Manispaa Magharibi "A"

Manispaa Magharibi "A" Ukurasa rasmi wa Baraza la Manispaa Magharibi "A" The Official Page of West "A" Municipal Council.

27/07/2026
Mkuu wa Wilaya ya Magharibi 'A' Mhe. Laila Burhani Ngozi, akiwa pamoja na Mstahiki Meya, Mkurugenzi na Waheshimiwa Madiw...
17/07/2026

Mkuu wa Wilaya ya Magharibi 'A' Mhe. Laila Burhani Ngozi, akiwa pamoja na Mstahiki Meya, Mkurugenzi na Waheshimiwa Madiwani wa Baraza la Manispaa Magharibi 'A' wamefanya kikao cha kujadili mikakati ya kuimarisha Usafi wa Mazingira na maendeleo ya mji.

Kikao hicho kimefanyika leo, tarehe 17 Julai 2026, katika Ukumbi wa Tume ya Uchaguzi, Mwera.

Mkurugenzi wa Baraza la Manispaa ya Magharibi 'A' Moh'd Simba Hassan, leo tarehe 14 Julai 2026, ameongoza kikao cha pamo...
14/07/2026

Mkurugenzi wa Baraza la Manispaa ya Magharibi 'A' Moh'd Simba Hassan, leo tarehe 14 Julai 2026, ameongoza kikao cha pamoja na Masheha pamoja na wawakilishi wa vikundi vya usafi kwa lengo la kujadili mikakati ya kuimarisha usafi wa mazingira katika shehia zote za Manispaa hiyo.

Kikao hicho kilichofanyika katika Ukumbi wa Baraza la Manispaa ya Magharibi 'A' Kianga, Zanzibar, kilijadili namna ya kuimarisha ushirikiano kati ya Manispaa, Masheha na vikundi vya Usafi ili kuhakikisha Mazingira yanakuwa safi, salama na yenye afya kwa Wananchi.

Baraza la Manispaa Magharibi 'A' limepokea ugeni kutoka Chuo Kikuu cha Harvard kutoka Marekani kwa ushirikiano na Taasis...
08/07/2026

Baraza la Manispaa Magharibi 'A' limepokea ugeni kutoka Chuo Kikuu cha Harvard kutoka Marekani kwa ushirikiano na Taasisi isiyo ya Kiserekali ya GENERATION ZANZIBAR ENVEROMENTAL COOPERATION UNION ( GZECU).

Ugeni huo umekuja kwa lengo la kufanya utafiti katika masuala ya Usafi wa Mazingira na mabadiliko ya tabianchi pamoja na usimamizi endelevu wa taka kwa Afya ya Jamii, faida ambazo zitapatikana kupitia ugeni huo ni pamoja na kuimarisha masuala mazima ya Afya na Mazingira hususani katika kupata Suluhisho la mabadiliko ya tabianchi.

Baraza linaendelea kuthamini ushirikiano na taasisi mbalimbali za kitaifa na kimataifa katika juhudi za kujenga Mazingira Safi, salama na yenye Afya kwa Wananchi wote.

Baraza la Manispaa Magharibi 'A' limekabidhiwa vyerehani kwa lengo la kuendeleza Kituo cha Wajasiriamali kinachomilikiwa...
06/07/2026

Baraza la Manispaa Magharibi 'A' limekabidhiwa vyerehani kwa lengo la kuendeleza Kituo cha Wajasiriamali kinachomilikiwa na Manispaa hiyo, kilichopo Dole, Wilaya ya Magharibi 'A'.

Mashine hizo zimekabidhiwa na Mkuu wa Mkoa wa Mjini Magharibi kupitia ufadhili wa SOS Zanzibar, ikiwa ni sehemu ya jitihada za kuimarisha ujuzi wa ufundi, kukuza ujasiriamali, na kuongeza fursa za ajira kwa wananchi.

Taarifa ya Makusanyo ya Mapato kwa Mwaka wa Fedha 2025/2026.
02/07/2026

Taarifa ya Makusanyo ya Mapato kwa Mwaka wa Fedha 2025/2026.

.
25/06/2026

.

Madiwani wa Baraza la Manispaa Magharibi 'A' wakipatiwa mafunzo juu mradi wa kuibua vipaumbele vitokanavyo na athari za ...
15/06/2026

Madiwani wa Baraza la Manispaa Magharibi 'A' wakipatiwa mafunzo juu mradi wa kuibua vipaumbele vitokanavyo na athari za Mabadiliko ya Tabia ya Nchi mafunzo hayo yalifanyika katika ukumbi wa manispaa hiyo Kianga.




Ushirikishwaji wa wananchi katika ngapi ya wadi Hadi Shehia kumeleta ufanisi mkubwa kwa kuweza kufanikisha zoezi zima la...
15/06/2026

Ushirikishwaji wa wananchi katika ngapi ya wadi Hadi Shehia kumeleta ufanisi mkubwa kwa kuweza kufanikisha zoezi zima la Uibuaji wa Vipaumbele vitokanavyo na Mabadiliko ya Tabia ya Nchi.




Team ya Mradi wa SCALE kutoka Baraza la Manispaa Magharibi A yafanya ziara katika wadi za Mwera, Welezo, Bububu na Kihin...
15/06/2026

Team ya Mradi wa SCALE kutoka Baraza la Manispaa Magharibi A yafanya ziara katika wadi za Mwera, Welezo, Bububu na Kihinani kwa lengo la kubaini changamoto zinazotokana na mabadiliko ya tabia nchi na kuweka mikakati ya kukabiliana nazo.




Address

Kianga
Zanzibar

Opening Hours

Monday 07:30 - 15:30
Tuesday 07:30 - 15:30
Wednesday 07:30 - 15:30
Thursday 07:30 - 15:30
Friday 07:30 - 15:30

Alerts

Be the first to know and let us send you an email when Manispaa Magharibi "A" posts news and promotions. Your email address will not be used for any other purpose, and you can unsubscribe at any time.

Shortcuts

Share