi lakini nimekwenda mitatu, mingine watakwenda Mabalozi.

'Yako mazungumzo kununua Ndege boeing abiria 242, hatuwezi kukuza utalii kwa kubahatisha lazima tuwe na ndege itokayo kwao mojakwamoja'- Rais Magufuli.

Ninamshukuru Mungu kufikia siku yangu ya kuzaliwa,ninawashukuru watanzania nyote kwa kuniombea.Nitafanya kazi kwa moyo n...
29/10/2016

Ninamshukuru Mungu kufikia siku yangu ya kuzaliwa,ninawashukuru watanzania nyote kwa kuniombea.Nitafanya kazi kwa moyo na nguvu zangu zote.....Ninaahidi kuendelea kufanya kazi kwa moyo na nguvu zangu zote kwa ajili ya maendeleo ya Taifa. Mungu Ibariki Tanzania.

JNIA 28/09/2016=> Rais Magufuli: Lakini unaweza ukajiuliza, ndege hii imetoka Canada imefika hapa, watu wanasema hazina ...
29/09/2016

JNIA 28/09/2016
=> Rais Magufuli: Lakini unaweza ukajiuliza, ndege hii imetoka Canada imefika hapa, watu wanasema hazina spidi, ni bajaji.

=> Rais Magufuli: Ndege hizi hazitumiki tu Tanzania, Marekani wana ndege zaidi ya 40 za aina hii, Misri wanazo-

=> Rais Magufuli: Ukitaka kujenga uchumi, kuinua utalii, huwezi kufanya k**a taifa halina ndege- Rais

=> Rais Magufuli: Ndege ya Jeti, kutoka Dar hadi Mbeya mafuta ni milioni 28, lakini hizi ni milioni moja

=> Rais Magufuli: K**a mtu anaona ana haraka sana ya kuwahi anapokwenda, akapande ndege za jeshi awahi

=> Rais Magufuli: Kutoka Dar hadi Mbeya, tofauti ya muda wa kufika kati ya ndege hii na Jet ni dakika 20 tu-

=> Rais Magufuli: Niwaombe watanzania tusipende kubeza, k**a kitu hukitaki, basi ukae kimya

=> Rais Magufuli: Tungenunua ndege hizi kwa kulipa polepole, tungekuja kulipa gharama kubwa, ndio maana tumelipa zote

=> Rais Magufuli: Tuna mpango wa kununua ndege mbili kubwa, moja itabeba watu 160, nyingine itabeba watu 240

=> Rais Magufuli: Tuliamua kununua ndege, tutazikodisha kwa ATCL, mwendo wa kucheza sasa umekwisha

=> Rais Magufuli: ATCL ilikuwa haijiendeshi kibishara, walikuwa wapo tu, wanategemea serikali kila kitu

=> Rais Magufuli: ATCL haikuwa ikijenga uchumi wa nchi na utalii k**a ilivyokuwa inatakiwa

=> Rais Magufuli: Maofisa wa ATCL walikuwa wakijilipa posho za TZS 50,000 kila wakitembelea uwanja wa ndege Dar-

=> Rais Magufuli: Vituo vya ATCL vya Comoro, Mwanza, Mtwara na Dar es Salaam, vilikithiri kwa ubadhirifu

=> Rais Magufuli: ATCL walikuwa hawafuati ratiba, unaweza kuambiwa ndege inaondoka leo, lakini isiondoke hadi wiki moja

=> Rais Magufuli: ATCL walikuwa wakijilipa overtime za uongo

=> Rais Magufuli: ATCL walikuwa wakinunua mafuta hewa, unaambiwa ndege imeenda Mwanza kumbe iko Dar es Salaam uwanjani

=> Rais Magufuli: Katika kituo cha Comoro, ilipotea TZS milioni 700, aliyepoteza akaongezewa muda ili apoteze nyingine

=> Rais Magufuli: Bodi ya ATCL naomba mchambuwe wafanyakazi, chambueni k**a Saida Karoli anavyosema, chambua k**a karanga

=> Rais Magufuli: Bodi ya ATCL msiogope kupunguza wafanyakazi, tulipunguza 500 wa NIDA, hawa hawatatushinda

=> Rais Magufuli: Mfanyakazi k**a unataka kuendelea kufanya kazi ATCL, utubu, uwe tayari kuwatumikia watanzania

=> Rais Magufuli: Ndani ya ATCL kuna wake wa Mawaziri, Shirika halizalishi lakini wake wa Mawaziri wameng'ang'ani tu

=> Rais Magufuli: Wale ambao hawawezi kwenda na mwendo wetu, waje tuwalipe fedha zao watuache tufanyekazi

=> Rais Magufuli: Haiwezekani wageni wakitaka kuja Tanzania, lazima watue nchi nyingine, hii ni aibu kubwa

=> Rais Magufuli: Lakini mjue mnaenda kwenye ushindani, washindani wenu hawatawafurahia, mjipange vizuri kuwakabili-

=> Rais Magufuli: Niwaombe Bodi ya ATCL, msitumie mawakala kukatisha tiketi zenu

=> Rais Magufuli: Kuna wafanyakazi wa ATCL naona wapo wanafanya kazi tangu mimi nipo shule ya msingi

=> Rais Magufuli: ATCL ya sasa ukiona hata sare za wafanyakazi zinatia kichefuchefu, hazitamaniki

=> Rais Magufuli: Lakini niwaombe Watanzania tuwe wazalendo, tutumie usafiri wa ATCL ili tuweze kununua ndege nyingine

=> Rais Magufuli: Niwaombe Bodi na Menejimenti, msimruhusu kiongozi asafiri bure, hata k**a ni mimi, mnitoze nauli

=> Rais Magufuli: Najua kunawakati ATCL mnajipendekeza kwa viongozi, lakini mjue mwishoni tutawapima kwa utendaji wenu

=> Rais Magufuli: Hata k**a ni kiongozi wa ATCL, ukisafiri hakikisha unalipa nauli, vitu vya bure ndivyo vinatumaliza-

=> Rais Magufuli: Sasa tuna kazi ya kukarabati viwanja, shughuli hii tutaianza mapema sababu fedha tunazo

=> Rais Magufuli: Sisi hatutaki kufukuza wafanyakazi, lakini watajifukuzisha wenyewe kutokana na utendaji wao

=> Rais Magufuli: Ujenzi wa reli ya kisasa kutoka Dar- Mwanza- Kigali- Bujumbura tayari tenda zimetangazwa

=> Rais Magufuli: Tunataka kuanza ujenzi wa treni za umeme Dar es Salaam, haya si Ulaya tu, hata hapa yatafanyika

=> Rais Magufuli: Ujenzi wa daraja la Coco Beach hadi Agha Khan umeanza, Interchange ya Ubungo itaanza karibuni

=> Rais Magufuli: Mkoa wa Dar es Salaam, una jumla ya wanafunzi hewa 7000, Wafanyakazi hewa wapo 17,000

=> Rais Magufuli: Hii nchi ilikuwa imefika pabaya, kila kona ukigeuka ni hewa, hewa, hewa

=> Rais Magufuli: RAS, DED tuliowafukuza jana, leo wamefikishwa mahak**ani, hii imesaidia Uingereza kutuchangia bilioni 6

=> Rais Magufuli: Uingereza imetuchangia bilioni 6 sababu wameona wakitupa fedha zao zitafika kwa walengwa kule Kagera

=> Rais Magufuli: Tunakagua vyeti ili kujua viwango vya elimu na sehemu watu waliposoma, lengo si kuwafukuza wafanyakazi

=> Rais Magufuli: Ndugu zangu kazi hii ni ngumu, Mawaziri msiwaone, hawana raha hawa

=> Rais Magufuli: Waandishi wa habari, ninyi ni muhimili k**a ilivyo Bunge, tusaidiane tunapochukua hatua-

=> Rais Magufuli: Waandishi wakati mwingine mnaandika habari za uongo k**a nyie mna mahali pengine pakuishi ila si hapa

=> Rais Magufuli: Watanzania mjue, tukishindwa sisi, tumeshindwa sote, tukiweza tumeweza wote

=> Rais Magufuli: No research, no right to speak, lakini hapa ni kinyume, watu hawajui lakini wanaongoza kuongea

=> Rais Magufuli: K**a kungewezekana mtu ukiwa Rais baada ya miaka miwili na nusu unamuachia mwingine, mimi ningefurahi-

=> Rais Magufuli: Natamani huyo aliyesema hazina spidi nimjue nimlipie nauli akae mbele aone zinavyokata mawingu-

=> Rais Magufuli: Ninaishukuru CCM kwa kuandika ilani inayotekelezeka, naamini tutafanya zaidi

=> Rais Magufuli: Mungu ibariki ATCL, Mungu bariki Bodi ya ATCL, Mungu bariki wafanyakazi wazuri, Mungu ibariki Tanzania

"..Serikali ninayoiongoza, ilichaguliwa na masikini...K**a matajiri walifikiri nitakuwa upande wao basi wamenoa. Mimi ni...
15/05/2016

"..Serikali ninayoiongoza, ilichaguliwa na masikini...K**a matajiri walifikiri nitakuwa upande wao basi wamenoa. Mimi nilichaguliwa na masikini na nitawatumikia masikini na si matajiri."-----Rais Magufuli.

Rais Magufuli anaposema matajiri anamaanisha wale wanaojitajirisha kwa mgongo wa wananchi - wakwepa kodi, wafanya magendo, wauza madawa ya kurevya, wala rushwa na mafisadi...

“Sitojali idadi ya watu nitakaowasimamisha au kuwafuta kazi hata ikifikia 2,000...Ninachoangalia na kujali ni watanzania...
05/03/2016

“Sitojali idadi ya watu nitakaowasimamisha au kuwafuta kazi hata ikifikia 2,000...Ninacho
angalia na kujali ni watanzania milioni 50 wafaidike" ---Rais John Pombe Magufuli.

“Nimekuwa nasema nchi yetu si masikini. Hii nchi ni tajiri sana, lakini wapo watu wamekuwa wanajinufaisha wao. Wapo taya...
25/02/2016

“Nimekuwa nasema nchi yetu si masikini. Hii nchi ni tajiri sana, lakini wapo watu wamekuwa wanajinufaisha wao. Wapo tayari wapokee virushwa ili waneemeke wao huku Watanzania wengi wakiumia na kuteseka. “Ndio maana nasisitiza kwamba nitaendelea kutumbua majipu ya viongozi mafisadi na wala rushwa''-Rais Magufuli.

Address

Ukonga

Website

Alerts

Be the first to know and let us send you an email when Rais wetu MagufuliJP posts news and promotions. Your email address will not be used for any other purpose, and you can unsubscribe at any time.

Share