Wizara ya Uchumi wa Buluu na Uvuvi Zanzibar

Wizara ya Uchumi wa Buluu na Uvuvi Zanzibar Contact information, map and directions, contact form, opening hours, services, ratings, photos, videos and announcements from Wizara ya Uchumi wa Buluu na Uvuvi Zanzibar, Government Official, ZURA BUILDING, MAISARA, Zanzibar City.

Wizara ya Uchumi wa Buluu na Uvuvi Zanzibar na Wizara ya Mifugo na Uvuvi ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania imefanya Kon...
13/08/2026

Wizara ya Uchumi wa Buluu na Uvuvi Zanzibar na Wizara ya Mifugo na Uvuvi ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania imefanya Kongamano la Uchumi wa Buluu katika Tamasha la Kizimkazi likiwa na kaulimbiu ya Hifadhi Bahari, Changamkia Fursa za Uchumi wa Buluu lililofanyika katika Hoteli ya Kwanza Kizimkazi.

Kongamano hilo limefunguliwa na Naibu Waziri wa Wizara ya Uchumi wa Buluu na Uvuvi Zanzibar Mheshimiwa Mboja Ramadhan Mshenga ambaye ameelezea umuhimu wa uhifadhi wa bahari, maziwa na mito ili yawe na matumizi endelevu kwa maslahi ya wananchi na taifa kwa ujumla.

Naibu Waziri amesisitiza kuwa kuna fursa nyingi za kiuchumi katika sekta hiyo ya maji ikiwemo kuongeza uwekezaji wa ndani, kikanda na kimataifa, kuzigeuza changamoto kuwa fursa za kiuchumi na kukuza na kuimarisha utamaduni wa Watanzania na kupambana na kupiga vita uvuvi haramu ambao unarudisha nyuma malengo katika sekta hiyo.

Akifunga Kongamano hilo Naibu Waziri wa Wizara ya Mifugo na Uvuvi ya Serikali ya Jamhuri ya Tanzania Mheshimiwa Ng’wasi Damas Kamani amehimiza ushirikiano wa Taasisi, nchi, kikanda na kimataifa wa uhifadhi na ulinzi wa bahari, kupambana na uvuvi haramu, mabadiliko ya tabianchi na uchafuzi wa mazingira wa taka hasa za plastiki ili kuyafanya maji barani Afrika kuwa salama na yenye tija.

Pamoja na uhifadhi wa bahari aidha amehimiza kutumia teknolojia, kufanya utafiti na ubunifu katika kuongeza mchango wa sekta ya uvuvi kupitia uzalishaji wenye tija, kuongeza thamani na kuimarisha ushindani wa mazao nchini.

Kongamano hilo pia lilijumuisha utiaji Saini wa hati ya makuballiano baina ya Kampuni ya Mwani Zanzibar ZASCO na Mamlaka ya Udhibit wa Mbolea Tanzania TFRA, yakiwa na lengo la kuwezesha uzalishaji na udhibiti wa mbolea ya kimiminika inayotokana na mwani.

Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Mheshimiwa Hemed Suleiman Abdulla amesema kaulimbiu ya Okoa Mvuvi, Ongeza Uzalishaji ...
11/08/2026

Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Mheshimiwa Hemed Suleiman Abdulla amesema kaulimbiu ya Okoa Mvuvi, Ongeza Uzalishaji wa Samaki iende sambamba na utekelezaji wake kwa vitendo kwa kumuwezesha na kumuinua mvuvi kiuchumi.

Akizindua program ya Okoa Mvuvi, Ongeza Uzalishaji wa Samaki, iliyofanyika Uroa Pongwe, Mheshimiwa Hemed amesema kuimarisha ustawi wa mvuvi na kuzingatia usalama wake ni jambo muhimu ikiwemo kupewa zana za kisasa zinazohimili mabadiliko ya hali ya hewa baharini zitakazowakinga na majanga kazini.

Mheshimiwa Hemed amesema program ya Okoa Mvuvi itakuwa sehemu ya msingi ya ukuaji wa sekta ya uvuvi inayokwenda sambamba na kuongezeka kwa uzalishaji wa zao la Samaki na mwani ambao unatoa matokeo chanya ya ukuaji wa sekta ya uvuvi.

Hivyo Makamu wa Pili wa Rais ametoa wito kwa wananchi kuchangamkia fursa za kiuchumi katika sekta ya uvuvi ambayo itakuwa ni msingi mkuu wa kiuchumi ambao una fursa nyingi za kiuchumi ambazo hazijatumika ipasavyo na kuzitunza vifaa vya uvuvi vinavyotolewa ili kupata nguvu ya kupambana na uvuvi haramu.

Mapema Naibu Waziri wa Uchumi wa Buluu na Uvuvi Zanzibar Mheshimiwa Mboja Ramadhan Mshenga amesema mpango wa Serikali ni kuhakikisha kuwa kila diko linakuwa na boti za uokozi zenye zana za kisasa kwa lengo la kuweka mazingira salama ya wavuvi na watumiaji wengine wa bahari.

Amesema madhumuni ya program ya Okoa mvuvi ni kumlinda na kumpa hadhi ya kiuchumi mvuvi, kuwa na mazingira salama ya kufanyia kazi kurasimishwa katika taasisi za kifedha na kuweza kupata mikopo hali itakayoinua kipato chao na taifa kwa ujumla.

Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar, Mhe. Hemed Suleiman Abdulla, anatarajiwa kuwa mgeni rasmi katika uzinduzi wa Kampeni...
09/08/2026

Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar, Mhe. Hemed Suleiman Abdulla, anatarajiwa kuwa mgeni rasmi katika uzinduzi wa Kampeni ya Okoa Mvuvi, unaotarajiwa kufanyika Agosti 10, 2026 katika maeneo ya Uroa Pongwe, Zanzibar.

Akizungumza na waandishi wa habari katika Ukumbi wa Wizara ya Uchumi wa Buluu na Uvuvi, Maisara, Mkoa wa Mjini Magharibi, Katibu Mkuu wa Wizara hiyo, Cap. Hamad Bakar Hamad, amesema kampeni hiyo imelenga kuimarisha usalama wa wavuvi na kuhakikisha wanaokolewa kwa haraka wanapokumbwa na majanga baharini.

Amesema kampeni hiyo inalenga kuwarasimisha wavuvi nchini ili waweze kutambuliwa na kupata huduma za uokozi wanapokumbwa na majanga.

Cap. Hamad amesema uamuzi huo umetokana na takwimu zinazoonesha kuwa zaidi ya wavuvi 100 kwa mwaka hukumbwa na matukio ya kuzama ambapo asilimia 27 wakipoteza maisha pamoja na mali zao.

Amesema Wizara hiyo kwa kipindi cha miaka tisa imefanya utafiti kubaini maeneo mbalimbali ya uvuvi ambayo wavuvi wa Zanzibar hupendelea kwenda kuvua ambapo samaki hupatikana kwa wingi.

“Utafiti huo tumeshirikiana na Taasisi ya WorldFish kupitia Taasisi ya Utafiti wa Mazao ya Baharini (ZAFIRI) ili kubaini maeneo hayo na kuwalinda wavuvi,” amesema Cap. Hamad.

Amefafanua kuwa Wizara imechagua boti 100 ambazo zimefungwa vifaa maalumu vya kutoa ishara kupitia mfumo maalumu kwa mamlaka husika hatua inayolenga kurahisisha ufuatiliaji na uokozi wa wavuvi wanapokuwa baharini.

Cap. Hamad, mfumo huo ni muhimu kutokana na wavuvi kwenda kuvua katika maeneo ya mbali ambayo wakati mwingine huwa vigumu kufikika wanapopata majanga.

Amesema taarifa zitakazopatikana kupitia mfumo huo zitagawanywa kwa vyombo vya ulinzi na usalama, ikiwemo KMKM, ZMA na Shirika la Bandari, ili kusaidia kufahamu maeneo ambayo wavuvi huenda kuvua katika vipindi vya upepo mkali.

Ameeleza kuwa mfumo huo tayari umeanza kutekelezwa katika baadhi ya maeneo ya Unguja na Pemba ambapo Wizara ikiendelea na mpango wa kuufikisha nchi nzima ili kupata taarifa kamili kuhusu wavuvi.

Amesema mfumo huo utasaidia kuonesha maeneo ambayo wavuvi huenda kuvua, kutoa taarifa zitakazotumika na taasisi za uokozi na watoa huduma pamoja na kusaidia kuwapatia wavuvi huduma na stahiki kulingana na

"Uchumi wa Buluu Kwa Maendeleo Endelevu"
09/08/2026

"Uchumi wa Buluu Kwa Maendeleo Endelevu"

Naibu Waziri wa Uchumi wa Buluu na Uvuvi Mhe. Mboja Ramadhan Mshenga  akiwa katika ziara ya kutembelea Vituo vidogo vya ...
08/08/2026

Naibu Waziri wa Uchumi wa Buluu na Uvuvi Mhe. Mboja Ramadhan Mshenga akiwa katika ziara ya kutembelea Vituo vidogo vya Utafiti wa Mawimbi na Mikondo ya Bahari, na Upepo.
katika ziara hio Naibu Waziri alikabidhi Shilingi Milioni 6 kwa Kamati ya Uvuvi ya Kendwa, ikiwa ni mchango wa Taasisi ya (ZAFIRI) na (SIO) kuwezesha ujenzi wa Ofisi ya Kamati ya Uvuvi ya Kendwa.

02/08/2026

SAFARI YA MVUVI NA TASFAM

Zanzibar imebahatika kuwa mwenyeji wa mkutano wa 13 wa Kamati ya Kisayansi ya Uvuvi ya Kusini Magharibi mwa Bahari ya Hi...
28/07/2026

Zanzibar imebahatika kuwa mwenyeji wa mkutano wa 13 wa Kamati ya Kisayansi ya Uvuvi ya Kusini Magharibi mwa Bahari ya Hindi SWIOFC unaojadili uvuvi na usimamizi sahihi wa rasilimali za bahari ambao umehudhuriwa na nchi wanachama 12 wa ukanda huo unaofanyika katika hoteli ya Marumaru Zanzibar.

Mkutano huo wa siku tano pamoja na mambo mengine utajadili udhibiti wa rasilimali za bahari, ushirikiano wa kikanda, usalama wa chakula cha baharini na maisha ya raia pamoja na changamoto kubwa zinazowakabili.

Akifungua mkutano huo Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Uchumi wa Buluu na Uvuvi Zanzibar Zahor Kassim El Kharousy amesema nchi wanachama wa SWIOFC kwa pamoja wanazingatia uhifadhi wa bahari na rasilimali zake ili ziwe endelevu na kwa siku hizo tano wataweka maazimio yatakayotilia nguvu uongozi imara wa bahari katika ukanda huo kwa faida ya vizazi vya sasa na vijavyo.

Amesema kwa ujumla rasilimali za bahari hazina udhibiti wa moja kwa moja kwa nchi husika lakini zikiwepo nguvu za pamoja kwa nchi za ukanda huo za kupambana na uvuvi haramu na usimamizi na uendelezaji sahihi wa rasilimali za baharini itatimiza malengo ya kimataifa ya kuifanya bahari kuwa chanzo kikuu cha kukuza kipato cha wananchi.

Mwenyekiti wa sasa wa Kamati ya kisayansi ya SWIOFC Sekiwe Mbande amesema Jumuiya hiyo inatoa fursa na kuzishauri nchi wanachama kufanya kazi kwa pamoja kitaalamu hasa kwa kufuata vigezo vya nchi k**a Msumbiji ambayo imepiga hatua kubwa katika sekta ya uvuvi.

Katibu wa SWIOFC Jon Lansley amesema mikutano ya Jumuiya hiyo kwa wanachama wake wanapata mbinu nzuri za kuwainua wananchi wake na kuwawezesha ili wawe na matumizi mazuri ya bahari na rasilimali zake kulingana na matokeo ya tafiti zinazofanyika.

Aidha wamesisitiza kuwepo kwa nguvu kubwa ya kitaalamu kwa tafiti zinazofanyika kwa lengo la kuwa na uhifadhi mzuri wa bahari na rasilimali zake kuwa endelevu, ubunifu na ushirikiano wa kikanda ambao utaleta mafanikio na kujenga misingi imara ya muda mrefu.

Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar, imesema kuandaa mijadala na makongamano kuhusu sekta ya mafuta, gesi na nishati safi ...
26/07/2026

Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar, imesema kuandaa mijadala na makongamano kuhusu sekta ya mafuta, gesi na nishati safi ni mkakati muhimu wa kuitangaza Zanzibar kimataifa na kuvutia wawekezaji watakaosaidia kukuza uchumi wa taifa kupitia rasilimali hizo.

Katibu Mkuu wa Wizara ya Uchumi wa Bluu na Uvuvi, Kepteni Hamad Bakar Hamad, alitoa kauli hiyo wakati akifungua Kongamano la Pili la Mafuta na Gesi Asilia kwa Nchi za Afrika lililofanyika katika Ukumbi wa New Amani Complex, Zanzibar.

Alisema kongamano hilo limekusanya pamoja taasisi za elimu, wadau wa sekta ya mafuta na gesi pamoja na wawekezaji kutoka mataifa mbalimbali ya Afrika kwa lengo la kujadili namna bora ya kutumia rasilimali za mafuta na gesi zilizopo barani humo ili ziwe chachu ya maendeleo ya waafrika.

Aidha alisema Afrika imeonekana ina rasilimali ya mafuta na gesi lakini haijawanufaisha na bado inaendelea kuagiza kutoka nje rasilimali hii hivyo kongamano hilo limeangalia namna gani wanaweza kuzikabili changamoto hizo na kuvutia wawekezaji.

Alibainisha kuwa Zanzibar imepiga hatua kubwa katika maandalizi ya kuingia rasmi kwenye sekta ya mafuta na gesi chini ya serikali ya awamu ya nane, ambapo tayari vitalu 10 vya utafutaji wa mafuta na gesi, vikiwemo vya baharini na nchi kavu, vimetangazwa kwa ajili ya kuvutia kampuni za kimataifa kuwekeza.

Kepten Hamad alisema serikali inaendelea na tafiti za kina zitakazoweka msingi wa kubaini maeneo yenye uwezekano mkubwa wa kuchimbwa visima vya utafiti, hatua ambayo inaongeza matumaini ya kugunduliwa kwa mafuta na gesi asilia nchini katika siku zijazo.

“Tuna matumaini kuwa baada ya kongamano hili tutapata wawekezaji wengi zaidi watakaovutiwa kuwekeza katika sekta ya mafuta na gesi Zanzibar,” alisema.

Address

ZURA BUILDING, MAISARA
Zanzibar City

Website

Alerts

Be the first to know and let us send you an email when Wizara ya Uchumi wa Buluu na Uvuvi Zanzibar posts news and promotions. Your email address will not be used for any other purpose, and you can unsubscribe at any time.

Shortcuts

Share