01/09/2026
Katibu Mkuu Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa, Serikali za Mitaa na Idara Maalum za SMZ, Ndugu Issa Mahfoudh Haji, amewataka wahandisi kuandaa michoro na makisio halisi ya bajeti ya miradi mbalimbali iliyoibuliwa, ili kuhakikisha inatekelezwa kwa ufanisi, uwazi na uwajibikaji.
Ameyasema hayo wakati akifungua mafunzo ya wahandishi kutoka Mamlaka za Serikali za Mitaa za Unguja na Pemba, yaliyofanyika katika Hoteli ya Visitorβs Inn, Jambiani, Mkoa wa Kusini Unguja.
Amesema miradi hiyo inalenga kupunguza uharibifu wa miundombinu unaosababishwa na mvua kubwa, ukame na athari nyingine za mabadiliko ya tabianchi.
Akiwasilisha mada katika mafunzo hayo, Mhandisi wa Miradi kutoka Wakala wa Barabara za Vijijini na Mijini, TARURA, Eng. Thobias Malando, amesema ni muhimu kushirikisha jamii katika hatua za awali za uandaaji wa taarifa na michoro ya miradi.
Kwa upande wake, Mkurugenzi wa Idara ya Uratibu wa Serikali za Mitaa, Zainab Khamis Kibwana, amesema mafunzo hayo yanalenga kuwajengea wahandisi uwezo wa kuibua na kuandaa miradi yenye tija inayozingatia mahitaji ya ya jamii katika kukabilinana Athari za mabadilko ya Tabia nchi,
Nao Wahandisi walioshiriki mafunzo hayo wamesema wamepata ujuzi utakaowasaidia kuandaa michoro na makisio ya gharama kwa usahihi, hatua itakayorahisisha utekelezaji wa mirad hiyo.
Jumla ya miradi 38 iliobuliwa katika Mikoa mbali mbali inatarajiwa kutekelezwa kupitia Program ya Uhimilivu wa Athari za mabadiliko ya Tabianchi (Scale Program) inayofadhiliwa na Benki ya Dunia.
π 01 Septemba, 2026
π Jambiani, Zanzibar.