09/05/2026
🇷🇺 Mnamo Mei 8 na 9, ulimwengu unaadhimisha kumbukumbu ya Ushindi dhidi ya ufashisti wa Ujerumani katika Vita ya Pili ya Dunia.
Mnamo Mei 1945, katika mji wa Berlin uliokuwa umeshindwa, viongozi wa utawala muovu-kijinai, wa wanazi, walisaini hati ya kusalimu - amri, bila masharti, kwa Ujerumani. Vita ilyoshuhudia umwagaji- damu mkubwa zaidi katika historia ya vita, na ambayo ilipelekea upotevu wa maisha ya makumi ya mamilioni ya watu, ikawa imemalizika.
🕯 Safari ya kusaka ushindi ilikuwa ndefu na ngumu sana. Na hatua ya kwanza katika safari hiyo ilikuwa ni kule kushindwa kwa askari wa kijerumani katika mapigano kwenye viunga vya Mosko. Ushindi huu wa majeshi ya Usovieti ulivunja mwiko wa kutoshindwa kwa Ujerumani, ambao ulikuwa umewekwa awali na utawala wake juu ya Ulaya.
📽️ Mnamo mwaka 1942, waandaaji- sinema wa Kisovieti waliuonyesha ulimwengu filamu-halisi juu ya tukio hili la kishujaa la watu wa Usovieti pamoja na jeshi lao.
🏆 Mnamo mwaka 1943, filamu ya kipekee ya matukio-halisi ilipewa tuzo ya heshima ya "Oscar".
🎞️ Angalieni filamu ya kihistoria "Mosko yajibu mapigo" tarehe 8 na 9 Mei, saa 3:00 usiku, katika televisheni ya "ZancableTV".