Mamlaka ya Maji Zanzibar - ZAWA

Mamlaka ya Maji Zanzibar - ZAWA Mamlaka ya Maji ya Zanzibar (ZAWA) ni taasisi ya Serikali ilionzishwa chini ya Sheria. Na. 4 ya 2006

Waziri wa Maji, Nishati na Madini Zanzibar Mhe. Shaibu Hassan Kaduara amefungua mradi wa Maji wa Kisima kinachotumia ume...
19/03/2025

Waziri wa Maji, Nishati na Madini Zanzibar Mhe. Shaibu Hassan Kaduara amefungua mradi wa Maji wa Kisima kinachotumia umeme wa jua Weni Wete Pemba.

Mradi huo uliojengwa na kampuni ya Oikos East Africa unazalisha kilowatt 41.4 ambapo umefadhiliwa na Umoja wa Ulaya na kugharimu kiasi cha shilingi za kitanzania milioni 250 kwa Skimu ya Weni na Kizimbani Wete Pemba.

Kitengo cha Uhusiano – ZAWA
19 Machi 2025
Weni Wete Pemba.

19/03/2025
Mkurugenzi Mkuu Mamlaka ya Maji  Zanzibar – ZAWA Mhandisi Dkt. Salha Mohammed Kassim ameshiriki katika kikao cha tatu ch...
17/03/2025

Mkurugenzi Mkuu Mamlaka ya Maji Zanzibar – ZAWA Mhandisi Dkt. Salha Mohammed Kassim ameshiriki katika kikao cha tatu cha kamati ya viongozi Pemba kinachojadili masuala mbali mbali ya miradi ya huduma za kijamii Zanzibar.

Kikao hicho kilichohudhuriwa na viongozi mbali mbali wa taasisi za Serikali pamoja zisizo za Serikali kina lengo la kujadili utekelezaji wa miradi ya maendeleo Pemba inayosimamiwa na taasisi ya Green and Smart Cities Sasa! Programme.

Aidha, wadau wengine waliohudhuria katika kikao hicho ni kampuni ya Oikos ambao ni watekelezaji wa Mradi wa umeme wa nishati ya jua katika kisima cha Weni na Kizimbani Wete Pemba Pamoja na Kfw ambao ni watekelezaji wa Mradi wa Usalama wa Maji unaotarajiwa kutekelezwa Pemba.

Kitengo cha Uhusiano – ZAWA
Tibirinzi Chake Chake Pemba
17 Machi 2025

Uongozi wa Mamlaka ya Maji Zanzibar – ZAWA pamoja na Rand Water umekutana na Wafanyakazi wa ZAWA ofisi ya Tawi la Pemba....
14/03/2025

Uongozi wa Mamlaka ya Maji Zanzibar – ZAWA pamoja na Rand Water umekutana na Wafanyakazi wa ZAWA ofisi ya Tawi la Pemba.

Katika kikao hicho kilichofanyika katika ukumbi wa Baraza la Manispaa Chake Chake Pemba Wafanyakazi hao wamesisitizwa kuweka mashirikiano na Kampuni ya Rand Water kutoka Afrika ya Kusini ambao ndio wanaotarajiwa kuiongoza ZAWA.

Mkutano huo umefanyika ikiwa ni miongoni mwa mchakato wa hatua za makabidhiano ya ZAWA kwa kampuni ya Rand Water.

Kitengo cha Uhusiano – ZAWA
Chake Chake Pemba
14 Machi 2025

Mamlaka ya Maji Zanzibar – ZAWA pamoja na kampuni ya Rand Water kutoka Afrika Kusini  zimeendelea na ziara ya kutembelea...
14/03/2025

Mamlaka ya Maji Zanzibar – ZAWA pamoja na kampuni ya Rand Water kutoka Afrika Kusini zimeendelea na ziara ya kutembelea miundombinu ya Maji Mkoa wa Kaskazini Pemba.

Ziara hiyo ni miongoni mwa hatua za mchakato wa makabidhiano ya ZAWA kwa kampundi ya Rand Water ambao wanatarajiwa kuiendesha Mamlaka ya Maji Zanzibar – ZAWA.

Ziara hiyo imetembelea Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Kaskazini Pemba, visima vya maji pamoja na matangi katika eneo la Kilindini, Makangale na Weni Pemba.

Kitengo cha Uhusiano – ZAWA
Mkoa wa Kaskazini Pemba
14 Machi 2025

Uongozi wa ZAWA pamoja na Kampuni ya Rand Water umefanya ziara ya kutembelea Miundombinu ya Maji ya ZAWA Mkoa wa Kusini ...
12/03/2025

Uongozi wa ZAWA pamoja na Kampuni ya Rand Water umefanya ziara ya kutembelea Miundombinu ya Maji ya ZAWA Mkoa wa Kusini Pemba.

Ziara hiyo ni hatua za mchakato wa Makabidhiano yanayoendelea ya ZAWA kwa kampuni ya Rand Water kutoka Afrika Kusini ambao ndio wanatarajiwa kuiendesha Mamlaka ya Maji Zanzibar – ZAWA.

Mwanzoni ziara hiyo ilianza kwa ZAWA na kampuni ya Rand Water kufika kujitambulisha Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Kusini Pemba na kuomba mashirikiano ya utendaji kazi.

Maeneo yaliyotembelewa katika ziara hiyo ni Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Kusini Pemba, Tangi la Maji Chanjaani, Pujini na Kiwani. Kisima cha Maji Kengeja na Mjimbini.

Kitengo cha Uhusiano – ZAWA
Mkoa wa Kusini Pemba
12 Machi 2025

Mkurugenzi Mkuu Mamlaka ya Maji Zanzibar – ZAWA Mhandisi Dkt. Salha Mohammed Kassim amekagua kazi inayoendelea ya uwekaj...
08/02/2025

Mkurugenzi Mkuu Mamlaka ya Maji Zanzibar – ZAWA Mhandisi Dkt. Salha Mohammed Kassim amekagua kazi inayoendelea ya uwekaji wa umeme wa nishati ya jua katika kisima cha Kizimbani namba 6 kilichopo Wilaya ya Wete Mkoa wa Kaskazini Pemba.

Kazi hiyo inayofanywa na kampuni ya Oikos East Africa kwa kushirikiana na ZAWA, mara baada ya kukamilika kwake inatarajiwa kuzalisha umeme wa kilowatt 36 ambao utatumika kuendeshea mitambo ya kusukumia maji katika kisima hicho. Hadi sasa tayari asilima 90 za utekelaji wa kazi hiyo imeshafikiwa.

Kitengo cha Uhusiano – ZAWA
Kizimbani Wete Pemba
08 FEBRUARI 2025

04/02/2025

ZAWA yaanza majaribio ya kutumia umeme wa jua kwenye visima vyake.

MAJI, TUIMARISHE HUDUMA

03/02/2025

Baada ya kutokea hitilafu ya kupasuka kwa bomba la maji linalopeleka maji maeneo ya mjini ambapo bomba hilo limepasuka katika eneo linaloendelea na ujenzi wa barabara ya flyover Amani round about.

Jitihada za kiufundi kutoka ZAWA zinaendelea kufanywa kwa haraka ili kurejesha huduma hiyo kwa wananchi.

Aidha, ZAWA inawataka wananchi kuwa wastahamilivu na kuwaomba radhi kwa usumbufu unaoendelea kujitokeza katika kipindi hichi.

MAJI, TUIMARISHE HUDUMA

Address

Mwembe Madema
Zanzibar City

Opening Hours

Monday 09:00 - 17:00
Tuesday 09:00 - 17:00
Wednesday 09:00 - 17:00
Thursday 09:00 - 17:00
Friday 09:00 - 17:00

Telephone

+255774778888

Alerts

Be the first to know and let us send you an email when Mamlaka ya Maji Zanzibar - ZAWA posts news and promotions. Your email address will not be used for any other purpose, and you can unsubscribe at any time.

Contact The Organization

Send a message to Mamlaka ya Maji Zanzibar - ZAWA:

Share