Mkoa Mjini Magharibi

Mkoa Mjini Magharibi Ukurasa unaokuletea habari na matukio mbali mbali ya Mkoa Mjini Magharibi

Mkuu wa Mkoa Mjini Magharibi Mhe. Idrissa Kitwana Mustafa amefunga mkutano mkuu wa mwaka wa Jumuia ya Wakimbiza Mwenge w...
04/07/2023

Mkuu wa Mkoa Mjini Magharibi Mhe. Idrissa Kitwana Mustafa amefunga mkutano mkuu wa mwaka wa Jumuia ya Wakimbiza Mwenge wa Uhuru Kitaifa (TAUTA) uliofanyika ukumbi wa Chuo cha Mafunzo Kilamani.

πŸ“OISI YA MKOA MJINI MAGHARIBI

πŸ—“03-07-2023












Mkoa mjini Magharibi Alfajir ya Leo Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dr.  Hussein Ali Mwinyi amerej...
02/07/2023

Mkoa mjini Magharibi

Alfajir ya Leo Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dr. Hussein Ali Mwinyi amerejea nchini akitokea China πŸ‡¨πŸ‡³
AAKIA ✈️

Rais wa Zanzibar Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe. Dkt. Hussein Ali Mwinyi amezindua rasmi mradi wa ujenzi wa maduk...
18/02/2023

Rais wa Zanzibar Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe. Dkt. Hussein Ali Mwinyi amezindua rasmi mradi wa ujenzi wa maduka 452 wa Darajani Souk. Akizungumza na hadhara iliyohudhuria hafla hiyo Dkt. Mwinyi amepongeza mashirikiano yaliyooneshwa na Serikali ya Mkoa Mjini Magharibi na Chama cha Mapinduzi katika katika kipindi chote cha utekelezaji wa mradi huo.
Aidha amewataka watakaosimamia mradi huo pamoja wafanyabiashara watakaokodishwa milango kuhakikisha wanaitunza na kufanya matengenezo pale panapotokea hitilafu badala ya kuacha kuendelea kuharibika.

Rais Mwinyi kuzindua Darajan souk Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe. Dkt. Hussein Ali Mwinyi ana...
16/02/2023

Rais Mwinyi kuzindua Darajan souk
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe. Dkt. Hussein Ali Mwinyi anatarajiwa kuzindua rasmi kituo cha biashara cha Darajani Souk siku ya jumaamosi ya tarehe 18/02/2023.

Taarifa rasmi juu ya uzinduzi wa kituo hicho imetolewa na Mkuu wa Mkoa Mjini Magharibi Mhe. Idrissa Kitwana Mustafa alipokuwa akizungumza na vyombo vya habari kuhusiana na uzinduzi wa mradi huo hapo Darajani.
Amesema ujenzi wa kituo hicho cha kisasa chenye maduka 452, bustani na eneo la kuegesha magari tayari umeshakamilika na matayarisho mbali mbali ya uzinduzi wake yanaendelea vizuri.

Mkuu wa Mkoa amewaomba wananchi wa Mkoa Mjini Magharibi na Mikoa mengine jirani kuhudhuria kwa wingi kwenye uzinduzi wa mradi huo ambao amesema mbali na kubadilisha mandhari ya eneo la Darajani vile vile utatoa fursa nyingi zaidi kwa wafanyabiashara kuendesha shughuli zao.

Amesema kwamba tayari mpango mzuri wa kuendesha biashara umeshapangwa ili kurahisisha upatikanaji wa bidhaa mbali mbali zitakazouzwa katika kituo hicho yakiwemo mavazi, vifaa vya kiektroniki na huduma nyenginezo.

Mhe. Idrissa amewahakikishia wafanyabishara waliokuwepo kabla ya ujenzi huo kuwa watarudi kuendesha biashara zao mahala hapo na nafasi zitakazobaki watapewa wafanyabiashara wengine waliyoomba kukodi milango ya biashara kwenye eneo hilo.
Aidha Mkuu wa Mkoa amemshukuru Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe. Dkt. Hussein Ali Mwinyi kwa maelekezo yake yaliyopelekea kufanikisha ujenzi wa mradi huo katika eneo hilo la Darajani.

Ujenzi wa Darajani Souk uliogharimu kiasi ya shilingi bilioni nane ulianza mwezi februari mwaka 2022 huku awamu ya pili ya mradi huo ikitarajiwa kuanza hivi karibuni na kukamilika mwishoni mwa mwaka 2023.

USAID yafadhili mradi wa kuwawezesha Vijana.Serikali ya Mkoa Mjini Magharibi imeeleza kuwa itatoa  mashirikiano ya kutos...
01/02/2023

USAID yafadhili mradi wa kuwawezesha Vijana.
Serikali ya Mkoa Mjini Magharibi imeeleza kuwa itatoa mashirikiano ya kutosha ili kufanikisha mradi wa miaka minne wa kuwawezesha vijana kujitegemea unaofadhiliwa na Shirika la Misaada la Marekani USAID.
Hayo yamesemwa na Katibu Tawala Mkoa Mjini Magharibi Moh'd Ali Abdalla alipokuwa akifungua kikao cha kutoa elimu kwa maofisa wa afya, ustawi wa jamii, vijana na mipango juu ya namna mradi huo utakavyotekelezwa katika Mkoa huo.
Akizungumza na maofisa hao pamoja na wasimamizi wa mradi huo, Katibu Tawala amesema Mkoa wake umefarijika sana kuja kwa mradi huo kwa vile una malengo mazuri ya kuwaendeleza vijana kielimu, kiujuzi pamoja na kuwapa stadi za maisha ambazo zitawawezesha kujitegemea na kuwa na maisha bora hapo baadae.
Aidha ameeleza kuwa mradi huo unakwenda sambamba na mpango wa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar ya kuwainua vijana katika nyanja mbali mbali, hivyo Mkoa pamoja na Wilaya zake zitahakikisha malengo ya mradi huo yanatimia.
Akiwasilisha maelezo juu ya utekelezaji ya mradi huo unaofahamika k**a USAID - Kijana Nahodha, Meneja wa Mradi Upendo Laizer amesema mradi huo utahusisha vijana kuanzia umri wa miaka 15 hadi 24 wakiwemo waliyoacha Skuli,waliokuwa hawajaajiriwa na wale waliopata ujauzito katika umri mdogo ili kuwapa mafunzo mbali mbali yatakayoweza kuwaandaa waweze kujitegemea.
Amewataka maofisa wa Mkoa na Wilaya watakaohusika na mradi huo kushirikiana katika kuwatambua vijana watakaopatiwa mafunzo hayo pamoja na maeneo na makundi watakayotoka.
Amesema kuwa kiasi cha dola za Marekani milioni 10.6 zitatukumika kwa mradi huo wa miaka minne kwa Mikoa mitano ya Zanzibar na Mikoa miwili kwa Tanzania Bara utakaosimamiwa na T-MARC Tanzania.
Kwa upande wao maofisa walioshiriki kikao hicho wametoa michango mbali mbali itakayopelekea kufanikisha mradi huo pamoja na kuahidi kutoa mashirikiano yao pale mradi utakapoanza kutekelezwa.

Akitoa salamu za wananchi katika shughuli hiyo, Mkuu wa Mkoa Mjini Magharibi Idrissa Kitwana Mustafa  amasema Mkoa utaen...
10/01/2023

Akitoa salamu za wananchi katika shughuli hiyo, Mkuu wa Mkoa Mjini Magharibi Idrissa Kitwana Mustafa amasema Mkoa utaendelea kushirikiana na Wizara ya Habari Vijana Utamaduni na michezo ili kufanikisha miradi yote iliyokusudiwa kutekelezwa ndani ya Mkoa wake katika sekta ya michezo.
Naye Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Fedha na Mipango Dkt. Saada Mkuya amesema mbali na miradi ya fedha za UVIKO, ipo miradi kadhaa inayotekelezwa kwa fedha za Serikali ukiwemo ujenzi wa uwanja huo wa michezo uliogharimu shilingi bilioni 1.1
Viongozi mbali waliopata fursa ya kuzungumza wamempongeza Rais wa Zanzibar kwa utekelezaji wake wa miradi ya maendeleo k**a inavyoelekeza ilani ya Chama cha Mapinduzi ya 2025
Uwanja huo utakuwa na viwanja vinne vya mpira wa miguu pamoja na michezo mengine, jengo la vyumba vya wachezaji kubadilishia nguo, vyoo na jukwaa la watazamaji unatekelezwa na Mfuko wa Hifadhi ya Jamii Zanzibar (ZSSF).
Serikali kujenga viwanja vya michezo kila Wilaya na Mkoa.

Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Mhe. Hemed Suleiman Abdulla ameipongeza Wizara ya Biashara na maendeleo ya viwanda kw...
10/01/2023

Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Mhe. Hemed Suleiman Abdulla ameipongeza Wizara ya Biashara na maendeleo ya viwanda kwa kuboresha Maonesho ya Tisa Biashara ya Biashara yanayoendelea katika viwanja vya Maisara Mjini Zanzibar.
Mhe. Hemed ameyasema hayo alipotembelea Maonesho hayo kujionea shughuli zinazofanywa na washiriki mbali mbali wa monesho hayo.
Amesema maonesho hayo ni ya aina yake hasa kuona washiriki wa Zanzibar na nchi mbali mbali ambapo kuongezeka kwa ushiriki wao kuonesha kuwepo kwa maandalizi mazuri yanayosimamiwa na Wizara ya Biashara na maendeleo ya viwanda.
Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar amesema Maonesho hayo yanawapa fursa wananchi kupata huduma mbali mbali katika eneo moja tu ambazo ilikuwa wazifate masafa marefu.
Aidha Mhe. Hemed amewataka Wananchi kujitokeza na kutembelea Taasisi za Serikali zinazotoa huduma pamoja na kupata maelekezo kuhusiana na huduma wanazozitoa.
Aidha Mhe. Hemed amefurahishwa kuwepo kwa kituo jumuishi (One Stop Center) katika Maonesho hayo ambacho kinajumuisha Taasisi mbali mbali zilizoshiriki na kueleza kuwa uwepo wa Kituo hicho kunaonesha ushirikiano uliopo baina ya Taasisi mbali mbali.
Nae waziri wa Biashara na Maendeleo ya Viwanda Zanzibar Mhe. Omar Said Shaban amemshukuru Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar kwa kutembelea maonesho hayo jambo ambalo linawatia hamasa Wananchi kujitokeza kwa wingi kutembelea maonesho hayo.
Aidha Mhe. Shaban amemuhakikishia Mhe. Hemed kuwa Wizara itaendelea kuchukua maelekezo watakayopatiwa na Viongozi mbali mbali wanaokuja kutembelea kwa lengo la kuboresha maeonesho hayo.
Akitembelea maonesho hayo Mhe. Hemed amezishauri Taasisi zinazotoa huduma kwa wananchi kuboresha huduma zao hasa kutumia muda mfupi kuwapatia huduma wanazostahiki.

Wananchi wa Mkoa Mjini Magharibi wamemshukuru Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe.Dkt.Hussein Ali ...
06/01/2023

Wananchi wa Mkoa Mjini Magharibi wamemshukuru Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe.Dkt.Hussein Ali Mwinyi kwa kuelekeza kiasi kikubwa cha fedha kwa ajili ya ujenzi wa majengo ya Skuli ndani ya Mkoa huo.
Shukurani hizo zimetolewa na Mkuu wa Mkoa Mjini Magharibi Idrissa Kitwana Mustafa alipokuwa akitoa salamu za wananchi wa Mkoa huo katika uzinduzi wa Skuli ya msingi Kwa Binti Amrani.
Amesema mafanikio hayo yaliyopatikana katika ujenzi wa miradi mikubwa katika sekta ya elimu yametokana na maono, hekima na busara zake katika kuiongoza Zanzibar.
Mkuu wa Mkoa amesema ujenzi wa Skuli hiyo na nyengine zilizojengwa katika Mkoa wake zinakwenda kuondosha changamoto ya msongamano wa wanafunzi katika madarasa.
Amewataka walimu waliokabidhiwa Skuli hiyo kuhakikisha wanaitunza ili iweze kubaki katika hali nzuri na kudumu kwa miaka mingi ijayo.
Katika salamu hizo pia Mkuu wa Mkoa amesema kuwa mashirikiano makubwa yaliopo baina ya Serikali na Cha cha Mapinduzi yamepelekea kufanikisha utekelezaji wa ilani ya CCM kwa kiasi kikubwa.
Akizungumza na wananchi, Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe. Dkt. Hussein Ali Mwinyi amewapongeza viongozi wa Mkoa Mjini Magharibi na Wilaya zake kwa kufatilia kwa karibu utekelezaji wa miradi ya maendeleo kwenye Mkoa huo.

Mkuu wa Mkoa wa Mjini Magharibi Mh. Idrissa Kitwana Mustafa amesema ipo haja kwa Watumishi kupatiwa Mafunzo ya Ulinzi wa...
06/12/2022

Mkuu wa Mkoa wa Mjini Magharibi Mh. Idrissa Kitwana Mustafa amesema ipo haja kwa Watumishi kupatiwa Mafunzo ya Ulinzi wa Mifumo ya Kompyuta na kuzuwia wizi wa Mitandao ili waweze kulinda taarifa mbalimbali zilizopo nchini.

Alitoa kauli hiyo wakati akifungua Mafunzo ya Ulinzi wa Mifumo ya Kompyuta na kuzuwia wizi wa Mitandao (Cyber Security) yanayofanyika katika Ukumbi wa Mkutano wa Dkt. Idrissa Muslim Hija katika Taasisi ya Sayansi na Teknolojia ya Karume (KIST) Mbweni Zanzibar.

Alisema kumekuwa na ongezeko kubwa la uwepo wa udukuzi wa tarifa za mtu mmoja mmoja na hata baadhi ya Taasisi jambo ambalo linaweza kusababisha matatizo mengi katika jamii ikiwemo uvunjivu wa Amani.

Alisema endapo Watumishi hasa Wataalamu wa Kompyuta watapata uelewa wa hali ya juu kuhusu mbinu zinazotumiwa na Wahalifu wa Mitandao wataweza kuisaidia Nchi kutunza na kudumisha Amani iliyopo.

Aidha Mkuu wa Mkoa huyo amewasisitiza wale wote watakaopata Mafunzo hayo muhimu, waitumie elimu hiyo katika kuleta maendeleo nchini na kuisaidia jamii kuepuka udhalilishaji unaofanywa Mitandaoni.

Akizungumza kwa niaba ya Mkuu wa Taasisi ya Karume, Kaimu Mkuu wa Idara ya Mipango Utawala na Rasilimali Watu Dkt.Iddy khatib Iddy amesema miongoni mwa malengo ya Taasisi ya Karume ni kutoa taalum ya mambo yanayoendana na wakati uliopo ikwemo taaluma ya ulinzi wa Mifumo na Komputa.

Alisema kuwa, Mafunzo hayo yatawawezesha Watu binafsi na Taasisi mbalimbali hasa za Serikali, kupata ulinzi wa taarifa zao.

Aidha alitumia fursa hiyo kumuomba Mkuu wa Mkoa wa Mjini Magharibi kuendelea kutoa ushirikiano wa karibu na Taasisi ya Karume hasa katika kufanikisha suala la kutumia Mkonga wa Taifa.

Mkoa Mjini Magharibi Watangaza Operesheni Maalum dhidi ya Panya RoadKamati ya Ulinzi na Usalama ya Mkoa Mjini Magharibi ...
20/10/2022

Mkoa Mjini Magharibi Watangaza Operesheni Maalum dhidi ya Panya Road
Kamati ya Ulinzi na Usalama ya Mkoa Mjini Magharibi imeanzisha operesheni maalum katika Shehia zote 121 za Mkoa huo ya kuwak**ata watu wanaofanya vitendo vya uporaji, wizi na uhalifu.
Akitoa taarifa kuhusu operesheni hiyo, Mkuu wa Mkoa Mjini Magharibi Idrissa Kitwana Mustafa amesema operesheni hiyo itafanywa na vikosi vyote vya ulinzi ili kuwatia mikononi wale wote wanaojihusisha na matendo hayo pamoja na kuwachukulia hatua za kisheria.
Mkuu wa Mkoa amesema Kamati ya Ulinzi na Usalama ya Mkoa ina dhima ya kusimamia suala zima la ulinzi ndani ya Mkoa huo hivyo ameonya kuwa haitachelea kumchukuli hatua mtu yoyote yule atakaebainika kujihusisha na uporaji, wizi na uhalifu wakati operesheni hiyo ikiendelea.
Ametanabahisha kuwa Serikali ina vyanzo vya kutosha kuweza kupata taarifa za vijana wanaofanya vitendo hivyo na kuwataka wazazi na walezi kuwaelimisha vijana wao kutojiingiza kwenye vitendo hivyo badala ya kuwalinda.
Aidha Idrissa amewataka pia Masheha na jamii kutoa mashirikiano yao katika operesheni hiyo kwa kutoa taarifa za watu wanaofanya matendo hayo na kusema kuwa vyombo vya ulinzi itawahifadhi wale wote watakaotoa taarifa hizo.
Kwa upande mwengine Mkuu wa Mkoa amewaasa vijana kutojiingiza kwenye vitendo vya aina hiyo kwani havina tija hata kidogo kwao, familia zao na taifa kwa ujumla.
Hata hivyo amewahakikishia wananchi kuwa Serikali ya Mkoa itaendelea kusimamia suala zima la amani na utulivu ndani ya Mkoa huo ili waweze kuendelee na shughuli zao za maisha k**a kawaida.

Address

Vuga Street
Zanzibar City

Alerts

Be the first to know and let us send you an email when Mkoa Mjini Magharibi posts news and promotions. Your email address will not be used for any other purpose, and you can unsubscribe at any time.

Contact The Organization

Send a message to Mkoa Mjini Magharibi:

Share