ZBC Zanzibar

ZBC Zanzibar Ukurasa Rasmi Wa Shirika la Utangazaji Zanzibar (ZBC).

Serikali kwa kushirikiana na wadau wa elimu imeendelea kuchukua hatua mbalimbali kuhakikisha wanafunzi wanapata mazingir...
03/09/2026

Serikali kwa kushirikiana na wadau wa elimu imeendelea kuchukua hatua mbalimbali kuhakikisha wanafunzi wanapata mazingira bora ya kujifunzia, ikiwemo upatikanaji wa vifaa vinavyowasaidia kukabiliana na changamoto ya uoni na kuimarisha uwezo wao wa kujifunza.

Akizungumza kwa niaba ya Katibu Mkuu wa Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Amali Zanzibar, Mkurugenzi wa Bodi ya Huduma za Maktaba Zanzibar, Ulfat Abdulaziz Ibrahim, amesema hatua hiyo ni sehemu ya jitihada za Serikali kuhakikisha kila mtoto anapata nafasi na haki ya kujifunza katika mazingira yanayomwezesha kufikia malengo yake.

03/09/2026

Naibu Waziri wa Kilimo, Umwagiliaji, Maliasili na Mifugo Zanzibar, Dkt. Salum Soud Hamed, amesema Serikali ipo tayari kuwaunga mkono vijana wanaojishughulisha na shughuli za kilimo, ikiwemo kuhakikisha wanapata pembejeo za kilimo ili kuwawezesha kuongeza uzalishaji.

Dkt. Salum amesema hayo wakati wa ziara ya kuwatembelea vijana wanaojishughulisha na kilimo katika Shehia ya Mkwajuni, Kidombo pamoja na Kambi ya Vijana Kigongoni, Wilaya ya Kaskazini A’, kwa lengo la kuona shughuli wanazofanya na namna wanavyotumia ubunifu na rasilimali zilizopo katika kuendeleza sekta ya kilimo.

Amesema hatua hiyo itawasaidia vijana kuongeza uzalishaji na kupata tija, huku akiwataka Umoja wa Jumuia na Baraza la Vijana Zanzibar kutumia elimu, ubunifu na mbinu za kisasa katika shughuli za kilimo ili kuchangia maendeleo ya Taifa.

Kwa upande wake, Mwenyekiti wa Baraza la Vijana Zanzibar, Dkt. Mohammed Abraham Juma, amesema ziara hiyo imelenga kubaini changamoto na mahitaji ya vijana wanaojishughulisha na kilimo, ili Serikali iweze kuchukua hatua za kuwasaidia.

Nao vijana wameishukuru Serikali kwa kuwaunga mkono, wakisema wataendelea kutumia mbinu za kisasa na fursa zinazopatikana kuwaelimisha na kuwahamasisha vijana wenzao kujiunga na shughuli za kilimo.

Makamu wa Pili wa Rais Zanzibar Mheshimiwa Hemed Suleiman Abdulla ameongoza kikao kazi kilichojadili hatua za kupambana ...
03/09/2026

Makamu wa Pili wa Rais Zanzibar Mheshimiwa Hemed Suleiman Abdulla ameongoza kikao kazi kilichojadili hatua za kupambana na kujikinga na Mvua za El-Nino zinazotarajiwa kuanza kunyesha kuanzia mwezi Oktoba hadi Disemba, 2026. Aidha, kikao hicho kimepokea taarifa inayoelezea hatua zilizofikiwa za matayarisho ya Mashindano ya AFCON 2027 kutoka kwa K**ati Saidizi za Mashindano hayo.

Kikao hicho kimefanyika katika Ukumbi wa Uchaguzi House, Maisara, Mkoa wa Mjini Magharibi Unguja, tarehe 03.09.2026.

K**ati ya Uongozi ya ZBC imejengewa uelewa kuhusu namna ya kufikia kiwango cha juu cha utendaji katika kutekeleza majuku...
03/09/2026

K**ati ya Uongozi ya ZBC imejengewa uelewa kuhusu namna ya kufikia kiwango cha juu cha utendaji katika kutekeleza majukumu yao, kwa kuzingatia uwezo wa kujituma, tabia na mitazamo chanya katika kazi.

Mkurugenzi Mwendeshaji wa Taasisi ya Peak Performance, Bw. Phillemon C.G. Kisamo, ametoa mafunzo hayo kwa K**ati ya Uongozi ya ZBC, yakilenga kuwajengea uwezo viongozi katika kuboresha utendaji wao na kufikia kiwango cha juu cha ufanisi katika majukumu yao.

Kipindi cha DIRA kipo LIVE muda huu!Host: Ali Kinasa na Aisha Omar Mgeni ni Dickson Senzi, Meneja Mwandamizi – Mahusiano...
03/09/2026

Kipindi cha DIRA kipo LIVE muda huu!

Host: Ali Kinasa na Aisha Omar

Mgeni ni Dickson Senzi, Meneja Mwandamizi – Mahusiano wa Stanbic Bank Tanzania

📺 Washa ZBC Channel 01 kupitia king’amuzi cha BAYT.
Usikose mada mbalimbali zenye kuelimisha na kuburudisha.

🕖 Jumatatu hadi Alhamisi saa 7 kamili mchana
🕗 Ijumaa saa 8 kamili mchana


ANZA SIKU YAKO PAMOJA NA PAMBAZUKO kupitia ZBC Radio.Pata uchambuzi wa mada mbalimbali, habari za magazetini, Habari za ...
03/09/2026

ANZA SIKU YAKO PAMOJA NA PAMBAZUKO kupitia ZBC Radio.

Pata uchambuzi wa mada mbalimbali, habari za magazetini, Habari za Mawio pamoja na matangazo ya vifo ukiwa na Msham Juma na Mwajuma Khamis.

Tufuatilie kupitia Unguja 90.6 MHz na Pemba 94.1 MHz, kuanzia saa 12:00 kamili asubuhi.

Umetazama leo kipindi cha Asubuhi Njema? K**a hujatazama, kipindi kizima kipo kwenye YouTube Channel ya ZBC Zanzibar.🎙Am...
03/09/2026

Umetazama leo kipindi cha Asubuhi Njema? K**a hujatazama, kipindi kizima kipo kwenye YouTube Channel ya ZBC Zanzibar.

🎙Amina Mkombe, Ally Mwaita na Godfrey Hussein na



03/09/2026

Ziara ya wajumbe wa Shirikisho la Soka Afrika (CAF) katika Uwanja wa Fumba na Amaan Complex, Zanzibar, imeongeza matumaini kwa viongozi wa soka nchini Tanzania kuhusu maandalizi ya Mashindano ya AFCON 2027.

Rais wa Shirikisho la Soka Tanzania (TFF), Wallace Karia, amesema ujumbe huo wa CAF umeridhishwa na maendeleo ya ujenzi wa Uwanja wa Fumba, ambao unatarajiwa kukamilika ifikapo Desemba mwaka huu.

Mbali na Uwanja wa Fumba, wajumbe hao wametembelea miundombinu mingine muhimu inayoboreshwa kwa ajili ya maandalizi ya mashindano hayo.

Karia amesema ujumbe huo pia umetembelea maeneo mbalimbali, ikiwemo sekta ya afya, viwanja vya michezo na maeneo ya mazoezi, kwa lengo la kutathmini kiwango cha utayari wa Tanzania katika maandalizi ya AFCON 2027.

Kurasa za juu za Magazeti ya leo Septemba 03 2026.
03/09/2026

Kurasa za juu za Magazeti ya leo Septemba 03 2026.

Address

Zanzibar
Zanzibar
70001

Alerts

Be the first to know and let us send you an email when ZBC Zanzibar posts news and promotions. Your email address will not be used for any other purpose, and you can unsubscribe at any time.

Contact The Organization

Send a message to ZBC Zanzibar:

Shortcuts

Share