Maendeleo ya Vijana Zanzibar

Maendeleo ya Vijana Zanzibar Contact information, map and directions, contact form, opening hours, services, ratings, photos, videos and announcements from Maendeleo ya Vijana Zanzibar, Public & Government Service, Migombani, Zanzibar.

Idara ya Maendeleo ya Vijana Zanzibar inafanya kazi ya kuratibu shughuli za Maendeleo ya Vijana kwa kuhakikisha idadi ya Vijana wa K**e na kiume wanatoa mchango katika maendeleo ya taifa kiuchumi, kisiasa na kijamii.

04/09/2026
Mkurugenzi idara ya maendeleonya Vijana Zanzibar ndugu Shaib Ibrahim Muhamed akizungumza katika kikao cha pamoja na vion...
22/08/2026

Mkurugenzi idara ya maendeleonya Vijana Zanzibar ndugu Shaib Ibrahim Muhamed akizungumza katika kikao cha pamoja na viongozi wa Shirika la Save the Children waliofika ofisini kwake magomeni Wandaras

Waziri wa Nchi, Ofis ya Makamu wa Pili wa Rais Zanizbar anayeshughulikia Sera, Uratibu na Baraza la Wawakilishi Mhe. Ham...
20/08/2026

Waziri wa Nchi, Ofis ya Makamu wa Pili wa Rais Zanizbar anayeshughulikia Sera, Uratibu na Baraza la Wawakilishi Mhe. Hamza Hassan Juma amesisitiza umuhimu wa kuendeleza kuimarisha ushirikiano wa kufanya kazi na kutoa elimu baina ya Chama cha msalaba mwekundu na wadau mbalimbali katika kazi ya kukabiliana na maafa nchini.

Akifungua kongamano la Kimataifa masuala ya kibinadamu kwa niaba ya Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe.Dkt. Hussein Ali Mwinyi.

Mhe. Hamza amesema Chama cha Msalaba Mwekundu ni kioo cha jamii kwani kwa upande wao yanapotokea maafa kinakuwa mstari wa mbele katika kazi za uokoaji.

Amewataka washiriki wa kongamano hilo kubadili mikakati mbalimbali ili kutoa matokeo mazuri yatakayosaidia katika kutoa huduma mzuri kwa wananchi.

Nae rais wa Chama cha Msalaba mwekundu Tanzania David Mwakiposa Kihenzile amesema kongamano hilo linajadili masuala ya kibinadamu yakiwemo mazingira na mabadiliko ya tabianchi ili kuiweka Tanzania katika hali ya usalama.

Amesema Serikali inahakikisha Dunia na rasilimali zake zinakuwa salama na kuwepukana na maafa.

Kongamano hilo zimeshirikisha nchi Zaidi 20 kutika Mataifa mbalimbali.

MHE. HEMED.....VVYUO  5  VYA UFUNDI NA ELIMU YA AMALI KUJENGWA ZANZIBAR.Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar imechukua hatu...
12/08/2026

MHE. HEMED.....VVYUO 5 VYA UFUNDI NA ELIMU YA AMALI KUJENGWA ZANZIBAR.

Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar imechukua hatua mbalimbali katika kuzipatia ufumbuzi changamoto zinazowakabili vijana kwa kuanzisha Wizara maalum ya Vijana, Ajira na Uwekezaji ili kubuni, kupanga na kusimamia utekelezaji wa programu za maendeleo ya vijana.

Hayo yamesemwa na Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Mhe. Hemed Suleiman Abdulla kwa niaba ya Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe.Dkt Hussein Ali Mwinyi katika Maadhimisho ya siku ya vijana Kimataifa yaliyofanyika katika Ukumbi wa Hoteli ya Golden Tulip Uwanja wa Ndege Zanzibar.

Amesema Serikali kupitia Wizara ya Vijana, Ajira na Uwezeshaji ipo katika hatua za mwisho za maandalizi ya mpango mkakati wa Kitaifa wa uzalishaji wa ajira Zanzibar ambao unajumuisha sekta za Umma na binafsi ili kutoa mchango wao katika uzalishaji wa ajira ndani na nje ya nchi.

Mhe. Hemed amesema Serikali kupitia Wakala wa Uwezeshaji wananchi kiuchumi imetoa zaidi ya shilingi Bilioni 12.7 k**a mkopo wenye masharti nafuu zitakazo wanufaisha wananchi 4,730 wakiwemo vijana .

Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar amesema Serikali imeweka mkazo katika kuimarisha sekta ya elimu, mafunzo ya amali na ubunifu kwa vijana ambapo Bajeti ya Sekta ya elimu imeongezeka kutoka Bilioni 864 kwa mwaka 2025/2026 hadi kufikia zaidi ya Trilioni 1.1 kwa mwaka wa fedha 2026/2027.

Sambamba na hayo Mhe. Hemed amesema Serikali imeimarisha upatikanaji wa mafunzo ya Ufundi na Elimu ya Amali kwa vijana kwa kujenga vyuo saba (7) vya mafuzo ya Ufundi na Elimu ya Amali ambapo vyuo vyengine vitano (5) k**a hivyo vinatarajiwa kujengwa katika mwaka wa fedha 2026/27 pamoja na kujengwa karakana 25 katika Skuli za Sekondari Unguja na Pemba.

Aidha, Mhe. Hemed amesema kwa upande wa Elimu ya juu, jumla ya vijana 18,593 wamepatiwa mikopo ya elimu ya juu ambapo dhamira ya Serikali ni kuendelea kuimarisha elimu ya juu kwa kuongeza bajeti na fursa za upatikanaji wa mikopo kwa wanafunzi wa elimu ya juu Zanzibar kwa kuanzia na ngazi ya stashahada (DIPLOMA).

Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar imechukua hatua mbalimbali katika kuzipatia ufumbuzi changamoto zinazowakabili vijana ...

Kilele cha maadhimisho ya siku ya Vijana Kamataifa katika ukumbi wa  hotel ya Golden Tulip Airport Zanzibar
12/08/2026

Kilele cha maadhimisho ya siku ya Vijana Kamataifa katika ukumbi wa hotel ya Golden Tulip Airport Zanzibar

12/08/2026

Address

Migombani
Zanzibar

Website

Alerts

Be the first to know and let us send you an email when Maendeleo ya Vijana Zanzibar posts news and promotions. Your email address will not be used for any other purpose, and you can unsubscribe at any time.

Contact The Organization

Send a message to Maendeleo ya Vijana Zanzibar:

Shortcuts

Share