ZPRA

ZPRA Contact information, map and directions, contact form, opening hours, services, ratings, photos, videos and announcements from ZPRA, Government Organization, Maisara, Unguja.

Zanzibar Petroleum Regulatory Authority (ZPRA) is a government institution established under Section 8 of Zanzibar Oil and Gas Upstream Act, No 6 of 2016 to Monitor and Regulate Exploration, Development and Production of Petroleum in Zanzibar.

26/04/2026
Kikao cha Kamati ya Ufundi ya pamoja baina ya Mamlaka ya Udhibiti wa Utafutaji na Uchimbaji wa Mafuta na Gesi Asilia Zan...
18/03/2026

Kikao cha Kamati ya Ufundi ya pamoja baina ya Mamlaka ya Udhibiti wa Utafutaji na Uchimbaji wa Mafuta na Gesi Asilia Zanzibar (ZPRA) na Mamlaka ya Udhibiti wa Mkondo wa Juu wa Petroli (PURA).

Kikao hicho pamoja na ajenda nyengine kitajumuisha kupokea na kujadili taarifa ya utekelezaji kwa kipindi cha Julai 1, 2025 hadi Machi 31, 2026. Sambamba na kuandaa ripoti ya utekelezaji kwa kipindi cha Julai 1, 2025 hadi Machi 31, 2026.

Hati ya Mashirikiano (MoU) baina ya ZPRA na PURA imelenga kuimarisha ufanisi na kujengeana uwezo katika maeneo mbalimbali ikiwemo: Masuala ya Sheria, Usimamizi wa Data, Usimamizi wa Mkataba (PSA), Ushirikishwaji wa wazawa katika Sekta ya Mafuta na Gesi Asilia, pamoja na kujengeana uwezo katika nyanja mbalimbali kwa wafanyakazi wa Mamlaka hizo.

Kikao hicho ni cha kawaida kwa mujibu wa utaratibu wa vikao vya Kamati hiyo ambavyo hufanyika kila Robo Mwaka kwa kukutana Zanzibar au Tanzania Bara ambapo kwa mara hii Kikao hicho kinafanyika Zanzibar katika Ukumbi wa Mikutano wa ZPRA Maisara Zanzibar.

22/01/2026
Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi ya Mamlaka ya Udhibiti wa Utafutaji na Uchimbaji wa Mafuta na Gesi Asilia Zanzibar Dkt...
15/01/2026

Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi ya Mamlaka ya Udhibiti wa Utafutaji na Uchimbaji wa Mafuta na Gesi Asilia Zanzibar Dkt. Omar D. Shajak amesema Mamlaka ya Udhibiti wa Utafutaji na Uchimbaji wa Mafuta na Gesi Asilia Zanzibar (ZPRA) na Mamlaka ya Udhibiti wa Mkondo wa Juu wa Petroli (PURA) zinahitaji kuwa na dhamira ya dhati ya kushirikiana kwa ajili ya maendeleo ya Sekta ya Mafuta na Gesi Asilia nchini.

Ameyasema hayo wakati wa kikao cha Uongozi baina ya Mamlaka ya Udhibiti wa Utafutaji na Uchimbaji wa Mafuta na Gesi Asilia Zanzibar (ZPRA) na Mamlaka ya Udhibiti wa Mkondo wa Juu wa Petroli (PURA) walipokutana kutambulishana na kujadili mambo mbalimbali ya maendeleo ya Mafuta na Gesi Asilia.

Dkt. Shajak ameongeza kuwa kupitia makubaliano ya Hati ya mashirikiano (MoU) ZPRA na PURA zinategemea kuendelea kufanya kazi kwa pamoja na kwa mashirikiano makubwa kupitia ili kufikia malengo ya uwepo wa Taasisi hizi sambamba na kupata matokeo yatakayo jibu mategemeo ya Watanzania wote.

Aidha, Dkt. Shajak amewataka watendaji wa Taasisi hizo mbili kufanya kazi kwa karibu zaidi ili kuleta maendeleo katika Sekta ya Mafuta na Gesi Asilia.

Pia, ameushukuru Uongozi wa PURA kwa kuja kujitambulisha na kusalimiana sambamba na kupata nafasi ya kujadili mambo mbalimbali ya maendeleo ya Sekta ya Mafuta na Gesi Asilia kwa maslahi mapana ya Tanzania.

Kwa upande wake Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi ya Mamlaka ya Udhibiti wa Mkondo wa Juu wa Petroli (PURA) Bwana Khalfan R. Khalfan ameeleza mafanikio yaliyopatikana kupitia utekelezaji wa Hati ya mashirikiano (MoU) baina ya ZPRA na PURA ikiwa ni pamoja na kukabidhi data za Mafuta na Gesi Asilia kutoka Tanzania Bara kwa vitalu vinavyopatikana Zanzibar pamoja na Visima vya awali vya utafiti wa Mafuta na Gesi Asilia.

Aliongeza mafanikio mengine ikiwa ni kubadilishana uzoefu wa utayarishaji wa Mkataba Kifani wa Uzalishaji (Model Production Sharing Agreement), utendaji kwa Bodi za Wakurugenzi, utangazaji wa Vitalu pamoja na kujenga uwezo wa kiutendaji kwa wataalamu wa Mamlaka hizi mbili.

Kikao hicho ni muendelezo wa utekelezaji wa Hati ya Mashirikiano baina ya ZPRA na PURA iliyosainiwa Mwezi wa Febuari 2022.

Waziri wa Uchumi wa Buluu na Uvuvi Mheshimiwa Masoud Ali Mohammed amekutana na kuzungumza na Uongozi wa Mamlaka ya Udhib...
15/01/2026

Waziri wa Uchumi wa Buluu na Uvuvi Mheshimiwa Masoud Ali Mohammed amekutana na kuzungumza na Uongozi wa Mamlaka ya Udhibiti wa Mkondo wa Juu wa Petroli (PURA) walipofika ofisini kwake kwa lengo la kumsalimia na kujitambulisha.

Mheshimwa Masoud amesema kuwa Mamlaka za udhibiti za ZPRA na PURA zina jukumu la msingi la kuhakikisha Sekta ya Mafuta ya Mafuta na Gesi Asilia inaendelea kukua na kuleta manufaa kwa wananchi wa Tanzania.

Amesema ”Naamini Bodi zetu zote mbili zina uwezo mkubwa wa kuhakikisha kuwa sote tunapata matokeo ya haraka katika Sekta ya Mafuta na Gesi Asilia, hivyo tufanye kazi kwa pamoja ili ifike siku kila mmoja afurahi kwa mafanikio kupitia ushirikiano wa Taasisi mbili hizo”.

Amesema anafarajika kuona Mamlaka zinafanya kazi kwa karibu na amewataka ZPRA na PURA kujenga udugu na kutembea bega kwa bega ili kupata mafanikio kwa pamoja ndani ya nchi yetu.

Mheshimwa Masoud amewataka kuendeleza mashirikiano yaliyopo kwa maslahi ya pande zote mbili pamoja na kuendeleza kuimarisha utamduni wa kutatatua changamoto zitakazojitokeza bila ya kuchelewa kwa ajili ya kupata matokeo ya haraka.

Aidha, amewataka Viongozi hao kuweka mkazo
zaidi katika kuwaendeleza waatalamu kupitia mafunzo ya vitendo ili kuwa na watendaji wenye uwezo na ujuzi wa kuendeleza Sekta hiyo.

Waziri Masoud amewashukuru Viongozi hao kwa kumtembelea na kusalimiana na kuwatakia kila la kheri katika kutekeleza majukumu yao kwa masalahi ya wananchi.

Kwa upande wake Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi ya Mamlaka ya Udhibiti wa Utafutaji na Uchimbaji wa Mafuta na Gesi Asilia Zanzibar Dkt. Omar D. Shajak ametoa salamu za shukrani kwa Ujumbe huo pamoja kuelezea nia ya dhati ya ZPRA ya kuendeleza mashirikiano na PURA kwa lengo la kukuza Sekta ya Mafuta na Gesi Asilia kwa maendeleo ya Tanzania.

Naye Mweneyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi ya Mamlaka ya Udhibiti wa Mkondo wa Juu wa Petroli (PURA) Bwana Khalfan R. Khalfan ameeleza kuwa mashirikiano baina ya PURA na ZPRA yameleta mafanikio makubwa ikiwemo kubadilishana data za Mafuta na Gesi Asilia na kubadilishana uzoefu katika shuhuli nyengine za kitaalamu.

Waziri wa Uchumi wa Buluu na Uvuvi Mhe. Masoud Ali Mohamed ameitaka Bodi ya Wakurugenzi ya Mamlaka ya Udhibiti wa Utafut...
13/01/2026

Waziri wa Uchumi wa Buluu na Uvuvi Mhe. Masoud Ali Mohamed ameitaka Bodi ya Wakurugenzi ya Mamlaka ya Udhibiti wa Utafutaji na Uchimbaji wa Mafuta na Gesi Asilia Zanzibar (ZPRA) kuwa na ushirikiano katika utendaji kazi ili kutimiza malengo ya Serikali ya kuwaletea wananchi maendeleo.

Ameyasema hayo katika kikao na Bodi ya Wakurugenzi ya ZPRA huko Ofisini kwake Maisara Mkoa wa Mjini Magharibi amesema kuwa endapo Bodi hiyo itaendelea kutoa ushirikiano kwa Wizara pamoja na kwa Tasisi ya ZPRA katika utendaji kazi itasaidia kufanikisha malengo yaliyoainishwa katika Sheria ya uanzishwaji na utendaji kazi wa ZPRA.

Aidha ameitaka Bodi hiyo kufanyakazi iliyoainisha katika Sheria ya ZPRA Namba 6 ya Mwaka 2016, ikiwemo kumshauri Waziri kwa lengo la kuimarisha Sekta ya Mafuta na Gesi Asilia na kuongeza ufanisi.

Amefafanua kuwa Bodi inajukumu la kumshauri Waziri pamoja na kusimamia utendaji wa Taasisi husika ili kuweza kufikia malengo yaliyousudiwa ya kuleta maendelo katika nchi.

Waziri Masoud amesisitiza kuwa na uharaka katika utendaji kazi ili kuendana na kasi ya Serikali ya Awamu ya Nane kuweza kupata matokeo ya maendeleo kwa haraka.

“Tunapokuwa na jambo lolote ambalo tunadhani jambo hilo lisingeweza kutekelezeka bila ya kupata ridhaa au ushauri kutoka kwenye Bodi, tuweke utaratibu pembeni kwa dhamira njema ili kuharakisha jambo hilo” alieleza.

Akitoa wito kwa wajumbe wa Bodi pamoja na watendaji wa ZPRA amewasisitiza kuwa tayari kusimamia wakiwa wadhibiti wa shuhuli za Mafuta na Gesi Asilia ili kupata matokeo chanya ambayo yamekusudiwa yaonekane kwa wananchi, lengo kuzifikisha Taasisi za mafuta na gesi katika hatua nyengine za kimaendeleo.

Nae Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi ya Mamlaka ya Udhibiti wa Utafutaji na Uchimbaji wa Mafuta na Gesi Asilia Zanzibar, Dkt. Omar Dadi Shajak amesema mikakati ya kikao hicho ni pamoja na kuweka mbele malengo ya Serikali hasa katika masuala ya Mafuta na Gesi Asilia ili kutimiza dhamira ya Serikali.

Kwa upande wake Mkurugenzi Mwendeshaji ZPRA Mhandisi Mohamed Slum Said ambae pia Mjumbe wa Bodi hiyo amesema Serikali imeazimia kuipeleka Sekta ya Mafuta na Gesi Asilia katika hatua kubwa ya maendeleo na kuimarisha nchi.

Kikao hicho kimejadili mipango ya Serikali katika sekta ya Mafuta na Gesi Asilia ili kuwapatia wananchi maendeleo mazuri kupitia sekta hiyo.

Salaam za Pongezi
06/01/2026

Salaam za Pongezi

Mhandisi wa Mafuta na Gesi Asilia ndugu Sharifa H. Othaman kutoka Mamlaka ya Udhibiti wa Utafutaji na Uchimbaji wa Mafut...
31/12/2025

Mhandisi wa Mafuta na Gesi Asilia ndugu Sharifa H. Othaman kutoka Mamlaka ya Udhibiti wa Utafutaji na Uchimbaji wa Mafuta na Gesi Asilia Zanzibar (ZPRA) akitoa uelewa wa masuala mbalimbali ya Mafuta na Gesi Asilia kwa wafanyakazi wa Taasisi ya Utafiti wa Uvuvi na Mazao za Baharini ( ZAFIRI) katika mkutano wa kujenga uelewa juu masuala ya Mafuta na Gesi Asilia Zanzibar.

Address

Maisara
Unguja

Opening Hours

Monday 08:00 - 16:00
Tuesday 08:00 - 16:00
Wednesday 08:00 - 16:00
Thursday 08:00 - 16:00
Friday 08:00 - 16:00

Website

Alerts

Be the first to know and let us send you an email when ZPRA posts news and promotions. Your email address will not be used for any other purpose, and you can unsubscribe at any time.

Share