Wizara ya Maji, Nishati na Madini Zanzibar - Mowem

Wizara ya Maji, Nishati na Madini Zanzibar - Mowem Ministry of Water, Energy and Minerals is responsible for Managing and Developing Water, Energy and Minerals issues in Zanzibar.

12/06/2026
10/06/2026
MKURUGENZI MIPANGO, SERA NA UTAFITI AFAFANUA MAJUKUMU YA WIZARA NA FURSA ZA KOZI MPYA YA CHEMICAL PROCESSING AND ENGINEE...
10/06/2026

MKURUGENZI MIPANGO, SERA NA UTAFITI AFAFANUA MAJUKUMU YA WIZARA NA FURSA ZA KOZI MPYA YA CHEMICAL PROCESSING AND ENGINEERING

Katika juhudi za kuimarisha uelewa wa wanafunzi kuhusu mchango wa sekta za maji, nishati na madini katika maendeleo ya taifa, Mkurugenzi wa Mipango, Sera na Utafiti wa Wizara ya Maji, Nishati na Madini Zanzibar ndg Mohammed Hassan Khamis amewasilisha mada maalum iliyoeleza majukumu ya Wizara pamoja na mipango mbalimbali inayotekelezwa katika sekta hizo muhimu.

Akiwasilisha mada hiyo katika Chuo cha IT Madrasat Bweleo, Mkurugenzi huyo alifafanua nafasi ya Wizara katika kusimamia upatikanaji wa huduma bora za maji safi na salama, kuimarisha uzalishaji na usambazaji wa nishati, pamoja na kusimamia rasilimali za madini kwa manufaa ya wananchi na uchumi wa Zanzibar.

Aidha, alieleza mipango ya Wizara inayolenga kuendeleza sekta hizo kupitia matumizi ya teknolojia za kisasa, utafiti na ubunifu, huku akisisitiza umuhimu wa kuwaandaa wataalamu wenye ujuzi watakaoweza kukabiliana na changamoto na mahitaji ya sasa na ya baadaye.

Katika wasilisho lake, Mkurugenzi huyo pia alizungumzia matarajio ya faida zitakazopatikana kupitia kozi mpya ya Chemical Processing and Engineering inayotarajiwa kufundishwa katika Chuo cha IT Madrasat Bweleo. Alieleza kuwa kozi hiyo itatoa fursa kwa wanafunzi kupata maarifa na ujuzi wa kitaalamu katika uchakataji wa malighafi na rasilimali mbalimbali, jambo litakalosaidia kuongeza thamani ya rasilimali za ndani na kukuza maendeleo ya viwanda.

Aliongeza kuwa kuanzishwa kwa kozi hiyo kutachangia kuandaa wataalamu watakaoweza kushiriki kikamilifu katika maendeleo ya sekta za maji, nishati na madini, sambamba na kuongeza ajira na fursa za kiuchumi kwa vijana.

Akihitimisha wasilisho lake, Mkurugenzi huyo alitoa wito kwa wanafunzi kutumia vyema fursa ya masomo hayo mapya kwa kujifunza kwa bidii na kuzingatia ubunifu, ili waweze kuwa sehemu ya wataalamu watakaosukuma mbele maendeleo ya Zanzibar na Taifa kwa ujumla

Wizara ya Maji, Nishati na Madini kupitia Idara ya Nishati na madini inaendelea na juhudi za Serikali za kuhamasisha mat...
09/06/2026

Wizara ya Maji, Nishati na Madini kupitia Idara ya Nishati na madini inaendelea na juhudi za Serikali za kuhamasisha matumizi ya nishati safi ya kupikia ambapo imefanya ziara maalum ya utoaji elimu katika Skuli tofauti Pemba ikiwemo skuli ya Piki, Ole, Idrissa Abdulwakil, Wete sekondari, Kiwani na skuli ya Ufundi Kengeja.

Katika ziara hiyo, Wataalamu wa Wizara walielezea umuhimu wa kutumia nishati safi ya kupikia katika kulinda afya za wananchi, kuhifadhi mazingira na kupunguza matumizi ya nishati zinazochangia uharibifu wa misitu.

Watalamu walieleza kuwa elimu ya nishati safi inapaswa kuanza kutolewa kwa watoto tangu wakiwa shuleni ili kuwajengea uelewa na utamaduni wa kutumia nishati salama na rafiki kwa mazingira. Ambapo ilisistizwa kuwa matumizi ya nishati safi yana mchango mkubwa katika kuboresha afya za familia kwa kupunguza athari za moshi unaotokana na matumizi ya kuni na mkaa.

Aidha kwa upande wa Wanafunzi wa Skuli hizo, walipata fursa ya kujifunza aina mbalimbali za nishati safi za kupikia pamoja na faida zake, huku wakihimizwa kuwa mabalozi wa kuelimisha jamii zao kuhusu umuhimu wa matumizi ya nishati hizo.

Ziara hiyo ni sehemu ya kampeni inayoendelea ya Wizara kupitia Idara ya Nishati na Madini ya kuhamasisha matumizi ya nishati safi ya kupikia katika jamii, Taasisi za elimu na wadau mbli mbali mbalimbali nchini kwa lengo la kufikia maendeleo endelevu na kulinda mazingira kwa vizazi vya sasa na vijavyo.

Naibu Waziri wa Maji, Nishati na Madini Zanzibar Mhe. Seif Kombo Pandu amesema,Serikali ya Mapinduzi Zanzibar inalenga k...
02/06/2026

Naibu Waziri wa Maji, Nishati na Madini Zanzibar Mhe. Seif Kombo Pandu amesema,Serikali ya Mapinduzi Zanzibar inalenga kuleta mabadiliko makubwa katika kukuza sekta ya nishati kwa wananchi wake.
Akizungumza katika uzinduzi wa ushirikiano kati ya shirika la umeme Zanzibar (zeco)na kampuni ya Airtel Money katika hutba iliyosomwa kwa niaba yake na Naibu Wairi wa Wizara hiyo Mhe. Seif Kombo Pandu amesema, lengo la serikali ni kuona wananchi wake wanapata huduma nzuri ya nishati ya umeme bila usumbufu wowote.
Aidha amefafanua kuwa kutokana na sera ya nishsti Zanzibar ya mwaka 2025-2040 ina mpango wa kuimarisha usalama wa nishati na kupunguza gharama za uzalishaji.
“chini ya sera ya nishati ya Zanzibar 2025 na mpango wa muda wa miaka 15 wa umeme (2025-2040),serikali inalenga kuimarisha usalama wa nishati,kupunguza gharama za uzalishaji,na kuongeza uwezo wa uzalishaji wa ndani” amesema.
Akifafanua Kwa niaba ya Meneja Mkuu wa Zeco, Meneja Mipango na biashara Aisha Omar Makame amesema ushirikiano huo ni hatua muhimu katika kuimarisha huduma ya upatikanaji wa umeme umbao naweza kuibadilisha Zanzibar kwa kuweza kufikikia maendeleo kiurahisi.
Nae Mkurugenzi wa airtel money Tanzaniaa Andrew Rugamba ameeleza kuwa kampuni ya airtel moneya itahakikisha wananchi wa Zanzibar wanapata huduma hiyo ya umeme bila usumbufu wowote.
Ushirikiano huwo wa kimaendeleo kati ya Zeco na Airtel maney utasaidia wananchi wa Zanzibar kupata huduma kwa kununua umeme kwa njia ya simu (TUKUZA) Kupitia simu zao za mkononi.

Address

Maisara
Zanzibar City
255

Opening Hours

Monday 07:30 - 15:30
Tuesday 07:30 - 15:30
Wednesday 07:30 - 15:30
Thursday 07:30 - 15:30
Friday 07:30 - 15:30

Website

Alerts

Be the first to know and let us send you an email when Wizara ya Maji, Nishati na Madini Zanzibar - Mowem posts news and promotions. Your email address will not be used for any other purpose, and you can unsubscribe at any time.

Contact The Organization

Send a message to Wizara ya Maji, Nishati na Madini Zanzibar - Mowem:

Share