Zanzibar Municipal Council

Zanzibar Municipal Council Baraza la manispaa Zanzibar, ni taasisi ya serikali iliyopo chini ya sheria namba 3 ya mwaka 1995 ya baraza la wawakilishi la Zanzibar

22/05/2015

BARAZA LA MANISPAA LINAWATANGAZIA WAFANYABIASHARA WOTE KULIPIA HUDUMA ZA USAFI (SERVICE CHARGE ) ZA MADUKA KATIKA MAENEO YAO YA BIASHARA PAMOJA NA KUZIHIFADHI RISITI HIZO NA KUZIWEKA MADUKANI KWAO, KWANI KUTAKUWA NA UKAGUZI WA KUSHTUKIZA MARA KWA MARA, HATUA KALI ZITACHUKULIWA KWA WALE WOTE AMBAO WATAKIUKA TAARIFA HII IKIWEMO KULIPA FAINI YA ASILIMIA 20% YA KODI AMBAYO HUTOZWA, AU KIFUNGO KISICHOZIDI MIEZI SITA.

21/05/2015

KATIKA KUWASHIRIKISHA WANANCHI KATIKA KUWAPA HABARI JUU YA HUDUMA AMBAZO HUFANYWA NA BARAZA LA MANISPAA, SASA LIMEAMUA KUANZISHA KIPINDI AMBACHO KINAENDESHWA NA ZANZIBAR CABLE TELEVISION KWA KUSHIRIKIANA NA BARAZA LA MANISPAA AMBACHO HURUSHWA KILA SIKU YA JUMATATU SAA 3;00 KAMILI USIKU, KIPINDI HIKI HUA KINAELEZEA SHUGHULI MBALI MBALI NZINAZOFANYWA NA BARAZA LA MANISPAA NA HATIMAE KUPEWA NAFASI YA KUULIZA NA KUCHANGIA MAWAZO KWA KUPIGA SIMU.....NYOTE MNAKARIBISHWA KUTOWA MAWAZO YENU ......AHSANTENI SANA ....

21/05/2015

Wakufunzi pamoja na Wataalamu kutoka Baraza La Manispaa, Wizara ya Tawala za Mikoa na Halmashauri ya Magharibi wanategemea kushirkiana na Wananchi wa Shehiya ya Miembeni katika kutumia mbinu za ushirikishwa Wananchi katika kuibua vipaumbele na Changamoto ambazo zinawakabili na kuzitafutia Ufumbuzi kwa miniajili ya kuleta maendeleo kutokea ngazi za Shehiya hadi Taifa.

20/05/2015

BARAZA LA MANISPAA BADO LINAWAKUMBUSHA WANANCHI WOTE KWA JUMLA, JUU YA KUTUNZA MAZINGIRA YETU KUWA SAFI NA KUTUPA TAKA MAJAANI ASUBUHI MAPEMA KATIKA KIPINDI HIKI CHA MVUA INGAWA ZINAONEKANA ZIMEZUIA KIDOGO KWA SASA, PIA KULIPIA LESENI NA ADA NYENGINE KWANI HIZO NDIO CHACHU YA KUENDESHA SHUGHULI ZA KILA SIKU NDANI YA BARAZA LA MANISPAA

18/05/2015

Watendaji kutoka Baraza la Manispaa, Wizara ya Tawala za Mikoa, Afisi ya Rais na Halmashauri ya Magharibi Wamekuwa Wakipata Mafunzo ya Mpango shirikishi kwa Wanachi kutokea ngazi za chini (Shehiya) kwa kuweza kuwafikia na kupata Maoni yao juu ya huduma ambazo huzipata kutoka katika Taasisi mbali mbali za Serikali na kuzifanyia kazi ipasavyo kwa Maendeleo ya Nchi yetu ya Zanzibar. Mafunzo hayo yanawasilishwa na Andrew M. Komba kutoka Chuo Kikuu Dodoma na Henrry Mgingi kutoka Tume ya Mipango ya Taifa ya Tanzania Mafunzo ambayo yatachukua siu (5) katika Ukumbi wa Bima Mpirani Madema kuanzia siku ya Jumatatu tarehe18/5 hadi ijumaa tarehe 22/5/2015

15/05/2015

BARAZA LA MANISPAA LINAWATAKIA IJUMAA NJEMA YENYE MAFANIKIO MAKUBWA KATIKA MAISHA NA KUWAOMBEA MAPUMZIKO YA FURAHA NA FAMILIA KATIKA SIKU ZA MWISHO WA WIKI PAMOJA NA KUWAKUMBUSHA JUU YA SUALA ZIMA LA KUTUNZA MAZINGIRA YETU NA KUTUPA TAKA ASUBUHI MAPEMA ILI KUWARAHISISHIA WACHUKUAJI WA TAKA HIZO KUONDOKANA NA USUMBUFU USIO WA LAZIMA

14/05/2015

BARAZA LA MANISPAA LINAWAOMBA WAFANYABIASHARA WOTE AMBAO WALILIPIA LESENI ZAO BARAZA LA MANISPAA, KUFIKA BARAZA LA MANISPAA AMANI, KUCHUKUA LESENI ZAO KWANI KUANZIA SIKU YA JUMATATU TAREHE 18/5/2015 KUTAKUA NA ZOEZI MAALUM LA KUKAGUA MADUKA, VIOSKI, MIKAHAWA N.K, PIA BARAZA LA MANISPAA LINAWATAKA WAFANYABIASHARA KUTOWA MASHIIKIANO YAO YA DHATI KWA MAAFISA WA BARAZA LA MANISPAA AMBAO WATAPITA KWA UKAGUZI

08/05/2015

BARAZA LA MANISPAA LINASIKITIKA KUTANGAZA KIFO CHA MFANYAKAZI WAKE AMINA JOHNAS CHANDE KILICHOTOKEA SIKU YA ALHAMIS TAREHE 7/5/2015, KIBOJE NA KUZIKWA LEO IJUMAA SAA 7:30 BAADA YA SALA YA IJUMAA KIBOJE, BARAZA LINAUNGANA NA NDUGU , JAMAA NA MARAFIKI KATIKA KUMTAKIA MALAZI BORA PEPONI. AMIN.............

07/05/2015

BARAZA LA MANISPAA LINAWATAKA WANANCHI WOTE KUTUNZA MAZINGIRA AMBAYO YANAWAZUNGUKA KWA KUYASAFISHA NA KUTOMWAGA TAKA OVYO, KUTOWAACHA WATOTO WAKICHEZEA MAJI MACHAFU, KUCHEMSHA MAJI YA KUNYWA, KUTOTAPISHA MAKARO YA MAJI MACHAFU NA KUYAMWAGA MITAANI, KUTUMIA VYOO N.K KUFANYA HIVI KUTATASAIDIA KUEPUKA MARADHI YA MIRIPUKO NA MATUMBO

06/05/2015

Watendaji wa Baraza la Manispaa, Halmashauri na kutoka Wizara ya Tawala za Mikoa wamekuwa wakipata mafunzo ya UWANDIKAJI PAMOJA NA UWASILISHAJI WA MIRADI inayotolewa na Wakufunzi kutoka TUME YA MIPANGO, Semina ambayo inachukuwa siku mbili tarehe 5-6/5/2015. ambapo inalenga hasa katika;
kutengeneza WAZO KUU LA MRADI, UWASILISHAJI WAKE HADI KUFIKIA KUKAMILIKA KWA MRADI Ukijumuisha na Changamoto zinazoweza kujitokeza.kipindi cha Mradi unapotekelezwa.

05/05/2015

TUKIWA BADO TUNAENDELEA NA KUPATA MVUA ZA MASIKA, BARAZA LA MANISPAA LINAWAPA POLE WALE WOTE AMBAO WAMEATHIRIKA KWA NAMNA MOJA AU NYENGINE NA KUWAOMBA KUWA PAMOJA BARAZA KATIKA KUHAKIKISHA MAZINGIRA YETU YANAKUWA KATIKA HALI YA USAFI NA SALAMA ILI KUEPUSHA ATHARI ZAIDI ZISITOKEE AHSANTENI.

23/04/2015

BARAZA LA MNISPAA LINAWAKUMBUSHA WANANCHI WOTE KUCHUKUA TAHADHARI KATIKA KIPINDI HIKI CHA MVUA KWA ;
KUACHA KUTUPA TAKA OVYO, NA WANATAKIWA WAZITIE KATIKA MAKONTENA YA TAKA.
KUACHA KUUZA BIASHARA ZA VYAKULA ZISIZOFUNIKWA AU KATIKA MAZINGIRA MACHAFU.
KUTOTUPA TAKA KATIKA MITARO YA MAJI YA MVUA.
KUTOWARUHUSU WATOTO WADOGO KUCHEZEA MAJI MACHAFU.
KUFANYA HAYA NI KUHATARISHA AFYA ZETU.

Address

Creek Road/Darajani
Zanzibar
P.OBOX1288

Opening Hours

Monday 07:30 - 15:30
Tuesday 07:30 - 15:30
Wednesday 07:30 - 15:30
Thursday 07:30 - 15:30
Friday 07:30 - 15:30

Telephone

+255242231330

Website

Alerts

Be the first to know and let us send you an email when Zanzibar Municipal Council posts news and promotions. Your email address will not be used for any other purpose, and you can unsubscribe at any time.

Contact The Organization

Send a message to Zanzibar Municipal Council:

Share