16/08/2026
UJIO WA TREY SONGZ ZANZIBAR WAFUNGUA FURSA MPYA ZA UTALII, MUZIKI NA UCHUMI
Msanii maarufu wa R&B kutoka Marekani, Trey Songz, Amewasili Zanzibar akitokea Jijini Dar Es Salaam leo katika Kiwanja cha Ndege cha Abeid Aman Karume na Kupokelewa na viongozi wa Serikali, akiwemo Mkurugenzi wa Masoko, Kamisheni ya Utalii Zanzibar, Rahma Sanya, pamoja na Mkurugenzi wa Utumishi na Uendeshaji, Wizara ya Utalii na Mambo ya Kale.
Akizungumza mara ya Mapokezi hayo Mkurugenzi Masoko Kamishen ya Utalii Zanzibar amefahamisha kuwa Ujio wa Trey Songz, ambaye ana wafuasi wengi duniani, unaifanya Zanzibar kuendelea kuonekana k**a kituo cha kipekee cha Utalii na burudani kimataifa, huku Uwepo wa mastaa wa kiwango hicho ukitoa fursa ya kuitangaza Zanzibar kupitia Muziki, Mitandao ya kijamii na tasnia ya burudani.
Aidha, Nd. Rahma amesema kua ujio huo unaweza kuchochea fursa za kiuchumi kwa Vijana na Sekta binafsi, kuongeza Mahitaji ya huduma za Utalii, pamoja na kukuza mwingiliano wa Utamaduni na kuimarisha nafasi ya Zanzibar katika ramani ya burudani kimataifa.
Mkurugenzi ameeleza kuwa Zanzibar inaendelea kung'ara si kwa Uzuri wa fukwe na Urithi wake pekee, bali pia k**a sehemu ambayo burudani na Utalii inakutana jambo ambalo limzidi kuongeza Mvuto kimataifa kwa Visiwa hivi .
Rahma Sanya ZanzibarTourism treysongz Ikulu Zanzibar Zanzibar Airports Authority