Zanzibar Business And Property Registration Agency -BPRA

Zanzibar Business And Property Registration Agency -BPRA Karibu katika ukurasa wetu, Wakala wa Usajili wa Biashara na mali (BPRA).

Katika ukurasa huu utapata taarifa kuhusu huduma zinazotolewa na BPRA, njia za mawasiliano, mitandao yetu ya kijamii, taarifa na matukio mbalimbali yanayotokea katika Taasisi hii, Lengo ni kuhakikisha kuwa taarifa zote muhimu zinazohitajika zinapatikana katika ukurasa huu ili kukuwezesha kuwa na uelewa mpana wa majukumu na huduma zitolewazo na BPRA. Majukumu ya BPRA ni pamoja na kusajili Makampuni

, Majina ya Biashara, Alama za Biashara,Nyaraka na Kusimami mirathi kwa wasio kuwa waislamu, BPRA Ipo tayari ya kusikiliza na kutoa huduma bora ili kufanikisha lengo.

BPRA Yatoa Elimu ya Usimamizi wa Mirathi kwa Wasiokuwa WaislamuOfisi ya Wakala wa Usajili wa Biashara na Mali Pemba (BPR...
16/08/2026

BPRA Yatoa Elimu ya Usimamizi wa Mirathi kwa Wasiokuwa Waislamu

Ofisi ya Wakala wa Usajili wa Biashara na Mali Pemba (BPRA) imeendelea na ziara za kutoa elimu kwa jamii, ambapo safari hii imetembelea Kanisa la Roman Catholic lililopo Kizimbani, Wete Pemba, kwa lengo la kutoa elimu kuhusu usimamizi wa mirathi kwa wasiokuwa Waislamu pindi mmiliki wa mali anapofariki.

Katika ziara hiyo, Mratibu wa BPRA Pemba, Ndg. Mohammed Ali Maalim, alitoa ufafanuzi kuhusu umuhimu wa kusajili mali na biashara zote zinazomilikiwa, akisisitiza kuwa uwasilishaji wa mirathi ni hatua muhimu katika kulinda haki na umiliki wa mali.

Naye Msaidizi Mrajis Nyaraka BPRA Zanzibar, Ndg. Khamis Haji Bakar, alitoa ufafanuzi kuhusu taratibu zinazofuatwa katika usimamizi wa urithi wa mali kwa wasiokuwa Waislamu. Aidha, aliwataka waumini kufika katika ofisi za BPRA zilizopo Unguja na Pemba ili kuziwasilisha mali zao kwa mujibu wa sheria na taratibu zilizowekwa.

Kwa niaba ya waumini wa Kanisa la Roman Catholic lililopo Wete Pemba, Makamo mwenyekiti wa Parokia kanisa la Roman Catholic Nd. Innocent Selle aliishukuru BPRA kwa kuwafikishia elimu hiyo, akieleza kuwa waumini wengi hawakuwa na uelewa wa kutosha kuhusu taratibu za usimamizi wa mirathi ya mali kwa wasiokuwa Waislamu.

BPRA — Usajili Wetu, Safari ya Mafanikio Yako.

Ofisi ya Wakala wa Usajili wa Biashara na Mali Zanzibar (BPRA), imetembelea Shehia ya Pujini kwa lengo la kuhamasisha wa...
31/07/2026

Ofisi ya Wakala wa Usajili wa Biashara na Mali Zanzibar (BPRA), imetembelea Shehia ya Pujini kwa lengo la kuhamasisha wananchi kuhusu umuhimu wa kusajili mali na biashara wanazomiliki.

Akizungumza na wananchi, Mratibu wa BPRA Pemba, Nd. Mohammed Ali Maalim, aliisisitiza jamii kuhakikisha inasajili mali na biashara zao ili kupata ulinzi wa kisheria na kunufaika na huduma mbalimbali zinazotolewa na Serikali.

Naye Afisa Usajili wa Nyaraka kutoka BPRA Pemba, Nd. Abdulla Ali Abdulla, alitoa ufafanuzi kuhusu taratibu zinazofuatwa katika usajili wa mali, akiwataka wananchi kufuata taratibu sahihi ili kurahisisha upatikanaji wa huduma hizo.

Kwa niaba ya wananchi wa Shehia ya Pujini, Sheha wa Shehia hiyo, Nd. Khamis Uledi Kombo, aliishukuru BPRA kwa kufika na kutoa elimu hiyo muhimu, akieleza kuwa wananchi wengi hawakuwa na uelewa wa kutosha kuhusu huduma za usajili wa mali na biashara, hivyo elimu hiyo imeongeza uelewa na kuwahamasisha kutumia huduma zinazotolewa na BPRA.

Mratibu wa BPRA Pemba, Nd. Mohammed Ali Maalim, amefanya ziara katika benki mbalimbali kwa lengo la kutoa ufafanuzi kuhu...
29/07/2026

Mratibu wa BPRA Pemba, Nd. Mohammed Ali Maalim, amefanya ziara katika benki mbalimbali kwa lengo la kutoa ufafanuzi kuhusu umuhimu wa huduma zinazotolewa na BPRA kwa wafanyabiashara.

Akitembelea matawi ya benki ya NMB, PBZ na CRDB yaliyopo Mkoa wa Kaskazini Pemba , amesisitiza kuwa maafisa wa benki wanapaswa kuhakikisha wafanyabiashara wote wanaofika kuomba huduma za kibenki wamepitia BPRA na kupata uhalali wa nyaraka zao kwa kugongwa Muhuri wa Kijani (Green Seal). Hatua hiyo inasaidia kuthibitisha uhalali wa nyaraka za biashara na kuimarisha uzingatiaji wa sheria na taratibu za usajili.

BPRA inaendelea kushirikiana na taasisi mbalimbali ili kuimarisha mazingira bora ya biashara na kuongeza uelewa kuhusu umuhimu wa usajili na uthibitishaji wa nyaraka za biashara.

25/07/2026
25/07/2026

BPRA yatoa mafunzo kwa Mawakili na Wanasheria ya kuwasaidia na kuwaongoza wateja wao katika kuwatambua na kuwasilisha taarifa za wamiliki manufaa wa Makampuni.

BPRA YATOA ELIMU YA USAJILI WA BIASHARA NA MALI KWA WANANCHI WA SHEHIA YA WAWI.Wakala wa Usajili wa Biashara na Mali Zan...
13/07/2026

BPRA YATOA ELIMU YA USAJILI WA BIASHARA NA MALI KWA WANANCHI WA SHEHIA YA WAWI.

Wakala wa Usajili wa Biashara na Mali Zanzibar (BPRA) umeendelea na juhudi zake za kutoa elimu kwa jamii juu ya uhamasishaji kuhusu umuhimu wa Usajili wa biashara na mali kwa wananchi wa Shehia ya Wawi.

Akizungumza na wananchi, Mratib Wakala wa Usajili biashara na mali Zanzibar, Nd. Mohammed Ali Maalim alieleza umuhimu wa kusajili mali na biashara pamoja na alama za biashara (Trade Mark) kupitia BPRA. Alifafanua kuwa usajili unalinda haki za umiliki, hubainisha uhalali wa biashara, hujenga imani kwa wateja na hufungua fursa mbalimbali za kiuchumi.

Aidha, alionya kuhusu hasara zinazoweza kujitokeza kutokana na kutosajili mali au biashara, ikiwemo migogoro ya umiliki, kupoteza haki za kisheria na kukosa fursa za maendeleo ya biashara.

Kwa upande wake, Afisa Usajili Nyaraka BPRA Nd. Abdalla Ali Abdulla aliwasilisha mada kuhusu aina za Nyaraka zinazopaswa kusajiliwa. Alizitaja nyaraka hizo kuwa ni pamoja na hiba, wasia, mikataba ya amana pamoja na viapo vya umiliki wa nyumba, akisisitiza kuwa Usajili wa Nyaraka hizo unasaidia kulinda haki za wahusika na kurahisisha utatuzi wa migogoro ya Kisheria pale inapojitokeza.

Akihitimisha kikao hicho, Sheha wa Shehia ya Wawi, Nd. Khamisi Issa, aliishukuru BPRA kwa kufika shehiani hapo na kutoa elimu muhimu kwa wananchi. Alieleza kuwa mafunzo hayo yatachangia kuongeza uelewa wa wananchi kuhusu umuhimu wa kusajili biashara na mali zao, jambo litakalosaidia kulinda haki zao na kuchochea maendeleo ya kijamii na kiuchumi.

BPRA imeendelea kuwahimiza wananchi kutumia huduma zake za usajili kwa wakati ili kuhakikisha Mali, biashara na haki zao zinalindwa kwa mujibu wa Sheria, sambamba na kuimarisha mazingira bora ya biashara na uwekezaji Zanzibar.

Imetolewa,
Kitengo Cha Uhusiano.
BPRA

Msaidizi Mrajis kutoka Wakala wa Usajili wa Biashara na Mali (BPRA) Nd. Mustafa A. Haji  akishiriki mjadala  wa fursa za...
13/07/2026

Msaidizi Mrajis kutoka Wakala wa Usajili wa Biashara na Mali (BPRA) Nd. Mustafa A. Haji akishiriki mjadala wa fursa za uwekezaji Micheweni, Pemba katika siku ya Zanzibar Day iliyofanyika katika maonesho ya Biashara ya Sabasaba Jijini Dar es Salaam.

BPRA Yatoa Elimu ya Usajili kwa Wananchi wa Shehia ya MfikiwaMfikiwa, Chake Chake, Pemba – Juni 19, 2026Wakala wa Usajil...
20/06/2026

BPRA Yatoa Elimu ya Usajili kwa Wananchi wa Shehia ya Mfikiwa

Mfikiwa, Chake Chake, Pemba – Juni 19, 2026

Wakala wa Usajili wa Biashara na Mali Zanzibar (BPRA) umeendelea kutoa elimu kwa wananchi kuhusu umuhimu wa usajili wa biashara na nyaraka mbalimbali kupitia kikao cha uhamasishaji kilichofanyika katika Shehia ya Mfikiwa siku ya Ijumaa, tarehe 19 Juni 2026.

Akizungumza katika kikao hicho, Mratib Wakala wa Usajili wa Biashara na Mali Pemba, Nd. Mohammed Ali Maalim, alieleza umuhimu wa usajili wa biashara na Mali zikiwemo nyaraka mbalimbali kwa wananchi. Alisema kuwa usajili husaidia kulinda haki za wamiliki wa mali, kuimarisha shughuli za biashara na kuweka mazingira bora ya maendeleo ya kiuchumi kwa jamii.

Aidha, alisisitiza kuwa usajili wa biashara huongeza uaminifu kwa wateja na taasisi za kifedha, pamoja na kutoa fursa kwa wafanyabiashara kupata huduma mbalimbali zinazotolewa na Serikali na taasisi nyingine.

Kwa upande wake, Afisa Usajili wa Nyaraka Kutoka BPRA Pemba, Nd. Abdalla Ali Abdulla, alitoa maelezo kuhusu aina mbalimbali za usajili wa nyaraka zinazotolewa na BPRA. Alifafanua kuwa huduma hizo zinajumuisha usajili wa hati za mauziano ya ardhi, mikataba, hati za zawadi, wosia na nyaraka nyingine za kisheria zinazohitaji kutambuliwa na kuhifadhiwa kwa mujibu wa sheria.

Wananchi waliohudhuria kikao hicho walipata fursa ya kuuliza maswali na kupata ufafanuzi kuhusu huduma zinazotolewa na BPRA, hatua iliyosaidia kuongeza uelewa wao kuhusu umuhimu wa usajili wa biashara na nyaraka katika kulinda maslahi yao.

Kikao hicho ni sehemu ya juhudi za BPRA za kuendelea kuelimisha wananchi kuhusu huduma zake na kuhamasisha matumizi sahihi ya mifumo ya usajili kwa maendeleo ya kijamii na kiuchumi nchini.

20/03/2026

Address

Mazizini Second Floor Sheria House
Zanzibar

Opening Hours

Monday 07:30 - 15:30
Tuesday 07:30 - 15:30
Wednesday 07:30 - 15:30
Thursday 07:30 - 15:30
Friday 07:30 - 15:30

Alerts

Be the first to know and let us send you an email when Zanzibar Business And Property Registration Agency -BPRA posts news and promotions. Your email address will not be used for any other purpose, and you can unsubscribe at any time.

Contact The Organization

Send a message to Zanzibar Business And Property Registration Agency -BPRA:

Shortcuts

Share