PPP Centre Tanzania

PPP Centre Tanzania Welcome to PPPC Page!We forge impactful partnerships between Public and Private sectors.

Maandalizi kuelekea kongamano la Ubia kati ya Sekta ya Umma na Binafsi na nafasi yake katika kuleta mageuzi katika sekta...
06/06/2026

Maandalizi kuelekea kongamano la Ubia kati ya Sekta ya Umma na Binafsi na nafasi yake katika kuleta mageuzi katika sekta ya Afya Nchini yamekamilika.

Kongamano linatarajiwa kuanza hivi karibuni katika ukumbi wa CHPE katika Chuo Kikuu cha Muhimbili, Dar es Salaam.

“Taxes and loans alone can not fund the mega-infrastructure—modern rail, ports, and hospitals—required for Tanzania’s De...
06/04/2026

“Taxes and loans alone can not fund the mega-infrastructure—modern rail, ports, and hospitals—required for Tanzania’s Development Vision 2050.

The PPP-Centre’s legal frameworks give these investors the confidence to safely inject private trillions into our public projects while protecting national resources.”

​ David Kafulila, Executive Director of the PPP-Centre

MATUKIO: MHADHARA WA WAZI.​Kituo cha Ubia kati ya Sekta ya Umma na Sekta Binafsi (PPPC), kwa ushirikiano na Chuo Kikuu c...
06/03/2026

MATUKIO: MHADHARA WA WAZI.

​Kituo cha Ubia kati ya Sekta ya Umma na Sekta Binafsi (PPPC), kwa ushirikiano na Chuo Kikuu cha Dodoma (UDOM), kimeandaa Mhadhara wa Wazi uliofanyika leo chuoni hapo.

​Mhadhara huo umelenga kujadili nafasi na mchango wa Ubia kati ya Sekta ya Umma na Sekta Binafsi (PPP) katika kufikia malengo ya Mpango wa Nne wa Maendeleo wa Miaka Mitano (FYDP IV) kuelekea Dira ya Mwaka 2050.

06/03/2026

KAFULILA ANOGESHA MJADALA WA VYUO VIKUU KUFUNDISHA PPP.

Mkurugenzi Mtendaji wa Kituo cha Ubia kati ya Sekta ya Umma na Binafsi (PPP-Centre), David Kafulila ameahidi kufanya kila kinachowezekana kuhakikisha Chuo kikuu Cha Dodoma (UDOM) kinaanza kutoa shahada ya uzamili ya Ubia wa Sekta ya Umma na Binafsi (Masters of Public-Private Partnership (PPP).

Akizungumza katika mhadhara wa umma ulioandaliwa na UDOM leo Jumatano (Juni 3, 2026) chuoni hapo, Kafulila amesema kuwa kuna nchi chache duniani zinazotoa programu hiyo huku akiitaja Malaysia k**a miongoni mwa nchi zinazotambulika zaidi duniani kwa utoaji wa programu ya PPP.

Kafulila amesema kuanzishwa kwa programu hiyo kutasaidia kujenga wataalamu wenye ujuzi wa hali ya juu katika masuala ya ubia kati ya sekta ya umma na binafsi, jambo litakalochangia maendeleo ya kiuchumi na utekelezaji wa miradi ya kimkakati nchini.

Aidha, ameeleza kuwa uwepo wa programu ya PPP chuoni hapo utaimarisha uwezo wa nchi kuzalisha wataalamu wa ndani watakaosaidia kusimamia na kuendeleza miradi ya ubia kwa ufanisi zaidi, sambamba na kukuza mchango wa sekta binafsi katika maendeleo ya taifa.

06/01/2026

PPP Yaleta Mapinduzi Katika Huduma za Hijja Makka – KafulilaMkurugenzi Mtendaji wa PPP-Centre, David Kafulila amesema mf...
05/27/2026

PPP Yaleta Mapinduzi Katika Huduma za Hijja Makka – Kafulila

Mkurugenzi Mtendaji wa PPP-Centre, David Kafulila amesema mfumo wa Ubia kati ya Sekta ya Umma na Binafsi (PPP) umeleta mageuzi makubwa katika huduma za Hijja nchini Saudi Arabia kwa kuongeza ufanisi na kupunguza adha kwa mahujaji.

Akitoa salamu za Eid al-Adha kwa Waislamu duniani, Kafulila amesema moja ya mafanikio makubwa ya PPP ni maboresho yaliyofanyika katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa King Abdulaziz (KAIA) uliopo Jeddah, unaotumiwa na mamilioni ya mahujaji wanaoelekea Makka.

Amesema kabla ya maboresho hayo, mahujaji walikuwa wakitumia kati ya saa sita hadi 10 kukamilisha taratibu za uwanjani, lakini baada ya utekelezaji wa mradi wa PPP wenye thamani ya dola milioni 249, muda huo umepungua hadi dakika 45 na saa moja.

“PPP imeongeza ufanisi mkubwa sana. Kabla ya mradi huu, uwanja ulikuwa ukihudumia wastani wa mahujaji milioni moja kwa mwaka, lakini sasa unahudumia kati ya abiria milioni nane hadi tisa kwa mwaka,” amesema Kafulila.

Kafulila amefafanua kwamba, mradi huo ulitekelezwa kupitia mkataba wa miaka 20 kati ya Mamlaka ya Anga ya Saudi Arabia (GACA) na kampuni binafsi ya Hajj and Umrah Terminals Development Company, ukihusisha Saudi Binladin Group pamoja na Aéroports de Paris Management huku Shirika la IFC likiwa mshauri mwelekezi.

Mafanikio hayo yanapaswa kuwa somo kwa Tanzania katika kuendeleza sekta ya usafiri wa anga na miundombinu mingine kupitia uwekezaji wa PPP.

“Tusiogope kuwakaribisha wawekezaji kupitia PPP kwenye viwanja vyetu vya ndege ili kuongeza ufanisi wa huduma na kuchochea mageuzi ya kiuchumi,” amesema.

Aidha, amesema tathmini ya usafiri wa anga duniani ya mwaka 2023 inaonyesha kuwa licha ya viwanja vya ndege vinavyoendeshwa kwa PPP kuwa asilimia 14 pekee duniani, vinahudumia karibu asilimia 40 ya abiria wote duniani.

“PPP na ufanisi ni pacha,” amesema Kafulila huku akiwatakia Waislamu wote Eid Mubarak yenye amani na baraka.

A snapshot of eight mega infrastructure projects currently under implementation through the Public-Private Partnership (...
05/25/2026

A snapshot of eight mega infrastructure projects currently under implementation through the Public-Private Partnership (PPP) Framework in Tanzania.

These strategic investments span transport, logistics, urban mobility, commercial infrastructure, and more.

For more information, visit: www.pppcentre.go.tz

Chini ya mfumo wa Ubinafsishaji na Ushirikiano kati ya Sekta ya Umma na Sekta Binafsi (PPP), Kituo cha PPP cha Tanzania ...
05/23/2026

Chini ya mfumo wa Ubinafsishaji na Ushirikiano kati ya Sekta ya Umma na Sekta Binafsi (PPP), Kituo cha PPP cha Tanzania kwa kushirikiana na Shirika la Reli Tanzania (TRC) kinaendeleza mradi unaopendekezwa wa Reli ya Kiwango cha Kimataifa (SGR) kutoka Mtwara–Mbamba Bay–Mchuchuma/Liganga wenye thamani ya dola bilioni 5.6.

​Ukanda huo wa reli wenye urefu wa takriban kilomita 1,000 umesanifiwa kuunganisha Bandari ya Mtwara katika Bahari ya Hindi na Mbamba Bay katika Ziwa Nyasa, kukiwa na njia za kimkakati zinazojinyoosha hadi kwenye miradi ya mkaa wa mawe wa Mchuchuma och chuma cha Liganga kusini-magharibi mwa Tanzania.

​Ukiwa umeundwa chini ya mtindo wa PPP wa DBFOMT ( Design, Build, Finance Oparate, Maintain and Transfer) na kufunguliwa rasmi kwa ukandarasi wa ushindani, mradi huo wa reli unatarajiwa kufungua uwezo mkubwa wa sekta ya kilimo, madini, lojistiki, na biashara kusini mwa Tanzania, huku ukitengeneza ukanda mpya wa kiuchumi katika moja ya mikoa yenye rasilimali nyingi zaidi nchini.

​Aidha, mradi huo unaweka Tanzania katika nafasi ya kuwa kitovu kinachochipukia cha usafirishaji na viwanda kikanda, kikisukumwa na ushiriki mkubwa wa sekta binafsi katika maendeleo ya miundombinu ya kimkakati.

Address

Government City-Mtumba, Hazina Street
Auburn, WA

Alerts

Be the first to know and let us send you an email when PPP Centre Tanzania posts news and promotions. Your email address will not be used for any other purpose, and you can unsubscribe at any time.

Contact The Organization

Send a message to PPP Centre Tanzania:

Share