UVCCM Mkoa wa Magharibi

UVCCM Mkoa wa Magharibi Contact information, map and directions, contact form, opening hours, services, ratings, photos, videos and announcements from UVCCM Mkoa wa Magharibi, Political organisation, Mwera, Zanzibar.

RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe. Dk. Ali Mohamed Shein leo amewapisha Washauri wa Rais wa Zanz...
03/10/2019

RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe. Dk. Ali Mohamed Shein leo amewapisha Washauri wa Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi aliowateua hivi karibuni.

Walioapishwa ni Bwana Abdalla Rashid Abdalla aliyeapishwa kuwa Mshauri wa Rais Mambo ya Siasa.

Aidha, Dk. Shein amemuapisha Bwana Ali Mzee Ali kuwa Mshauri wa Rais katika Masuala ya Historia na Mambo ya Kale.

Hafla ya kuwapishwa viongozi hao ilifanyika Ikulu Mjini Zanzibar na kuhudhuriwa na viongozi mbali mbali wa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar akiwemo Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Idd, Spika wa Baraza la Wawakilishi Zubeir Ali Maulid

Viongozi wengine waliohudhuria hafla hiyo ni Jaji Mkuu wa Zanzibar Omar Othman Makungu, Mawaziri, Mwanasheria Mkuu wa Serikali Said Hassan Said, Katibu Mkuu Kiongozi na Katibu wa Baraza la Mapinduzi Dk. Abdulhamid Yahya Mzee na Makatibu Wakuu.

Wengine ni M***i Mkuu wa Zanzibar Sheikh Saleh Omar Kabih, Naibu Kadhi wa Zanzibar Sheikh Hassan Othman Ngwali, Mkuu wa Mkoa wa Mjini Magharibi Hassan Khatib Hassan, Meya wa Manispaa ya Mji wa Zanzibar Khatib Abrahman Khatib, Viongozi wa Vikosi vya SMZ, Washauri wa Rais wa Zanzibar, viongozi wengine wa Serikali pamoja na wanafamilia.

01/10/2019
RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Dk. Ali Mohamed Shein, amelitaka Shirika la Meli Zanzibar kuwa na...
01/10/2019

RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Dk. Ali Mohamed Shein, amelitaka Shirika la Meli Zanzibar kuwa na mipango madhubuti ya mafunzo kwa watendaji na waongozaji wa vyombo vya baharini, ili kuweza kufanyakazi zao kwa weledi.

Dk. Shein amesema hayo katika sherehe za uzinduzi wa Meli mpya ya Mafuta ya MT. Ukombozi ll, zilizofanyika Bandarini Malindi, mjini hapa.

Alisema wafanyakazi wanaoendesha vyombo baharini wana jukumu kubwa katika utekelezaji wa kazi zao, hivyo ni vyema kwa Shirika hilo likawa na mipango madhubuti katika upatikani wa mafunzo ya muda mrefu, kati na muda mfupi ili waweze kutekeleza kazi zao kwa ufanisi.

Aliutaka uongozi huo kutotosheka na utaalamu walionao watendaji wake, hivyo akataka ratiba maalum za mafunzo ziandaliwe, sambamba na kuwapa mishahara na stahiki zote zinazoendana na ukubwa wa kazi wanazofanya.

“Hawa wanafanya kazi nzito sana, sio rahisi kuranda na meli baharini kila siku, nasisistiza upatikanaji wa taaluma katika kuendesha vyombo hivi”, alisema.

Aidha, aliutaka uongozi huo kuhakikisha watendaji hao wanajuwa kanuni na sheria za nchi pamoja na zile za kimataifa, ili waweze kutekeleza vyema kazi zao.

Dk. Shein alitumia fursa hiyo kusisitiza umuhimu wa wafanyakazi wa meli hiyo kufanyakazi kwa misingi ya uwajibikaji, uadilifu na nidhamu, kwa kigezo kuwa hatua hiyo itawajengea heshima.

“Lazima tuzingatie nidhamu ya kazi zetu, mfanye kazi kwa kuzingatia imani, nidhamu na uwajibikaji kikamilifu”, alisema.

Vile vile, Dk. Shein aliwataka watendaji wa meli hiyo kuendeleza ushirikiano uliopo kati yao, sambamba na kusisitiza umuhimu wa kuwepo uangalifu na umakini ili uwepo usalama wa wafanyakazi na mali za serikali.

Aidha, alisifia ubora wa meli hiyo kwa kuwa katika viwango vya kimataifa, k**a ilivyo kwa meli ya MV, Mapinduzi ll.

Dk. Shein aliwatanabahisha wananchi akiwataka kuwa wazalendo kwa kuwa na utamaduni wa kuvipenda na kuvitukuza vilivyo vyao, badfala ya kuviponda.

“Hii ni meli yetu sote watu wa Zanzibar………………..imenunuliwa na Serikali yetu kwa manufaa yetu”, alisema.

Alieleza kuwa ujio wa meli hiyo unatarajiwa kuondoa kabisa tatizo la upungufu wa mafuta linalojitokea mara kwa mara nchini, akibainisha kuwa hivi sasa Serikali italazimika kuhoji pale nishati hiyo itakapoadimika.

Aidha, alisema uaptikanaji wa meli hiyo ni kichocheo katika uharakishaji wa ujenzi wa Bandari mpya ya Mpigaduri,

Katika hatua nyengine, Dk. Shein alisema uamuzi wa Serikali wa kujenga Bandari ya Mpigaduri upo pale pale, ukitarajiwa kuanza mishoni mwa mwaka huu au mapema mwakani.

Alisema serikali tayari imefanikisha maandalizi ya ujenzi wa Bandari mpya kwa ajili ya Mafuta na Gesi katika eneo la Mangapwani, kwa kuweka miundombinu, ikiwemo uwekaji wa umema, ujenzi wa barabara pamoja na nyumba kwa ajili ya wakaazi wa Dundua.

Aidha, alisema Serikali imefanikisha ununuzi wa meli za MV Mapinduzi 11, MT Ukombozi 11 ambapo kwa ujumla zimegharimu zaidi ya shilingi Bilioni 136 , pamoja na mambo mbali ya maendeleo, kutokana na kuimarika kwa uchumi wake, hatua inayotokana na ukusanyajii mzuri wa mpato.

Mapema, Waziri wa Ujenzi, Mawasiliano na Usafirishaji, Sira Ubwa Mamboya alisema ujenzi wa meli hiyo ni utekelezaji wa Ilani ya CCM ya 2015-2020, na kubainisha kuwa kwa kiasi kikubwa serikali imekamilisha ahadi zake.

Alisema Wizara hiyo inalenga kuaanda utaratibu maalum kwa Wazanzibari wote wenye nia ya kuiona meli hiyo kupata fursa hiyo, sambamba na kuahidi kuitunzwa ili iweze kuleta tija kwa Taifa.

Nae, Waziri wa Fedha na Mipango, ambae pia ni Mwenyekiti wa Kamati ya Ujenzi wa Meli hiyo, Balozi Mohamed Ramia, alisema meli hiyo ni bora na kubainisha kuwa thamani yake inaendana na hali halisi ya mahitaji, hivyo kuwa kichocheo katika uingizaji wa mapato na kukuza uchumi wa Taifa.

Aidha, akitowa salam mjenzi wa meli hiyo kutoka Kampuni ya DAMEN ya nchini Uholanzi Ronald Maat, alisema meli hiyo imeundwa kwa kufuata viwango vya kimataifa na kuzingatia usalama baharini.

Alitowa pongezi kwa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar kwa uamuzi wake wa kujenga meli hiyo na kubainisha azma ya Kampuni kuiunga mkono Serikali kwa juhudi zake za kuifanya kuwa na vyombo vya uhakika vya usafiri baharini, hususan katika usafirishaji wa mafuta.

Mapema, Katibu Mkuu Wizara ya ujenzi, Mawasiliano na Usafirishaji, Mustafa Aboud Jumbe alisema ujenzi wa meli hiyo iliyotengenzwa na Kampuni ya DAMEN kutoka Uholanzi, umegharimu shilingi Bilioni 36 hadi kukamilika kwake.

Alisema ujenzi huo umegharamiwa na serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar na kubainisha kuwa fedha zote zimeshalipwa katika Kampuni husika.

Alisema meli hiyo yenye urefu wa mita 86.21 ina uwezo wa kubeba tani 3,500 za mafuta ya aina nne, ikiwemo mafuta taa, Dizeli, Petroli na mafuta ndege.

Katika hafla hiyo,pamoja na mambo mengine kulifanyika tukio la makabidhiano ya meli hiyo baina ya mjenzi kutoka Kampuni ya DAMEN na Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar.

01/10/2019
MAKAMO MWENYEKITI WA UVCCM TAIFA NDUGU TABIA M. MWITA (MNEC) AFUNGUA MKUTANO MKUU WA CHAMA CHA MAPINDUZI JIMBO LA BUBUBU...
29/09/2019

MAKAMO MWENYEKITI WA UVCCM TAIFA NDUGU TABIA M. MWITA (MNEC) AFUNGUA MKUTANO MKUU WA CHAMA CHA MAPINDUZI JIMBO LA BUBUBU LEO JUMAPILI TAREHE 29.09.2019 KATIKA UKUMBI WA CHUO CHA KUMBUKUMBUKU YA MWALIMU NYERERE CAMPUS YA ZANZIBAR

Katika ufunguzi huo Ndg. Makamo Mwenyekiti alipongeza matayarisho na maandalizi mazuri ya mkutano huo.

Ndg. Makamo Mwenyekiti pia alisistiza na kutilia mkazo katika kujipanga vizuri katika kuhakikisha UANDIKISHAJI wa daftari la kudumu la mpiga kura litakaloanza karibuni tu hapa Zanzibar na kuutaka Uongozi wa Jimbo la BUBUBU kuhamasisha vijana kuweza kujiandikisha dftari hilo.

Vilevile Ndg. Makamo Mwenyekiti amewataka viongozi kuongeza mashirikiano, umoja na mshik**ano ili kuweza kutimiza malengo ya chama cha MAPINDUZI kupata ushindi wa kishindo katika uchaguzi mkuu wa 2020.

Pia makamo mwenyekiti aliahidi kuwapatia Computer moja kwa ajili ya kisaidia ufanisi wa kazi za chama cha MAPINDUZI katika jimbo la BUBUBU.

Pia amewataka wanaCCM kuweka maslahi ya chama kwanza na kuwataka Uongozi wa CCM na UVCCM Wilaya ya Mfenesini kukagua uongozi mzima kwa ngazi za chini ili kuendeleza ufanisi wa kazi za chama na jumuiya zake.

Pia makamo mwenyekiti aliendeleza kukumbusha katazo la MAKAMO MWENYEKITI WA CCM ZANZIBAR la kutokuwepo kwa makundi na kuzidisha umoja na mshik**ano.

Mkutano huo pia ukihudhuriwa na VIONGOZI mbalimbali wakiwemo MBUNGE wa Jimbo la BUBUBU na wa jimbo la Mfenesini, Mwakilishi wa Jimbo la BUBUBU na viti maalumu, mjumbe wa Halmashauri kuu ya taifa, Mwenyekiti wa UVCCM mkoa wa Magharibi, mwenyekiti wa wilaya ya Mfenesini, na wengine kwa ngazi zao.

KULINDA NA KUJENGA UJAMAA.

Imetolewa na;
Kitengo Cha Mawasiliano.
Afisi kuu - UVCCM Zanzibar.

RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Dk. Ali Mohamed Shein amerejea nchini leo akitokea Nchi za Umoja ...
29/09/2019

RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Dk. Ali Mohamed Shein amerejea nchini leo akitokea Nchi za Umoja wa Falme za Kiarabu (UAE) ambapo alifanya ziara nchini Ras Al Khaimah pamoja na Abudhabi ikiwa ni muwaliko wa kiongozi wa Ras Al Khaimah Sheikh Saud Bin Saqr Al Qasimi kwa ziara ya wiki moja.

Ziara hiyo ya Rais Dk. Shein ilianza tarehe 23 na kumaliza jana tarehe 28 Septemba mwaka huu 2019 ambapo katika ziara hiyo, alipata fursa ya kuzungumza na mwenyeji wake Mtawala wa Ras-Al-Khaimah Sheikh Saud Bin Saqr Al Qasimi pamoja na kuzungumza na Sheikh Mohammed bin Zayed Al Nahyan, Mrithi wa Mtawala wa Abu Dhabi na Naibu Amiri Jeshi Mkuu wa Vikosi vya Ulinzi wa Nchi za Umoja wa Falme za Kiarabu (UAE)

Katika uwanja wa ndege wa Kimataifa wa Abeid Amani Karume Rais Dk. Shein alipokewa na viongozi mbali mbali wa vyama vya siasa na Serikali pamaaoja na viongozi wa Vikosi vya Ulinzi na Usalama wakiongozwa na Makamo wa Pili wa Rais wa Zanzibar, Balozi Seif Ali Idd.

Mara baada kuwasili kiwanjani hapo, Rais Dk. Shein alifanya mazungumzo na Waandishi wa habari wa vyombo mbali mbali vikiwemo vya Serikali na binafsi ambapo katika maelezo yake alieleza mafanikio makubwa ya ziara hiyo ikiwa ni pamoja na mapokezi mazuri aliyoyapata yeye na ujumbe wake aliofuatana nao.

Aidha, Rais Dk. Shein alieleza hatua zilizofikiwa na Kampuni ya Mafuta ya “RAK GAS” inayojishughulisha na utafiti wa mafuta na gesi asilia hapa Zanzibar na kusisitiza kuwa kazi iliyofikiwa ni nzuri na kila hatua itakayofikia wananchi wataelezwa.

Rais Dk. Shein aliwataka wananchi wasihadaiwe na wale wanaopenda kusema kuwa Rais amefunja sharia na katiba na kusisitiza kuwa suala la mafuta na gesi liko vizuri wala hakuna Sheria wala Katiba iliyovunjwa.

Rais Dk. Shein pia, alieleza namna ya Kiongozi wa Abudhabi Sheikh Mohammed bin Zayed Al Nahyan alivyomuhakikishia kuwa yuko tayari kuiunga mkono Zanzibar katika kutafuta nishati mbadala ambayo kwa upande wa Zanzibar nishati hiyo inatazamiwa kuwa itakuwa nishati ya jua.

Alieleza kuwa tayari Zanzibar kazi imeshaanza kufanywa katika kuhakikisha nishati mbadala ya jua ndio kipaumbele ambapo kwa mashirikiano ya Shirika la Maendeleo la Umoja wa Mataifa (UNDP) pamoja na Umoja wa Ulaya (EU).

Pamoja na hayo, Rais Dk. Shein alieleza kuwa tayari kuna wawekezaji ambao wako tayari kuja kuekeza katika umeme wa jua ambapo kwa upande wa Serikali imo katika kuandaa mipango madhubuti.

Rais Dk. Shein alieleza hatua zinazochukuliwa na Serikali ikiwa ni pamoja na kutoa fedha zake wenyewe kwa ajili ya uendeleza wa ujenzi wa jengo jipya la abiria la uwanja wa ndege huku akieleza hatua za ujenzi wa bandari mpya ya Mpigaduri ambayo alieleza azma ya Serikali kuanza ujenzi japo wa awali kabda hajamaliza muda wake.

Alieleza kuwa tayari fedha za Mkopo kutoka Benki ya Exim ya Indonesia umepatikana sambamba na ujenzi wa bandari ya mafuta na gesi huko Mangapwani ambao unatarajiwa kuanza hivi karibuni.

Kwa upande wa msaada wa fedha Bilioni 23 zilizotolewa na Mfuko wa Khalifa Fund, Rais Dk. Shein alisema kuwa mbali ya fedha hizo pia, Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar kwa upande wake itatoa fedha k**a hizo na kufikia Bilioni 46 kwa ajili ya kuwawezesha vijana wakiwemo wajisiriamali na wanawake
Alisisitiza azma ya Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar kuweka mazingira mazuri kwa ajili ya wafanyabiashara ikiwa ni pamoja na kuimarisha uhusiano na ushsirikiano kati ya wafanyabiashara wa Zanzibar na wale wa Nchi za Umoja wa Falme za Kiarabu (UAE).

Akiwa UAE, Rais Dk. Shein alikutana na viongozi mbali mbali wakiwemo wa Kampuni ya Kimataifa ya Utafiti na Uchimbaji wa Mafuta na gesi asilia ya Ras Al Khaimah “Rak Gas”, Kampuni ya RAKEZ, Kampuni ya Mji wa Bahari wa Ras Al Khaiman, Mamlaka ya Uendelezaji Utalii ya Ras Al Khaimah, uongozi wa Taasisi ya Sera na Utafiti ya Kiongozi wa Ras Al Khaiman.

Kiongozi wa Ras Al Khaimah Sheikh Sheikh Saud Bin Saqr Al Qasimi alimuandalia Rais Dk. Shein dhifa maalum ya kitaifa ya chakula cha mchana mara baada ya mazungumzo yao huko nyumbani kwake mnamo Septemba 23 pamoja na kumuandalia dhifa maaluma ya kitaifa ya chakula la usiku huko katika hoteli ya Kimataifa ya “The ritz Carlton” katika jangwa la Wadi ya hifadhi ya asili iliyopo nje kidogo ya mji wa Ras Al Khaimah

Rais Dk. Shein akiwa Ras Al Khaimah atatembelea maeneo ya mji wa Ras Al Khaiman ikiwa ni pamoja na maeneo mengine ya kitalii katika mji huo na eneo la kiwanda cha Kampuni ya Kimataifa ya Utafiti na Uchimbaji wa Mafuta na gesi asilia ya Ras Al Khaimah.

Aidha, Dk. Shein atakwenda Abu Dhabi kwa ajili ya kushuhudia utiaji wa saini Mkataba wa Mashirikiano kati ya Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar na Serikali ya UAE kupitia Mfuko wa ‘Khalifa Fund’ kwa ajili ya kwuasaidia vijana.

Katika ziara hiyo, Dk. Shein amefuatana na viongozi mbali mbali akiwemo Mke wa Rais wa Zanzibar Mama Mwanamwema Shein, Waziri wa Ofisi ya Rais na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Issa Ussi Haji Gavu, Waziri wa Fedha na Mipango Balozi Mohamed Ramia Abdiwawa, Waziri wa Ardhi, Maji, Nishati na Mazingira Salama Aboud Talib.

Wengine ni Mwanasheria Mkuu wa Serikali Said Hassan Said, Balozi Mohamed Haji Hamza Kaimu Mkurugenzi Idara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki kwa upande wa Zanzibar pamoja na watendaji wengine wa Serikali.

SERIKALI ya Mapinduzi ya Zanzibar na Serikali ya Umoja wa Falme za Kiarabu (UAE) kupitia Mfuko wa Maendeleo wa Abudhabi ...
27/09/2019

SERIKALI ya Mapinduzi ya Zanzibar na Serikali ya Umoja wa Falme za Kiarabu (UAE) kupitia Mfuko wa Maendeleo wa Abudhabi zimetiliana saini Mkataba wa Makubaliano (MOU) juu ya ujenzi na matengenezo ya Hospitali ya Wete Pemba.

Makubaliano hayo yataipelekea Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar kupata Dola za Kimarekani Milioni 10 sawa na Shilingi za Kitanzani Bilioni 23 kupitia Mfuko huo ambazo zitasaidia katika ujenzi na matengenezo makubwa ya Hospitali hiyo ikiwewa ni pamoja na upanuzi wake.

Hafla hiyo ya utiliaji saini imefanyika katika ofisi ya Mfuko wa Maendeleo wa Abudhabi mjini Abudhabi ambapo kwa upande wa Zanzibar Waziri wa Fedha na Mipango Balozi Mohamed Ramia Abdiwawa alisaini kwa niaba ya Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar na Mkurugenzi Mkuu wa Mfuko wa Maendeleo wa Abudhabi Mohammed Saif Al Suwaid alisaini kwa niaba ya Serikali ya (UAE).

Mara baada ya utiliaji saini wa Mkataba huo Waziri Abdiwawa alieleza kuwa, fedha hizo zitasaidia kwa kiasi kikubwa katika kuimarisha sekta ya afya Zanzibar.

Alieleza kuwa kwa niaba ya Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar na wananchi wake wote wanatoa pongezi na shukurani za dhati kwa Umoja wa Nchi za Falme za Kiarabu (UAE) kwa juhudi zake za kuendelea kuiunga mkono Zanzibar katika kuimarisha sekta ya afya.

Balozi Ramia aliongeza kuwa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar inathamini sana juhudi hizo ambazo zimekuwa chachu katika kuimarisha uhusiano na ushirikiano wa kihistoria uliopo baina ya pande mbili hizo.

Aidha, Balozi Ramia alitumia fursa hiyo kutoa shukurani za pekee kwa Sheikh Khalifa Bin Zayed Al Nahyan Rais wa Nchi za Umoja huo kwa msaada wake huo na kueleza kuwa hatua hiyo inatoa taswira nzuri ya mashirikiano yaliopo kati ya viongozi wa umoja huo na viongozi wa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar pamoja na wananchi wao.

Nae Mkurugenzi Mkuu wa Mfuko wa Maendeleo wa Abudhabi, Mohammed Saif Al Suwaid alieleza kuwa Mfuko huo unajivunia kupata fursa hiyo na kusisitiza kuwa Serikali ya Umoja wa Nchi za Falme za Kiarabu utaendelea kuinga mkono Zanzibar.

Alieleza kuwa mradi wa ujenzi na matengenezo ya Hospitali ya Wete ni mradi mkubwa kwani unawagusa moja kwa moja wananchi hivyo, aliipongeza Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar chini ya uongozi wa Rais Dk. Shein kwa kuweka kipaumbele hicho hasa ikizingatiwa kuwa mradi huo ni muhimu katika maisha ya wananchi.

Sambamba na hayo, Al Suwaid alieleza kuwa Mfuko wa Maendeleo wa Abudhabi utachukua juhudi na ari za makusudi katika kahakikisha mradi huo unafanikiwa na unatekelezwa kwa muda uliopangwa.

Fedha hizo zilizotolewa na Serikali ya Umoja wa Nchi za Falme za Kiarabu (UAE) kupitia Mfuko wa Maendeleo wa Abudhabi zinatokana na agizo maalum la Rais wa Umoja wa nchi hizo Sheikh Khalifa Bin Zayed Al Nahyan katika kuhakikisha Serikali anayoiongoza inaiunga mkono Zanzibar katika kuimarisha sekta ya afya.
Katika hafla hiyo baadhi ya viongozi wa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar walishuhudia tukio hilo akiwemo Waziri Ofisi ya Rais na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Issa Ussi Haji Gavu, Waziri wa Ardhi, Maji, Nishati na Mazingira Salama Aboud Talib, Mwanasheria Mkuu wa Serikali Said Hassan Said pamoja na Balozi wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania katika Nchi za Umoja wa Falme za Kiarabu (UAE) Mbarouk Omar Mbarouk.
Hatua hiyo ni matunda ya ziara ya Rais Dk. Shein aliyoifanya katika nchi za Umoja wa Falme za Kiarabu (UAE) mnamo mwezi Januari mwaka 2018 kufuatia mwaliko wa Sheikh Mohammed bin Zayed Al Nahyan, Mrithi wa Mtawala wa Abu Dhabi na Naibu Amiri Jeshi Mkuu wa Vikosi vya Ulinzi wa Nchi za Umoja wa Falme za Kiarabu (UAE).

Katika kuhakikisha mazungumzo ya viongozi hao na makubaliano yao yanafanyiwa kazi mnamo mwezi wa Agosti mwaka 2018, Ujumbe wa timu ya Wataalamu kutoka Serikali ya Nchi za Umoja wa Falme za Kiarabu (UAE) ulikuja Zanzibar na kufanya ziara ya kutembelea maeneo mbali mbali ya Zanzibar ukiongozwa na Mshauri wa Waziri wa Nchi Ushirikiano wa Kimataifa wa Serikali ya Nchi za Falme za Kiarabu Bi Najla Al Kaabi.

Ujumbe huo ulifanya ziara ya siku moja katika Kisiwa cha Pemba na kutembelea barabara ya Chake Chake hadi Mkoani, Hospitali ya Abdalla Mzee, Bandari ya Mkoani, Hospitali ya Wete, Bandari ya Wete, pamoja na kutembelea kikundi cha Wajasiriamali cha Upendo cha mjini Wete.

RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk. Ali Mohamed Shein ameeleza kuwa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzi...
26/09/2019

RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk. Ali Mohamed Shein ameeleza kuwa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar iko tayari kushirikiana na Serikali ya Ras Al Khaimah katika kuanzisha programu ya mafunzo kwa walimu wa Zanzibar.

Rais Dk. Shein aliyasema hayo leo wakati alipokutana na ujumbe wa Taasisi ya Sera na Utafiti ya Sheikh Saud Bin Saqri Al Qasimi huko katika ukumbi wa Hoteli ya Waldorf Astoria iliyopo mjini Ras Al Khaimah.

Ujumbe huo umekuja kufuatia agizo la Mtawala wa nchi hiyo alilolitoa kwa Msaidizi wake wa masuala ya elimu siku ambayo Mtawala huyo alikutana na kufanya mazungumzo na Rais Dk. Shein katika ukumbi wa Kasri yake iliyopo Aldhait mjini Ras Al Khaimah.

Rais Dk. Shein alitoa shukurani zake kwa kiongozi wa Rais Al Khaimah Sheikh Saud Bin Saqr Al Qasimi kwa kulichukulia hatua ya haraka suala hilo na kupelekea kukutana na ujumbe wa viongozi wa Taasisi yake inayoshughulikia masuala hayo wakati bado yupo hapa hapa nchini Ras Al Khaimah.

Aidha, Rais Dk. Shein alipongeza juhudi za kiongozi huyo anazozichukua katika kuiunga mkono Zanzibar na jinsi alivyolipa kipaumbe suala la kuimarisha sekta ya elimu kwa kuanzisha programu maalum ya mafunzo ya Walimu hatua itakayoimarisha ubora wa elimu kupitia mafunzo hayo ya Uwalimu kwa Walimu wa Zanzibar.

Katika mazungumzo hayo, Rais Dk. Shein aliualika uongozi wa Taasisi hiyo kuja Zanzibar kwa lengo la kukutana na uongozi wa Wizara ya Elimu pamoja na uongozi wa Chuo Kikuu cha Taifa cha Zanzibar (SUZA) ili kuona jinsi gani wanaweza kushirikiana katika kutoa mafunzo ya kuwajengea uwezo walimu wa Zanzibar.

Rais Dk. Shein alieleza kuwa hatua hiyo itaiwezesha Wizara ya Elimu kutoa vipaumbele vya mahitaji waliyonayo ili iwe rahisi kutekeleza programu hiyo jambo ambalo litaisaidi Taasisi hiyo kutambua vipaumbe vya Zanzibar na hatimae kurahisisha utekelezaji wa programu hiyo.

Nae Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi hiyo ya Sera na Utafiti ya Sheikh Saud Bin Saqr Al Qasimi Natasha Ridge, alieleza kuwa Taasisi hiyo pia, inajishughulisha na utoaji wa mafunzo ya kitaalamu ya kuwajengea uwezo walimu kuanzia ngazi ya Msingi hadi Sekondari.

Aliongeza kuwa hatua hiyo ni kwa lengo la kutoa mafunzo bora kwa wanafunzi ambayo yatawasaidia katika kumudu masomo yao ya ngazi za juu hususan katika Vyuo Vikuu popote watakapokwenda kusoma.

Alieleza kuwa mafunzo hayo ni kwa ajili ya kuwajengea uwezo walimu wa Msingi na Sekondari ili waweze kuwatayarisha vizuri wanafunzi wao wanaopoingia katika ngazi za juu za masomo hasa Vyuo Vikuu vya ndani na nje ya nchi yao.

Vile vile, Mkurugenzi huyo alimueleza Rais Dk. Shein kuwa katika programu zao wana mafunzo ya kufundisha njia bora za uongozi katika masuala ya elimu na kusisitiza kuwa hatua hiyo itasaidia kwa kiasi kikubwa kuimarisha sekta ya elimu Zanzibar.

Aidha, alisema kuwa katika utaratibu wao wa kutoa mafunzo huwa wanatoa mafunzo kwa Wakufunzi ambao na wao wataweza kuwafundisha walimu wengine ili ujuzi huo usambae kwa walimu wengi zaidi.

Sambamba na hayo, Mkurugenzi Mtendaji huyo alimueleza Rais Dk. Shein kuwa wako uongozi wa Taasisi hiyo uko tayari kuja Zanzibar mnamo mwezi wa Novemba mwaka huu kwa ajili ya kukutana na uongozi wa Wizara ya Elimu pamoja na uongozi wa Chuo Kikuu cha Taifa cha Zanzibar (SUZA) ili kuangalia vipaumbelea ambavyo wao wataweza kuvifanyia kazi katika kutoa mafunzo hayo.

RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk. Ali Mohamed Shein ametembelea kiwanda cha Kampuni ya Kimataifa...
25/09/2019

RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk. Ali Mohamed Shein ametembelea kiwanda cha Kampuni ya Kimataifa ya Utafiti na Uchimbaji wa Mafuta na Gesi Asilia ya Ras Al Khaimah “RAK GAS” iliyopo nje kidogo ya mji wa Ras Al Khaimah na kujionea shughuli za kiwanda hicho.

Katika kiwanda hicho ambacho kimekuwa kikifanya shughuli mbali mbali za kupokea gesi kutoka katika maeneo maalum ya uchimbaji, kuisambaza sambamba na kuihifadhi kwa lengo la kuweza kuitumia.

Akiwa na ujumbe wake, Dk. Shein alipata maelezo kutoka kwa viongozi wa Kampuni hiyo ya Kimataifa ya Utafiti na Uchimbaji wa Mafuta na Gesi Asilia ya Ras Al Khaimah “RAG GAS” akiwemo Meneja Mkuu Peter Deibel, Msaidizi Meneja Mwendeshaji Jody Labbie na Mwangalizi Mkuu wa Uzalishaji Deepu Thomas ambaye alitoa ufafanuzi juu ya uzalishaji pamoja na usambazaji wa gesi asilia kiwandani hapo.

Rais Dk. Shein alieleza kuvutiwa na shughuli mbali mbali zinazofanywa na kiwanda hicho katika eneo hilo lililopo nje kidogo ya mji wa Ras Al Khaimah ambalo ni muhimu katika shughuli za gesi asilia ambayo imekuwa na mchango mkubwa katika maendeleo ya Ras Al Khaimah.

Alipongeza hatua kubwa za maendeleo pamoja na mchango mkubwa wa mradi huo wa gesi kwa uchumi na maendeleo ya Ras Al Khaimah unatokana na mikakati madhubuti iliyowekwa katika kuhakikisha juhudi hizo zinachangia na kuendeleza soko la ajira, ukuaji wa uchumi na maendeleo ya viwanda katika nchi hiyo.

Viongozi hao wa kiwanda hicho cha Kampuni ya “RAG GAS” walimueleza Rais Dk. Shein shughuli mbali mbali zinazofanywa katika eneo hilo la kiwanda cha gesi na kutoa maelezo yanayohusiana na usafirishwaji kutoka maeneo inayozalishwa gesi hiyo hadi kiwandani hapo.

Aidha, walimueleza Rais Dk. Shein hatua na njia zinazotumika kusafirisha gesi hiyo asilia kutoka kiwandani hapo hadi katika maeneo inayotumika ambapo kwa maelezo ya viongozi hao wakuu Kampuni ya “RAG GAS”, gesi hiyo imekuwa na mchango mkubwa wa uchumi wa Ras Al Khaimah.

Viongozi hao walimueleza Rais Dk. Shein pamoja na ujumbe wake kuwa gesi hiyo imekuwa ikisaidia kwa kiasi kikubwa katika matumizi ya ndani ya nchi na nje ya Ras Al Khaimah sambamba na kuhangia katika kuimarisha viwanda vikiwemo viwanda vya saruji pamoja na viwanda vya vifaa vya ujenzi.

Kwa maelezo ya viongozi wa Kampuni hiyo ya “RAG GAS”, Ras Al Khaimah imekuwa ikichangia sana katika sekta ya ujenzi kwa nchi za Umoja wa Falme za Kiarabu (UAE) kutokana na rasilimali mbali mbali zinazozalishwa nchini humo.

Walieleza kuwa rasilimali hizo zimeweza kuendeleza viwanda na kukuza uchumi mchanganyiko, kukuza soko la ajira pamoja na kuongeza thamani ya bidhaa mbali mbali zinazozalishwa nchini humo ambazo zina ubora mkubwa na zimekuwa maarufu sana duniani.

Mapema katika ukumbi wa Hoteli ya Waldorf Astoria mjini Ras Al Khaimah, Rais Dk. Shein akiwa na viongozi wa ujumbe aliofuatana nao walikutana na viongozi wa ngazi za juu wa Kampuni ya “RAS GAS” na kumpa taarifa juu ya hatua zilizofikiwa katika utafiti wa mafuta na gesi asilia unaofanywa Zanzibar.

Katika utoaji wa taarifa hiyo, viongozi hao wakiongozwa na Afisa Mtendaji Mkuu wa Kampuni ya “RAG GAS” Nishant Dighe pamoja na viongozi wa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar wote kwa pamoja walisisitiza haja ya kuendeleza zaidi ushirikiano katika shughuli hiyo ya utafiti, uendelezaji na uchimbaji wa mafuta na gesi asilia Zanzibar.

Sambamba na hayo viongozi wa Kampuni hiyo walitoa pongezi kwa viongozi wa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar pamoja na wananchi wake kwa mashirikiano makubwa wanayoyapata hatua ambayo inarahisisha zaidi utekelezaji wa utafiti huo.

Nao viongozi wa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar kwa upande wao waliahidi kuendeleza ushirikiano uliopo kati yake na Kampuni hiyo kwa lengo la kufikia mipango na mikakati iliyowekwa yenye tija kwa pande mbili hizo na kuipongeza Kampuni hiyo kwa mashirikiano hayo makubwa inayoonesha kwa Serikali.

Makamu wa Rais Samia Suluhu Hassan amekitaka Chuo Kikuu Huria chaTanzania (OUT), kuwaandaa Wanafunzi kimkakati kushiriki...
24/09/2019

Makamu wa Rais Samia Suluhu Hassan amekitaka Chuo Kikuu Huria cha
Tanzania (OUT), kuwaandaa Wanafunzi kimkakati kushiriki moja kwa moja katika
uchumi wa Viwanda pindi wanapohitimu masomo yao.

Makamu wa Rais ameeleza hayo jijini Dar es salaam, katika kilele cha
maadhimisho ya miaka 25 tangu kuanzishwa kwa Chuo Kikuu hicho Huria cha Tanzania.

Amefafanua kuwa, lengo la Serikali katika ujenzi wa uchumi wa Viwanda, ni kuleta
maendeleo jumuishi na endelevu kwa kutumia rasilimali zinazopatikana
nchini na kuongeza ajira.

Amesema Serikali inatambua umuhimu wa Sekta ya Elimu kwa maendeleo ya uchumi wa Viwanda, ndio maana inaendelea kuondoa changamoto kadhaa zinazoikabili sekta hiyo zikiwemo zile za Chuo Kikuu hicho.

Kwa upande wake, Mkuu wa Chuo Kikuu Huria cha Tanzania, Waziri Mkuu Mstaafu Mizengo Pinda amesema kuwa, chuo hicho kimekua kikitoa Wahitimu wenye mchango mkubwa kwa maendeleo ya Taifa.

Chuo Kikuu Huria cha Tanzania, ndio Chuo Kikuu Huria pekee katika
ukanda wa Afrika Mashariki.

Kilianzishwa mwaka 1994 kikiwa na Wanafunzi Wanane, lakini kwa sasa maelfu ya Wanafunzi wamekua wakihitimu kila mwaka.

Address

Mwera
Zanzibar

Website

Alerts

Be the first to know and let us send you an email when UVCCM Mkoa wa Magharibi posts news and promotions. Your email address will not be used for any other purpose, and you can unsubscribe at any time.

Contact The Organization

Send a message to UVCCM Mkoa wa Magharibi:

Share