28/07/2026
MHE. SORAGA AZINDUA BODI YA WAKURUGENZI YA MAMLAKA YA SERIKALI MTANDAO ZANZIBAR.
Mamlaka ya Serikali Mtandao Zanzibar (eGAZ) leo imezindua rasmi Bodi ya Wakurugenzi ya Mamlaka hiyo na wajumbe kusisitizwa kutekeleza na kuyafanyia kazi maono ya Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe. Dkt. Hussein Ali Mwinyi ya kuifanya Zanzibar ya kidijitali kwa kuiwezesha mifumo kusomana ili kukuza uchumi, kuondodha usumbufu pamoja na urasimu kwa wananchi.
Akizindua Bodi hiyo, Waziri wa Mawasiliano, Teknolojia ya Habari na Ubunifu Mhe. Mudrick Ramadhan Soraga ameyasema hayo leo wakati akizindua bodi hiyo na kuwataka wajumbe hao kuchukua hatua za haraka ili kufikia malengo hayo.
Nae Mwenyekiti wa bodi hiyo Ndugu Haji M. Haji alimshukuru Mhe. Waziri na kumuahidi kuwa watayatekeleza maagizo yote kwa kuyafanyia kazi kikamilifu kwa maendeleo ya Zanzibar.
Katika Hafla hiyo, mwenyekiti wa bodi hiyo amepata fursa ya kutoa hati za Ahadi na Uthibitisho wa wajumbe wa bodi hiyo.