ULEMO MPYA

ULEMO MPYA Contact information, map and directions, contact form, opening hours, services, ratings, photos, videos and announcements from ULEMO MPYA, Political organisation, Ulemo.

COUNTRY  BOY ATAKUWEPO 🗓24 JULAI 2026WIWANJA VYA SHULE YA MSINGI MISIGIRII
22/07/2026

COUNTRY BOY ATAKUWEPO

🗓24 JULAI 2026
WIWANJA VYA SHULE YA MSINGI MISIGIRII

JUMA NATURE ATAKUWEPO 🗓24 JULAI 2026WIWANJA VYA SHULE YA MSINGI MISIGIRII
22/07/2026

JUMA NATURE ATAKUWEPO

🗓24 JULAI 2026
WIWANJA VYA SHULE YA MSINGI MISIGIRII

DC MWENDA AZINDUA JUKWAA LA VIJANA IRAMBA: AHIMIZA UZALENDO NA USHIRIKI WA VIJANA KATIKA UJENZI WA TAIFAMkuu wa Wilaya y...
21/07/2026

DC MWENDA AZINDUA JUKWAA LA VIJANA IRAMBA: AHIMIZA UZALENDO NA USHIRIKI WA VIJANA KATIKA UJENZI WA TAIFA

Mkuu wa Wilaya ya Iramba, Alhaji Suleiman Yusuph Mwenda, leo tarehe 21 Julai, 2026, amezindua rasmi Jukwaa la Vijana la Halmashauri ya Wilaya ya Iramba (Vijana Platform), ikiwa ni maandalizi ya mapokezi ya Mwenge wa Uhuru Wilayani Iramba tarehe 24 Julai, 2026, na kuwataka vijana kuwa wazalendo kwa kuthamini na kujivunia mafanikio yanayopatikana katika sekta mbalimbali nchini.

Akizungumza wakati wa uzinduzi huo, uliofanyika katika Ukumbi Mkubwa wa Halmashauri ya Wilaya ya Iramba, DC Mwenda amesema vijana wana wajibu mkubwa wa kushiriki kikamilifu katika ujenzi wa taifa, akisisitiza kuwa wao ndiyo nguvu kazi ya nchi na kwamba utekelezaji wa miradi ya maendeleo unategemea mchango na ushiriki wao.

“ipendeni nchi yenu, wapendeni viongozi wenu, hatuna nchi nyingine zaidi ya hii Tanzania”

Aidha, amewahimiza vijana kuwa na maono makubwa ya maisha, kuendelea kuwekeza katika elimu na ujuzi, pamoja na kutumia uwezo wao kuleta maendeleo binafsi na ya jamii kwa ujumla.

Katika kongamano hilo, vijana wamepatiwa elimu kupitia mada mbalimbali zilizolenga kuwajengea uwezo, kuimarisha uzalendo na maadili mema, pamoja na kuwawezesha kushiriki kikamilifu katika maendeleo ya Taifa. Mada hizo zilihusu uzalendo na uraia, amani na mshikamano wa jamii, mapambano dhidi ya dawa za kulevya na rushwa, pamoja na matumizi ya fursa za kiuchumi zilizopo katika mazingira yao.



MASAI ATAKUWEPO MKESHA WA MWENGE WA UHURU MISIGIRI
21/07/2026

MASAI ATAKUWEPO MKESHA WA MWENGE WA UHURU
MISIGIRI

CHEGE CHIGUNDA ATAKUWEPO MKESHA WA MWENGE
21/07/2026

CHEGE CHIGUNDA ATAKUWEPO MKESHA WA MWENGE

KONGAMANO  LA VIJANA LA MWENGE WA UHURUWILAYA YA IRAMBA 🗓21 JULY 2026UKUMBI  MKUBWA WA  HALMASHAURI Mgeni rasmi. Mhe Alh...
20/07/2026

KONGAMANO LA VIJANA LA MWENGE WA UHURU
WILAYA YA IRAMBA
🗓21 JULY 2026

UKUMBI MKUBWA WA HALMASHAURI

Mgeni rasmi. Mhe Alhaj Suleiman Yusuph Mwenda

18/07/2026
Mkuu wa Wilaya ya Iramba, Alhaj Suleiman Yusuph Mwenda, akisalimiana na wanafunzi wa Kidato cha Tano wanaosoma tahasusi ...
18/07/2026

Mkuu wa Wilaya ya Iramba, Alhaj Suleiman Yusuph Mwenda, akisalimiana na wanafunzi wa Kidato cha Tano wanaosoma tahasusi ya CBG katika Shule ya Sekondari Kizaga, wakati wa ziara yake ya kukagua miradi itakayopitiwa na Mwenge wa Uhuru 2026.

Akizungumza na wanafunzi hao, Alhaj Mwenda amewahimiza kuweka kipaumbele katika masomo, kuwa na nidhamu, kujituma na kutumia ipasavyo muda wao ili kufikia malengo ya kitaaluma na kuwa viongozi bora wa Taifa hapo baadaye.

Amesema Serikali ya Awamu ya Sita, chini ya uongozi wa Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan, imeendelea kufanya maboresho makubwa katika sekta ya elimu kwa kujenga na kuboresha miundombinu ya shule, kuongeza vifaa vya kufundishia na kujifunzia, pamoja na kuweka mazingira wezeshi yanayowawezesha wanafunzi kupata elimu bora yenye ushindani wa kitaifa na kimataifa.

"Serikali imewatengenezea mazingira mazuri ya kujifunzia. Jukumu lenu ni kuyatumia vyema kwa kusoma kwa bidii, kuwa na nidhamu na kufanya vizuri katika masomo yenu ili muwe wataalamu na viongozi watakaoendelea kuijenga Tanzania," amesema Alhaj Mwenda.

Aidha, amewasisitiza wanafunzi hao kuzingatia maadili mema, kujiepusha na vitendo vinavyoweza kuathiri masomo yao, na kuwa mabalozi wa uzalendo, umoja na maendeleo katika jamii.

Address

Ulemo

Website

Alerts

Be the first to know and let us send you an email when ULEMO MPYA posts news and promotions. Your email address will not be used for any other purpose, and you can unsubscribe at any time.

Shortcuts

Share