Idara ya Habari Zanzibar (ZIS) ni Idara chini ya Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo . Idara ya Habari MAELEZO Zanzibar inajukumu la kutoa taarifa kuhusu Sera, Mipango na utekelezaji wa miradi ya Maendeleo mbalimbali ya Serikali kwa wananchi. Idara imeanzishwa mwaka 1996 baada ya kutenganishwa kwa Sauti ya Tanzania Zanzibar ambayo sasa ni Shirika la Utangazaji Zanzibar kutoka Idara ya H
abari na Utangazaji iliyoundwa baada ya Mapinduzi ya Januari 12 mwaka 1964. Kwa sasa Mkurugenzi wa Idara ya Habari MAELEZO ni Hassan Vuai na Naibu Mkurugenzi ni Dk Juma Mohammed Salum. Kimuundo wa Utawala, Idara imegawika sehemu tano(5) ambazo ndizo zinazounda Kamati ya Uongozi ya Idara k**a ifuatavyo:-
1. Sehemu ya Habari (Editorial)
3. Usajili wa Magazeti na Majarida
4. Sehemu ya Hesabu
S
MAJUKUMU YA IDARA HABARI MAELEZO ZANZIBAR
Majukumu ya Idara hii ni pamoja na :-
1. Kuwa msemaji wa mambo ya Serikali ya Mapinduzi Zanzibar
2. Kuiwekea Serikali kumbukumbu katika kutayarisha na kutoa vielelezo vya sinema, video, majarida, vitabu vya taaluma, tamthilia na burudani.
3. Kusimamia utekelezaji wa Sera ya Habari ya Zanzibar na sheria Na. 5 ya mwaka 1988 inayohusiana na mambo ya vitabu na Magazeti
4. Kutetea msimamo wa Serikali katika kupambana na habari na tuhuma zinazotolewa na vyombo vya habari vya ndani na nje ya nchi dhidi ya Serikali
5. Kuishauri Serikali kuhusu nyendo za vyombo vya habari na kupendekeza hatua muafaka za kuchukuliwa
6. Kusimamia, kutoa au kuzuia vibali vya uanzishwaji wa magazeti na majarida mbalimbali Zanzibar
7. Kusimamia kutoa vitambulisho kwa waandishi wa Habari na wapigapicha wa ndani na nje ya Zanzibar watakaofanya kazi Zanzibar
8. Kuwaelekeza waandishi wa habarui watakaofanyakazi hapa Zanzibar maadili, maeneo na mipaka yao na utendaji