Zanzibar Investment Promotion Authority

Zanzibar Investment Promotion Authority ZIPA is responsible for promotion and facilitation of investment in Zanzibar

Zanzibar Investment Promotion Authority is a semi autonomous government institution operating under the Zanzibar Investment Promotion and Protection Authority Act No. 10 of 2023.

14/08/2026

Pemba inaendelea kuwa sehemu muhimu katika utekelezaji wa ajenda ya Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar ya kukuza uchumi kupitia uwekezaji.

Eneo Huru la kiuchumi la Micheweni, lenye ukubwa wa hekta 808, limeandaliwa kwa ajili ya uwekezaji katika shughuli mbalimbali za kiuchumi likiwa na fursa katika uchakataji wa mazao ya kilimo, uvuvi na shughuli za baharini, uzalishaji, usafirishaji na uhifadhi wa bidhaa, nishati jadidifu pamoja na huduma zinazohusiana na utalii.

Uwepo wa eneo hili unatoa nafasi kwa wawekezaji kutumia fursa zilizopo Pemba, huku wakinufaika na vivutio vya uwekezaji vinavyotolewa Pemba kupitia ZIPA.

Micheweni ni sehemu ya mkakati wa kuendeleza uwekezaji nje ya maeneo ya mijini, kuongeza shughuli za uzalishaji, ajira na kuchochea ukuaji wa uchumi wa Pemba na Zanzibar kwa ujumla.

Tembelea na wekeza Zanzibar sasa!

KAMATI YA BARAZA LA WAWAKILISHI YA UCHUMI NA UWEKEZAJI YAKAGUA UTEKELEZAJI WA MRADI WA BARABARA YA FUMBAKamati ya Baraza...
13/08/2026

KAMATI YA BARAZA LA WAWAKILISHI YA UCHUMI NA UWEKEZAJI YAKAGUA UTEKELEZAJI WA MRADI WA BARABARA YA FUMBA

Kamati ya Baraza la Wawakilishi ya Uchumi na Uwekezaji Zanzibar imefanya mkutano na Mamlaka ya Kukuza Uwekezaji Zanzibar (ZIPA) ambapo imejadili utekelezaji wa Mradi wa Ujenzi wa Barabara ya Fumba yenye urefu wa kilomita nane (8km) katika maeneo huru ya uwekezaji.

Akizungumza wakati wa mkutano huo, Mwenyekiti wa Kamati hiyo, Mhe. Makame Mohammed Sufian, amesema kuwa Kamati inaendelea kufuatilia utekelezaji wa miradi inayolenga kuboresha miundombinu ya uwekezaji Zanzibar, ikiwemo barabara ya Fumba, ili kuhakikisha miradi hiyo inatekelezwa kwa ufanisi na kutoa matokeo yanayotarajiwa katika kukuza shughuli za kiuchumi.

Kwa upande wake, Mkurugenzi Mtendaji wa Mamlaka ya Kukuza Uwekezaji Zanzibar (ZIPA), Ndg. Saleh Saad Mohamed, amesema kuwa mradi huo ni sehemu ya juhudi za Serikali za kuimarisha miundombinu katika maeneo yaliyotengwa kwa ajili ya uwekezaji, hatua inayolenga kurahisisha usafiri na kuchochea ukuaji wa shughuli za kiuchumi katika eneo la Fumba.

Ameeleza kuwa ujenzi wa barabara hiyo utakuwa na mchango muhimu katika kuimarisha muunganiko wa miundombinu ndani ya maeneo ya uwekezaji, sambamba na kuweka mazingira bora kwa wawekezaji kuanzisha na kupanua shughuli zao.

Aidha, amesema maendeleo ya miundombinu katika maeneo ya uwekezaji yanaendana na maandalizi mapana ya Zanzibar kuelekea AFCON 2027, ambapo Serikali inaendelea kuimarisha miundombinu na huduma muhimu ili kuongeza uwezo wa Zanzibar kuwa mwenyeji wa matukio makubwa ya kimataifa.

ZANZIBAR INVESTMENT BANK KUJA NA FURSA MPYA YA MITAJI KWA WAWEKEZAJI ZANZIBARSerikali ya Mapinduzi Zanzibar imeendelea k...
12/08/2026

ZANZIBAR INVESTMENT BANK KUJA NA FURSA MPYA YA MITAJI KWA WAWEKEZAJI ZANZIBAR

Serikali ya Mapinduzi Zanzibar imeendelea kuchukua hatua za kuimarisha mazingira ya uwekezaji kwa kuandaa uanzishwaji wa Benki ya Uwekezaji Zanzibar (ZIB), taasisi inayolenga kuongeza upatikanaji wa mitaji kwa wawekezaji na kuchochea ukuaji wa uchumi wa Zanzibar.

Hayo yameelezwa na Mkurugenzi Mtendaji wa Mamlaka ya Kukuza Uwekezaji Zanzibar (ZIPA), Ndg. Saleh Saad Mohamed, wakati akifungua kikao kazi kilichowakutanisha wadau mbalimbali wa uwekezaji, kilichofanyika Maruhubi, Zanzibar.

Mkurugenzi Saleh amesema uanzishwaji wa benki hiyo utasaidia kwa kiasi kikubwa kuimarisha mazingira ya uwekezaji Zanzibar na kuwa kichocheo muhimu cha ukuaji wa uchumi.

“Lengo la benki hii ni kuhakikisha wawekezaji na miradi ya kimkakati wanapata mifumo na vyanzo vya fedha vinavyohitajika ili kukua na kufikia malengo yao,” amesema.

Kwa upande wao, ujumbe kutoka Wizara ya Fedha, pamoja na kampuni inayoshirikiana katika mchakato wa kuanzishwa kwa Benki ya Uwekezaji Zanzibar, umeeleza kuwa benki hiyo inatarajiwa kutoa fursa mbalimbali za ufadhili, ikiwemo ikiwemo ufadhili wa miradi, huduma za benki ya uwekezaji, uwekezaji wa mtaji wa hisa na uhamasishaji wa mitaji, ili kusaidia miradi yenye uwezo mkubwa kufikia hatua ya utekelezaji.

Wamesema sekta zinazoweza kunufaika na huduma hizo ni pamoja na miundombinu, uchumi wa buluu, viwanda, biashara ndogo na za kati (SMEs), utalii, nishati, pamoja na miradi mingine ya kimkakati inayokwenda sambamba na vipaumbele vya Serikali ya Zanzibar.

Aidha, wameeleza kuwa ZIB inatarajiwa kuunganisha na kuwezesha upatikanaji wa mitaji kutoka vyanzo mbalimbali, ikiwemo Serikali, taasisi za maendeleo, sekta binafsi, masoko ya mitaji, pamoja na wawekezaji wa ndani na wa kimataifa.

Hatua hiyo inalenga kuongeza uwezo wa Zanzibar katika kuvutia na kuelekeza mitaji mikubwa kwenye miradi yenye tija, kuchochea uwekezaji katika sekta muhimu za uchumi na hatimaye kuharakisha maendeleo endelevu ya Zanzibar.

10/08/2026

ZIPA YAWAKARIBISHA WAFANYABIASHARA WAZAWA KUSAJILI BIASHARA ZAO ZIPA

Mamlaka ya Kukuza Uwekezaji Zanzibar (ZIPA) inawatangazia wafanyabiashara wote wenye nia ya kukuza na kuendeleza biashara zao, kutumia fursa ya kusajili biashara zao na kunufaika na huduma na fursa mbalimbali za uwekezaji.

Kupitia usajili wa mradi wako ZIPA, utaweza kupata:

✅ Cheti cha Uwekezaji
✅ Kuwezeshwa kupata huduma kupitia One Stop Centre
✅ Mwongozo na ushauri wa kitaalamu kuhusu biashara na uwekezaji wako
✅ Kunufaika na vivutio na fursa mbalimbali zinazotolewa kwa wawekezaji wanaokidhi vigezo

🌾 Heri ya Siku ya Wakulima (8/8)! 🌿Mamlaka ya Kukuza Uwekezaji Zanzibar (ZIPA) inawatakia wakulima wote Heri ya Siku ya ...
08/08/2026

🌾 Heri ya Siku ya Wakulima (8/8)! 🌿

Mamlaka ya Kukuza Uwekezaji Zanzibar (ZIPA) inawatakia wakulima wote Heri ya Siku ya Wakulima (Nane Nane).

Tunatambua na kuthamini mchango mkubwa wa wakulima katika kuimarisha usalama wa chakula, kukuza uchumi na kuendeleza maendeleo endelevu ya Zanzibar.

ZIPA inaendelea kuhamasisha uwekezaji katika sekta ya kilimo, hususan katika kilimo cha kisasa, uchakataji wa mazao na kuongeza thamani ya bidhaa za kilimo ili kufungua fursa zaidi za ajira na ukuaji wa uchumi.

Tunawaenzi wakulima wote kwa juhudi, ubunifu na uzalendo wao katika kulijenga Taifa.

🌾 Heri ya Siku ya Wakulima – Nane Nane! 🌱

*ZIPA YAVUTIA WAWEKEZAJI WA ETHIOPIA KUWEKEZA HOTELI YA NYOTA TANO ZANZIBAR*Mkurugenzi Mtendaji wa Mamlaka ya Kukuza Uwe...
07/08/2026

*ZIPA YAVUTIA WAWEKEZAJI WA ETHIOPIA KUWEKEZA HOTELI YA NYOTA TANO ZANZIBAR*

Mkurugenzi Mtendaji wa Mamlaka ya Kukuza Uwekezaji Zanzibar (ZIPA), Saleh Saad Mohamed, amekutana na kufanya mazungumzo na ujumbe wa wawekezaji kutoka Supper Addis Hotel ya nchini Ethiopia waliowasili Zanzibar kwa lengo la kuangalia fursa ya kuwekeza Hoteli yenye hadhi ya Nyota Tano, ikiwa ni sehemu ya kuimarisha Uwekezaji katika sekta ya Utalii.

Katika mazungumzo hayo, Mkurugenzi Mtendaji ameeleza ujumbe huo kuhusu fursa mbalimbali za uwekezaji zilizopo Zanzibar na kubainisha kuwa, Serikali imeendelea kuboresha mazingira ya biashara na uwekezaji kupitia sera rafiki zinazowavutia wawekezaji wa ndani na wa kimataifa, hususan katika sekta ya utalii ambayo inaendelea kuwa nguzo muhimu ya uchumi wa Zanzibar.

Ameeleza kuwa, Sheria ya Uwekezaji Na. 10 ya mwaka 2023 imeondoa urasimu katika usajili na utekelezaji wa miradi ya uwekezaji kwa kuimarisha huduma kupitia Kituo Kimoja cha Utoaji Huduma kwa Wawekezaji (One Stop Centre), hatua inayorahisisha upatikanaji wa huduma muhimu kwa wakati na kuongeza ufanisi katika utekelezaji wa miradi ya kimkakati Zanzibar.

Aidha, amewafahamisha kuwa sheria na kanuni za uwekezaji za Zanzibar zipo kwa lengo la kulinda mitaji ya wawekezaji, kuhakikisha uwazi katika utekelezaji wa miradi na kutoa uhakika wa mazingira salama na yenye ushindani kwa biashara na uwekezaji wa muda mrefu.

07/08/2026

ZIPA YAPIGA MARUFUKU SHUGHULI ZA KIJAMII NDANI YA MAENEO YA UWEKEZAJI

Mamlaka ya Kukuza Uwekezaji Zanzibar (ZIPA) imepiga marufuku kufanyika kwa shughuli zozote za kijamii ndani ya maeneo yaliyotengwa kwa ajili ya uwekezaji katika visiwa vya Unguja na Pemba huku ikiwataka wananchi kuheshimu matumizi yaliyokusudiwa katika Maeneo hayo.

ZIPA umesema kuwa ni kinyume cha sheria kufanya shughuli k**a uuzaji wa viwanja, ukataji wa miti, uchimbaji wa mchanga pamoja na shughuli nyingine zozote zisizoruhusiwa ndani ya maeneo ya uwekezaji, yakiwemo Fumba, Dimani, Micheweni, Mashamba ya Mipira Pemba na kichwele.

imefafanua kuwa, maeneo hayo yametengwa mahsusi kwa ajili ya uwekezaji na yanalindwa kwa mujibu wa sheria ili kuhakikisha yanatumika kwa malengo yaliyokusudiwa na Serikali katika kuchochea ukuaji wa uchumi na maendeleo ya Zanzibar.

05/08/2026
ZIPA YAFANYA ZIARA MAALUM KISIWA CHA KWALE KUFUATILIA UWEKEZAJI WA KIMKAKATIMkurugenzi Mtendaji wa Mamlaka ya Kukuza Uwe...
31/07/2026

ZIPA YAFANYA ZIARA MAALUM KISIWA CHA KWALE KUFUATILIA UWEKEZAJI WA KIMKAKATI

Mkurugenzi Mtendaji wa Mamlaka ya Kukuza Uwekezaji Zanzibar (ZIPA), Ndg. Saleh Saad Mohamed, amefanya ziara maalum katika Kisiwa cha Kwale kwa lengo la kukagua eneo la uwekezaji na kufuatilia maendeleo ya maandalizi ya mradi mkubwa unaotarajiwa kutekelezwa katika eneo hilo.

Katika ziara hiyo, Mkurugenzi Mtendaji wa ZIPA amekagua eneo ambalo tayari limepata mwekezaji na kujionea mazingira halisi ya utekelezaji wa mradi huo, sambamba na kutoa taarifa muhimu kuhusu hatua zinazofuata za uwekezaji huo ili kuhakikisha unatekelezwa kwa ufanisi.

Akizungumza wakati wa ziara hiyo, Ndg. Saleh Saad Mohamed ameeleza dhamira ya Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar ya kuendeleza visiwa vidogo vidogo kwa kuvutia na kusimamia uwekezaji wenye tija, ambao utaongeza fursa za ajira, kukuza uchumi na kuboresha maisha ya wananchi.

Aidha, amekutana na wafanyabiashara, watoa huduma pamoja na wananchi wa Kisiwa cha Kwale na kuwaeleza kuwa Serikali itaendelea kuweka mazingira bora ya uwekezaji na kuhakikisha miradi inayokuja inaleta manufaa makubwa kwa jamii inayozunguka maeneo hayo.

Ziara hiyo ni sehemu ya juhudi za ZIPA katika kufuatilia utekelezaji wa miradi ya uwekezaji na kuhakikisha wawekezaji wanapata ushirikiano unaohitajika kutoka kwa Serikali katika hatua mbalimbali za maendeleo ya miradi yao.

Katika ziara hiyo, Mkurugenzi Mtendaji wa ZIPA ameambatana na watendaji wa ZIPA, maafisa kutoka Kamisheni ya Utalii Zanzibar pamoja na maafisa kutoka Wizara ya Ardhi, ambao kwa pamoja walifanya ukaguzi wa eneo hilo na kujadili hatua muhimu za kuendeleza uwekezaji katika Kisiwa cha Kwale.

29/07/2026

Zanzibar Investment Promotion Authority (ZIPA) invites investors to discover the opportunities that Zanzibar has to offer.

Through investment facilitation, guidance and dedicated support, ZIPA serves as a trusted partner, helping investors navigate their journey and build successful ventures in Zanzibar.

Address

V656+XV Zanzibar
Zanzibar

Opening Hours

Monday 07:30 - 15:30
Tuesday 07:30 - 15:30
Wednesday 07:30 - 15:30
Thursday 07:30 - 15:30
Friday 07:30 - 15:30

Alerts

Be the first to know and let us send you an email when Zanzibar Investment Promotion Authority posts news and promotions. Your email address will not be used for any other purpose, and you can unsubscribe at any time.

Shortcuts

Share