Zanzibar Electricity Corporation

Zanzibar Electricity Corporation Shirika la Umeme Zanzibar ni Shirika lenye jukumu la kusimamia uzalishaji, usambazaji na ugawaji ume

13/03/2026

ZECO na NOVAVIS International zatiliana saini mkata wa kumaliza changamoto ya upatikanaji umeme Pemba

KAMPUNI ya NOVAVIS International imetakiwa kukamilisha kwa wakati na kwa ufanisi mradi wa uimarishaji upatikanaji wa ume...
13/03/2026

KAMPUNI ya NOVAVIS International imetakiwa kukamilisha kwa wakati na kwa ufanisi mradi wa uimarishaji upatikanaji wa umeme ndani ya Kisiwa cha Pemba.

Waziri wa Maji Nishati na Madini Zanzibar, Mhe. Nadir Abdullatif Alwardy aliyasema hayo kwa watendaji wa kampuni hiyo mara baada ya kusaini mkataba wa utekelezaji wa kazi hiyo na Shirika la Umeme Zanzibar (ZECO) katika tukio lililofanyika tarehe 12 Machi, 2026 katika ofisi za Wizara ya Maji Nishati na Madini, hapo Maisara Mjini Unguja.

Akieleza lengo la mradi huo Meneja Mkuu Shirika la Umeme Zanzibar, Mhandisi: Haji Haji amesema kuwa kukamilika kwa mradi huo kutaondoa tatizo la uzimikaji wa umeme mara kwa mara jambo ambalo ni changamoto kwa kisiwa cha Pemba.

Alifafanua kuwa kisiwa cha Pemba bado kinapata nishati ya kutosha kwani waya wa baharini uliolazwa kutoka Majani Mapana, Tanga kuelekea Ras Mkumbuu, Pemba bado unatosheleza mahitaji ya Pemba na kufanya kuwa na umeme wa ziada ila changamoto kuu ya kisiwa hicho ni uchakavu wa mfumo wa usafirishaji na usambazaji umeme.

Kwa upande wake Mkurugenzi Mkaazi wa Kampuni ya NOVAVIS International tawi la Zanzibar, Salma Salum Adim ameishukuru Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar kwa kuwaamini tena kuwapa kazi hiyo na kuihakikishia kutekeleza mradi huo kwa ubora ili kujenga Imani zaidi.

Mradi huo ni wa pili kwa ZECO kwani kampuni hiyo ilishatekeleza mradi wa uimarishaji upatikanaji umeme Unguja ambapo vifaa mbali mbali vimefungwa katika mfumo wa usafirishji na usambazaji umeme katika kuongeza nguvu hali ya upatikanaji umeme.
Kazi mbali mbali zinakusudiwa kutekelezwa katika mradi huo ikiwa ni pamoja na kuimarisha kituo cha udhibiti mwendo wa umeme Wesha, kujenga njia ya urefu wa takribani kilomita 310 za usafirishaji umeme, uwekaji wa vifaa vya udhibiti wa mwendo wa umeme na kufanya matengenezo ya miundo mbinu ya umeme ikiwa ni pamoja na kuweka mfumo maalumu wa utambuzi wa changamoto pale tatizo la umeme linapotokezea.

Takribani kiasi cha Dola za Marekani milioni 64 zinakusudiwa kutumika katika utekelezaji wa mradi huo fedha ambazo zinatoka katika vyanzo vya ndani ambapo kazi hiyo itatekelezwa kwa muda wa miaka miwili (2) kuanza rasmini ni Aprili, 2026.
Kukamilika kwa mradi huo kutaondoa changamoto za upatikanaji umeme ndani ya kisiwa cha Pemba.

Imetolewa na;
Kitengo cha Uhusiano, ZECO.

04/03/2026
10/02/2026

WANANCHI wa Matemwe, Pwani Mchangani na Kandwi wamepewa elimu ya awali juu ya uwekezaji wa umeme mbadala utakaozalishwa kwa kutumia nishati ya jua ambao unatarajiwa kufanyika katika maeneo yao.

Waziri wa Maji Nishati na Madini Zanzibar, Mheshimiwa Nadir Abdullatif Alwardy akiongozana na Meneja Mkuu wa Shirika la Umeme Zanzibar, Mhadisi; Haji Haji wamewatoa hofu wananchi wa maeneo hayo kuwa mradi huo ni kwa ajili ya maslahi ya nchi na wananchi wake ambao wananchi wa maeneo hayo ya Matemwe, Pwani Mchangani na Kandwi ni miongoni mwa watakao faidika na mradi huo.

Aidha, wamewatoa hofu wananchi ya kuwa hakuna mwananchi atakayedhulumiwa kupitia uwekezaji huo ambao utazingatia maslahi ya nchi na wananchi wa maeneo hayo.

SERIKALI ya Wilaya ya Kaskazini A Unguja pamoja na Mkoa wa Kaskazini Unguja imezikutanisha Wizara ya Maji Nishati na Mad...
07/02/2026

SERIKALI ya Wilaya ya Kaskazini A Unguja pamoja na Mkoa wa Kaskazini Unguja imezikutanisha Wizara ya Maji Nishati na Madini, ZECO na wananchi wa shehia tatu ya Kandwi, Pwani Mchangani na Matemwe ili kujadili juu ya uwekezaji wa mradi wa nishati ya umeme mbadala unaotarajiwa kufanywa katika maeneo hayo.

Viongozi wa taasisi hizo ambazo zimehudhuria kikao hicho wamewaomba wanachi wa vijiji hivyo kuukubali mradi huo kwa maslahi ya nchi na wananchi wote.

Kikao hicho kimetayarishwa na Mkuu wa Mkoa Kaskazini Unguja, Mhe. Cassian Gallos Nyimbo, kimehudhuriwa na Mhe. Nadir Abdullatif Alwardy, Waziri wa Maji Nishati na Madini Zanzibar, Mhe. Rashid Simai Msaraka, Mkuu wa Wilaya Kaskazini Unguja, Meneja Mkuu Shirika la Umeme Zanzibar, Mhandisi; Haji Haji, Mhe. Sulubu Kidombo, Mwakilishi wa Jimbo la Mkwajuni, Masheha wa Shehia hizo pamoja na wananchi wa shehia hizo.

07/02/2026

Njia hizi zinasaidia kuepukana na majanga ya moto kwenye mifumo ya umeme

04/02/2026

Umuhimu wa kuwa na vyanzo vya kuzalisha umeme ndani ya Zanzibar wawekwa bayana

Address

Zanzibar

Opening Hours

Monday 08:00 - 17:00
Tuesday 08:00 - 17:00
Wednesday 08:00 - 17:00
Thursday 08:00 - 17:00
Friday 08:00 - 17:00
Saturday 08:00 - 12:00

Alerts

Be the first to know and let us send you an email when Zanzibar Electricity Corporation posts news and promotions. Your email address will not be used for any other purpose, and you can unsubscribe at any time.

Contact The Organization

Send a message to Zanzibar Electricity Corporation:

Share