21/06/2025
Wakala wa Maabara ya Mkemia Mkuu wa Serikali Zanzibar yatoa mafunzo kwa Wadau mbali mbali wanaojihusisha na masuala ya kemikali juu ya usimamizi na udhibiti wa matumizi na udhibiti salama wa kemikali.
Akifungua mafunzo hayo kwa niaba ya Mkemia Mkuu wa Serikali Mkurugenzi Utawala,Rasilimali watu, Mipango ,Sera na Utafiti Ndugu.Omary Abadalla Ameir tarehe 21-06-2025 katika eneo la Hotel ya Madinatul bahari liliyopo Mbweni Zanzibar amesema, Taasisi imeamua kufanya mafunzo hayo yenye lengo la kuwajengea uwezo Wadau wanaotumia kemikali katika utoaji wa huduma zao ili kuweza kutumia vyema sheria na kanuni za kemikali pamoja na kulinda usalama wa matumizi.
Sambamba na hayo, Mkurugenzi wa Kemikali na Mazingira Ngugu,Ussi Makame Kombo alifafanua kuwa, udhibiti na usimamizi wa kemikali ni jukumu la pamoja, hivyo aliwataka Wadau kuwa na mashirikiano katika uhifadhi wa kemikali ili kuzuia athari zinazoweza kuathiri afya ya mtumiaji.
Aidha, aliwataka Wadau kusimamia suala zima la kanuni na mfumo wa kemikali unaotarajiwa kuanza kazi hivi karibuni kwa ajili ya utoaji wa vibali alisema,utarahisisha kazi kwa wakati na kushauri Wadau kutumia mfumo huo ili kuweza kuleta mabadiliko.
Akiwasilisha mafunzo juu ya sheria na kanuni juu ya utoaji,uombaji, usambazaji wa bidhaa za kemikali Mwanasheria Kombo Shaame Kombo alieleza kuwa, lengo la mafunzo ni Wadau kujua sheria na kanuni ili kulinda usalama na mazingira ya mtumiaji, hivyo ni lazima Wadau kutambua sheria za Kimataifa pamoja na sheria za ndani ili kuweza kusimamia vizuri kemikali kuwa ni matumizi salama wakati wa utoaji wa huduma.
Mbali na hayo, Mchunguzi Mkemia Ndugu, Ayman Othman Salum akiwasilisha mada ya usalama wa kemikali katika maeneo yanayohifadhiwa kemikali, utambuzi wa kemikali sambamba na njia zinazotakiwa kuchukuliwa na Wadau katika uwekaji na uhifadhi wa kemikali katika usalama.
Kwa upande wake Mkuu wa Divisheni ya Kemikali na Mazingira aliwasisha mada ya dharura za kemikali kwa mazingira na binaaadamu ili Wadau