Tume ya Mipango Zanzibar

Tume ya Mipango Zanzibar Karibu katika ukurasa rasmi wa Tume ya Mipango Zanzibar

25/08/2026
24/08/2026

Zanzibar, Agosti 24, 2026 — Tume ya Mipango Zanzibar imefanya kikao kazi na washiriki mbalimbali wa maendeleo kutoka Jumuiya ya Umoja wa Mataifa, kwa lengo la kutathmini mafanikio yaliyopatikana katika utekelezaji wa Mpango wa Maendeleo ya Zanzibar (ZADEP), pamoja na kujadili changamoto zilizojitokeza katika utekelezaji wa ZADEP I.

Kikao hicho kilichofanyika leo katika Ukumbi wa Tume ya Mipango, Vuga, Mjini Zanzibar, kinalenga kuweka mikakati madhubuti ya kuhakikisha utekelezaji wa ZADEP II unakuwa na mafanikio makubwa zaidi na kuchochea maendeleo endelevu Zanzibar.

Aidha, kikao hicho kimejikita katika masuala ya uchumi jumuishi, kuongeza uelewa kuhusu maendeleo pamoja na kuhakikisha wadau wanashiriki kikamilifu katika mchakato wa kuandaa Mpango wa Maendeleo wa Miaka Mitano wa Zanzibar wa mwaka 2026–2031.

Washiriki wa kikao hicho wanatarajiwa kutoa uzoefu, mapendekezo na mitazamo mbalimbali itakayosaidia kuboresha utekelezaji wa ZADEP II, kwa kuzingatia mafanikio yaliyopatikana na changamoto zilizojitokeza katika awamu ya kwanza.

Katibu Mtendaji wa Tume ya Mipango Zanzibar Dkt. Josephine Rogate Kimaro amesema Serikali imeanza kuelekeza nguvu katika...
24/08/2026

Katibu Mtendaji wa Tume ya Mipango Zanzibar Dkt. Josephine Rogate Kimaro amesema Serikali imeanza kuelekeza nguvu katika utekelezaji wa Dira ya Maendeleo ya Zanzibar 2050 kupitia Mpango wa Maendeleo wa Zanzibar (ZADEP II) awamu ya Pili, unaolenga kuongeza uchumi, ajira na kipato cha wananchi.

Akizungumza wakati wa wa kikao cha uwasilishaji wa maandalizi ya ZADEP 2, kwa washirika wa Maendeleo huko Vuga alisema Zanzibar imepiga hatua katika sekta mbalimbali wakati wa utekelezaji wa ZADEP 1, ikiwemo uchumi wa bluu, miundombinu, afya, elimu, utalii na utawala bora.

Alisema uzalishaji wa samaki umeongezeka kutoka tani 38,000 mwaka 2020 hadi zaidi ya tani 80,000, hatua inayodhihirisha kukua kwa shughuli za uchumi wa bluu.

Katika miundombinu, alisema zaidi ya kilomita 1,000 za barabara zimejengwa, huku upatikanaji wa umeme vijijini ukifikia zaidi ya asilimia 85.

Alisema Serikali pia imeendelea kupanua viwanja vya ndege vya Pemba na Abeid Amani Karume kwa lengo la kuongeza fursa za utalii, biashara na uwekezaji.

Katika sekta ya afya, alisema maboresho yamefanyika kuanzia vituo vya afya vya msingi hadi hospitali za rufaa, pamoja na kuendelea na mipango ya kujenga na kuimarisha huduma maalumu.

Katibu Mtendaji Tume ya Mipango Zanzibar Dkt. Josephine Rogate Kimaro  amesema matumizi sahihi ya Takwimu za idadi ya wa...
20/08/2026

Katibu Mtendaji Tume ya Mipango Zanzibar Dkt. Josephine Rogate Kimaro amesema matumizi sahihi ya Takwimu za idadi ya watu ni muhimu katika kupanga na kutekeleza mipango ya maendeleo inayolenga kuimarisha maisha ya wananchi.

Akizungumza katika mkutano wa mashauriano kuhusu mipango ya maendeleo ya Zanzibar na uongozi wa Shirika la Umoja wa Mataifa la Idadi ya Watu (UNFPA) huko ofisini kwake Vuga alisema Serikali kupitia Tume ya Mipango Zanzibar inaendelea kuimarisha matumizi ya Takwimu katika kupanga maendeleo ya kiuchumi na kijamii.

Alisema lengo kubwa la Serikali ni kukuza uchumi unaowanufaisha wananchi wote kupitia utekelezaji wa Mpango wa Maendeleo Zanzibar (ZADEP), huku ikiweka mkazo katika kuongeza kipato cha wananchi, kuwawezesha kiuchumi na kuunda fursa zaidi za ajira.

Kamishna wa Idara ya Mipango ya Kitaifa na Maeneleo ya Kisekta kutoka Tume ya Mipango Zanzibar Mohamed Masoud Salim Ktoka Tume ya Mipango alieeleza hatua zinazochukuliwa katika kuimarisha uwajibikaji serikalini kupitia mfumo wa Mikataba ya utendaji, inayotarajiwa kuhusisha viongozi kuanzia Mawaziri, Makatibu Wakuu hadi ngazi za chini za utekelezaji wa shughuli za Serikali.

Nae kwa upande wake, Mwakilishi Mkaazi, Shirika la Umoja wa Mataifa la Idadi ya Watu (UNFPA) Mark Bryan Schreiner alieleza kuwa shirika linaendelea kuthamini ushirikiano wake wa muda mrefu na Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar, hasa katika masuala ya idadi ya watu na matumizi ya takwimu katika mipango ya maendeleo.

Imetolewa na kitengo cha Habari na Uhusiano
Tume ya Miapango Zanzibar
20.8.2026.

Katibu Mtendaji wa Tume ya Mipango Zanzibar, Dkt. Josephine Rugate Kimaro, ameongoza kikao kazi kilichowakutanisha viong...
19/08/2026

Katibu Mtendaji wa Tume ya Mipango Zanzibar, Dkt. Josephine Rugate Kimaro, ameongoza kikao kazi kilichowakutanisha viongozi wakuu wa Tume ya Mipango Zanzibar na ujumbe wa kidiplomasia kutoka Uingereza, kwa lengo la kutathmini mafanikio yaliyopatikana katika utekelezaji wa Mpango wa Maendeleo wa Zanzibar Awamu ya Kwanza (ZADEP I) na kuweka misingi ya utekelezaji wa awamu ya pili ya mpango huo, ZADEP II.

Kikao hicho kilichofanyika leo katika Ukumbi wa Wizara ya Fedha na Mipango, kimejadili maeneo mbalimbali ya ushirikiano wa maendeleo kati ya Zanzibar na Uingereza.

Akizungumza katika kikao hicho, Dkt. Kimaro amesema ushirikiano huo umejikita katika sekta mbalimbali, zikiwemo miundombinu, utalii, uimarishaji wa taasisi za Serikali, usalama na utawala bora.

Amesema Uingereza imeendelea kuwa mshirika muhimu katika utekelezaji wa miradi ya maendeleo Zanzibar, ikiwemo miradi ya ujenzi na uimarishaji wa miundombinu mbalimbali.

Aidha, amesema ushirikiano huo unalenga kuimarisha utoaji wa huduma za kijamii, kuongeza fursa za ajira na kupanua wigo wa shughuli za kiuchumi, hatua ambazo zinatarajiwa kuongeza mapato ya wananchi pamoja na Serikali.

Kwa upande wake, Kamishna wa Idara ya Mipango ya Kitaifa na Maendeleo ya Kisekta kutoka Tume ya Mipango Zanzibar, Mohamed Masoud Salim, amesema barabara zinazojengwa katika maeneo ya Fumba na Kizimkazi ni za kimkakati

Kamishna Salim amefahamisha kuwa Serikali tayari imeweka mikakati thabiti ya kuimarisha ulinzi na usalama, huduma za dharura za afya, pamoja na upanuzi wa miundombinu ya usafiri.

Aidha, amesema mipango hiyo inajumuisha upanuzi wa uwanja wa ndege ili kufikia uwezo wa kuhudumia wageni milioni 1.1, sambamba na kuanzishwa kwa mfumo wa usafiri wa umma unaotumia mabasi ya umeme.

Hatua hizo ni sehemu ya juhudi za Serikali za kuimarisha miundombinu, kukuza shughuli za kiuchumi na kijamii, pamoja na kuweka mazingira wezeshi ya kufikiwa kwa malengo ya maendeleo ya Zanzibar.

KAMISHNA Idara ya Mipango ya Maendeleo ya Watenda Kazi Dkt Rukkayya Wakif  Mohamed  ameongoza Kikao kazi  cha Wakurugenz...
17/08/2026

KAMISHNA Idara ya Mipango ya Maendeleo ya Watenda Kazi Dkt Rukkayya Wakif Mohamed ameongoza Kikao kazi cha Wakurugenzi Utumishi na Uendeshaji wa Wizara na Taasisi mbali mbali wa Serikali ya Mapinduzi Zanzibar chenye lengo la kuwapa uelewa jinsi ya matumizi ya Mfumo maalum wa Rasilimali watu .

Mfumo huo utasaidia kupata wataalaum na kuweza kuondokana na tatizo la rasilimali watu ambalo linazikabili taasisi nyingi za serikali.

Kikao hicho kilichofanyika katika Ukumbi wa Tume ya Mipango Vuga Mjini Zanzibar kilihudhuriwa na Wakurugenzi Utumishi kutoka Wizara na Taasisi mbali mbali kutoka serikali ya Mapinduzi Zanzibar.

Wakitoa maoni yao washiriki wa kikao hicho waliwashauri wataalamu wa mfumo huo mambo mbali mbali k**a vile kuongeza Ulizi na Usalama na kuwa na mbinu mbadala ya kuhifadhi Taarifa pindi tatizo lolote likijitokeza.

Akifunga Mafunzo hayo Dkt Rukkaya amewasihi Wakurugenzi hao kuweza kutumia Mafunzo hayo na kushajiisha Watumishi wao waweze kujiunga na mfumo huo ili iwe chachu kwa wengine kupata ushawishi Zaidi kuutumia ili kuweza kufikia lengo lililokusudiwa na serikali.

17/8/2026

Katibu Mtendaji Tume ya Mipango  Zanzibar Dkt Josephine Rogate Kimaro ameongoza kikao cha  Kamati ya Wataalamu ya Tume y...
15/08/2026

Katibu Mtendaji Tume ya Mipango Zanzibar Dkt Josephine Rogate Kimaro ameongoza kikao cha Kamati ya Wataalamu ya Tume ya Mipango Zanzibar ikiwa ni kikao chake cha kwanza kuongoza tangu Kuteuliwa kwake na Muheshimiwa Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dkt Hussein Ali Mwinyi .

Kikao hicho cha siku mbili kimefanyika katika Ukumbi wa Tume ya Mipango Zanzibar Vuga Mjini Zanzibar kilihudhuriwa na wataalamu wa Tume ya Mipango pamoja na wataalamu wengine kutoka Taasisi mbali mbali kutokana na ripoti hizo zinavohusisha moja kwa moja Taasisi na sekta zao.

15/8/2026.

Waziri wa Fedha na Mipango, Dkt. Juma Malik Akil, amezitaka Sekta Binafsi nchini kushirikiana kwa karibu na Serikali kat...
14/08/2026

Waziri wa Fedha na Mipango, Dkt. Juma Malik Akil, amezitaka Sekta Binafsi nchini kushirikiana kwa karibu na Serikali katika utekelezaji wa Mpango wa Maendeleo wa Zanzibar wa miaka Mitano kwa awamu ya pili (ZADEP II), ili kufanikisha malengo ya maendeleo na kukuza Uchumi Jumuishi.

Dkt. Akil alisema hayo wakati akizungumza katika Mkutano wa kujadili utekelezaji wa ZADEP II uliowakutanisha viongozi wa Serikali, sekta binafsi, wawekezaji na wadau mbalimbali wa maendeleo, huko Golden Tulip Uwanja ndege Zanzibar.

Alisema ushiriki wa sekta binafsi unapaswa kwenda zaidi ya kuhudhuria mikutano pekee bali ni kuwa sehemu ya utekelezaji wa mipango ya maendeleo, ambapo Serikali pekee haiwezi kufikia malengo ya maendeleo bila ushiriki madhubuti wa sekta hizo.“Serikali pekee haiwezi kufanya mabadiliko haya yote, tunataka sekta binafsi iwe kwenye usukani wa utekelezaji wa ZADEP II,” alisema Dkt. Akil.

Nae Katibu Mtendaji wa Tume ya Mipango Zanzibar Dkt. Josephine Rogate Kimario alisema mkutano huo umelenga kuwakutanisha Serikali na sekta binafsi ili kujadili namna ya kufadhili na kutekeleza Mpango wa Maendeleo wa Zanzibar wa miaka Mitano wa awamu ya pili (ZADEP II), pamoja na kuweka mikakati ya kupanga, kuweka vipaumbele na kupanga utekelezaji wa mipango hiyo.

Alisema Serikali imefanikiwa kutekeleza ZADEP I, ambapo tathmini imeonesha kupatikana kwa maendeleo katika maeneo mbalimbali, na kwamba sasa Serikali imeandaa rasimu ya ZADEP II inayohitaji ushirikiano wa wadau mbalimbali, hususan sekta binafsi, katika hatua za utekelezaji.

Kwa uapnde wake, Kamishna wa Idara ya Mipango ya Kitaifa Maendeleo ya Kisekta kutoka Tume ya Mipango Zanzibar Mohamed Masoud Malim alisema Dira ya Maendeleo ya Zanzibar 2050 inalenga kufikisha Zanzibar katika hadhi ya Uchumi wa kipato cha kati cha juu ifikapo mwaka 2050 kupitia Maendeo endelevu na jumuishi ya watu.

13/8/2026
Golden Tulip
Uwanja wa ndege

Address

Vuga
Zanzibar

Opening Hours

Monday 07:30 - 15:30
Tuesday 07:30 - 15:30
Wednesday 07:30 - 15:30
Thursday 07:30 - 15:30
Friday 07:30 - 15:30

Alerts

Be the first to know and let us send you an email when Tume ya Mipango Zanzibar posts news and promotions. Your email address will not be used for any other purpose, and you can unsubscribe at any time.

Shortcuts

Share